Prof Koboko
JF-Expert Member
- Aug 15, 2020
- 350
- 2,550
Nchi hii sijui imelaaniwa wapi, ni juzi tu Rais wetu mpendwa Mama Samia aliwaonya Task forces TRA waache kutumia nguvu kudai kodi lakini usiku huu wamevamia Mpo Afrika bar iliyopo Temeke na kubeba crates za bia wakiwa wameambatana na polisi wengi wenye silaha.Hivi unapomvamia biashara ya mtu usiku huu na kubeba vitu vyake, kesho analipaje kodi?
Unashindwa nini kumwandikia mmiliki wa Bar barua kesho aje ofisini kumweleza tatizo lake ili ajue? Kuvamia biashara yake usiku wa manane na kuchukua bidhaa zake ndio utatuzi wa tatizo?
Mama Samia Rais wangu ulisemahutaki kodi ya dhuluma, hawa wametumwa na nani huyo asiyekusikia Mama?
Meneja wa TRA mkoa wa kodi wa Temeke na Kamishna mkuu wanatakiwa kufukuzwa kazi, huu tunahesabia kama uporaji wa mali za watu.