TASAF inatumia Tshs Bilioni 900 kuhudumiwa watu milioni 5

TASAF inatumia Tshs Bilioni 900 kuhudumiwa watu milioni 5

Tatizo la ccm ni kuabudu watu, hawafatagi ilani yao zaidi ya mawazo ya walio juu yao.
 
naona mme anza kuchanganyikiwa unaleta Habari za TASAF saiv wakati ipo toka kipindi cha kikwete . Elfu 30 ina saidia nini sasa kukwamua umaskini
Mleta mada anafurahia umaskini.

Takwimualizoziweka tu ni ushahidi tosha kwamba wimbi la umaskini linaongezeka au TASAF haina dira.
 
Sijamaanisha wewe unaumia ila Nimemaanisha mtoa mada hajui jinsi wengine tunaumia yeye anavyosifia ni kama vile kazi kaifanya mtu mmoja wakati watu wanalipa kodi ndo hizo pesa zinatumika kuleta huduma.
Hawa watu wengine ama wana akili fupi sana, ama ni wazandiki wasiojali watu.

Yote majanga.
 
Hawa watu wengine ama wana akili fupi sana, ama ni wazandiki wasiojali watu.

Yote majanga.
Ukila keki ya taifa nadhani unakuwa humjui mwenye njaa.
Tangu 2015 tunasota hafu mtu anakuja kusifia sifa ambazo ukiangalia si zakweli, wasifanye hivi!
 
Ukila keki ya taifa nadhani unakuwa humjui mwenye njaa.
Tangu 2015 tunasota hafu mtu anakuja kusifia sifa ambazo ukiangalia si zakweli, wasifanye hivi!
Hizi ni tabia tu mara nyingine.

Kuna watu wanakula vumbi tu halafu wanasifia watawala.

Wakati sisi wenyewe tuliopata nyumba za Oysterbay hazitufanyi tushindwe kusema ukweli.
 
Hizi ni tabia tu mara nyingine.

Kuna watu wanakula vumbi tu halafu wanasifia watawala.

Wakati sisi wenyewe tuliopata nyumba za Oysterbay hazitufanyi tushindwe kusema ukweli.
😅😅😅😅😅kaka sidhani ila maisha haya yalivyo magumu kwetu, unasikia tu taarifa za CAG hafu kimya na kusifia inauma sana..kiumweli watu walio kwenye mnyororo wanakula pesa.
Acha wengine sisi tupambane kupata mkate.
 
Wangetengeneza mazingira ya kupunguza umasikini Tanzania hizi mambo za kugawa cash itapungua sana na pia hela nyingi zinapotea huko kwenye kukagawana...
 
Moja ya shabaha kuu iliowekwa na Dira 2050 ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2050 Taifa letu liwe limetokomeza kabisa umasikini uliokithiri, ambapo kwa mujibu ripoti ya Benki ya Dunia (2025) Asilimia 26 ya watanzania linaishi katika kundi hili, Katika kupambana kuwatoa wananchi wanaoishi katika lindi la umasikini.

Rais Samia amefanya jitihada mbalimbali ikiwa ni Pamoja na, kuongeza kiwango cha fedha kwa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF) inayohudumia wananchi wanaoishi katika kaya masikini waweze kumudu gharama za mahitaji yao ya kila siku.

Ambapo Rais aliongeza fedha katika mfuko huo kutoka TZS580.2bn mwaka 2020 hadi TZS962bn mwaka 2024 jitihada hizi zimesaidia kuongezeka kwa idadi ya wanufaika kutoka 5,000,000 na kufikia 5,202,655 mwaka 2024, sawa na ongezeko la wanufaika wapya 202,655. Jitihada na uwekezaji huu katika kuwanusuru kaya masikini ni msingi mzuri wa kutimiza shabaha ya dira 2050 inayolenga kutokomeza umasikini uliokithiri kwa makundi yote miongoni mwa watanzania.
Hongera sana Rais Samia
 
Back
Top Bottom