Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO) inawatangazia abiria na umma wote kwa jumla kuwa meli ya New Victoria Hapa Kazi Tu itaanza safari zake rasmi siku ya Alhamisi tarehe 22 Mei 2025 ikitokea Bandari ya Mwanza Kaskazini kuelekea Bandari ya Bukoba kupitia Bandari ya Kemondo.
Hivyo kampuni inawakaribisha abiria wote kufika bandarini Saa 1:30 Jioni au kabla ya muda huo kwa ajili ya maandalizi ya safari na meli itaondoka saa 3:00 usiku.