TARURA, hii biashara mliyoanzisha ya maegesho ya kulipia kwanini msingetenga na kuandaa maeneo maalum badala ya kutumia barabara zetu?

TARURA, hii biashara mliyoanzisha ya maegesho ya kulipia kwanini msingetenga na kuandaa maeneo maalum badala ya kutumia barabara zetu?

fatakifataki

Senior Member
Joined
Nov 2, 2009
Posts
134
Reaction score
60
Kwanza nawapa kongole mamlaka ya usimamizi wa barabara za mjini na vijijini (TARURA) kwa kuanzisha na kurahisisha huduma za parking kwa njia ya kulipia hususani maeneo ya miji na majiji makubwa hapa nchini.

Mapungufu makubwa niliyoyaona hapa ni Parking space nyingi ziko katika barabara ambazo zingepaswa kutumika mfano unakuta barabara ziko mbili lakini TARURA wamewapa reserve parking watu katika upande wa barabara almost moja na kisha ile iliyopaswa kutumika kama barabara nzima ya njia mbili sasa wananchi tunabanana kwenye njia moja.

Mfano mtaa wa lumumba Mwanza n.k

Pili hata hizi parking za pembeni ya barabara TARURA zinafinya njia na kusababisha msongamano ingawa mradi huu unaongeza wigo wa mapato ya serikali.

Tatu nashauri sasa jengeni maeneo maalum ambayo watu watapaki magari na kuendelea na huduma hii bila kusababisha mbanano au msongamano mijini ambao wakati mwingine unawaletea shida kutokana na ufinyu sasa uliotokana na huduma hizi.
 
Tena mlipe sana tu huko Mwanza. Maana yule kichaa alikuwa anawalea sana akidai ndiyo ninyi mlimpigia kura.

Mkabila yule aliboa nchi na dunia kwa ujumla
Dunia alibomoa vipi we kenge..hasira na chuki hazito kusaidia wakati kila siku ukipita ubungo flyover karoho kana kusuta na kukiri moyoni jpm alikua rais mpenda maendeleo.

#MaendeleoHayanaChama
 
Tena mlipe sana tu huko Mwanza. Maana yule kichaa alikuwa anawalea sana akidai ndiyo ninyi mlimpigia kura.

Mkabila yule aliboa nchi na dunia kwa ujumla
Mwanza ni mtaa upo Dsm si mwanza jijini
 
Miji imeshajaa watajenga wapi? Nje ya mji hakuna atayeenda kupaki kwa hiyo ni kuibiana tu, barabara zinakuwa za njia moja na misongamano isiyokuwa na sababu,
Magu angekuwepo asingekubali huu upuuzi
 
Nashauri TARURA kila gari lililokwisha ingia katika huduma za parking lifunguliwe account kama ilivyo kwa huduma za maji, mteja(mwenye gari) kulipia shilingi 500 au 1000 kwa simu inakuwa na kausumbufu, wengine twasubiri deni likue kue hadi zaidi ya 5k.

Fanyeni utaratibu mmiliki/dereva akiamua kuwekamo 10k ama zaidi iwe inatumika hadi iishapo (prepaid)
 
Hivi hii biashara ya parking inalipa? Mwenye uelewa anisaidie
 
Back
Top Bottom