Mpigamaji
Senior Member
- Oct 24, 2018
- 152
- 244
Kwenye uchaguzi uliofanyika 28/Oct kweli nilikua natarajia Magufuli atashinda japo siyo kwa % nyingi kama alizokua anatamka Polepole na zilizotangazwa kumpa ushindi. Hivyo sijaona maajabu hapa kwa Urais wake labda hizo 84% tu. Zile nafasi za wabunge waliopita bila kupingwa majimbo 28 zilikua ni sehem tayari ya kuhakikishia ushindi kwa mgombea wa Urais, maana kazi kubwa iliyokua imebaki ni kumnadi mgombea Urais na madiwani tu. Pia wale wanaopita bila kupingwa ukifirikia hilo jina wanaloitwa kwa tafakari unaona ina impact sana katika kuwapa kura wagombea wa nafasi zingine wa chama husika kweny hayo maeneo.
Kilichoshangaza wengi zaidi ni kwenye nafasi za wabunge, kuna wengi najua tuliweka probabilities kwa baadhi ya wabunge wenye majina makubwa wa upinzani kutorudi na wengine kurudi bungeni. Lakini matokeo yametoa utafauti mkubwa sana ambao umeleta mshituko miongoni mwa wagombea, wapiga kura na hata nchi jirani na jumuiya za kimataifa. Kuamini kwamba kweli wameshinda ubunge wapinzani wawil tu ni ngumu sana kuiamini. Ndipo dhama ya kuamini wizi wa kura umefanyika.
Kwa jinsi inavyostaajabisha najua kuna viongozi wa CCM na hata wanachama wanaona aibu kwa kilichofanyika, na hili halileti taswira nzuri sana kwa yajayo ndani ya chama. Nilimsikiliza mchambuzi mmoja wa mambo ya kisiasa akisema "itakua ni changamoti sana kwa serikali ijayo kutekeleza ilani, maana wapo wenyew tu hamna mawazo mbadala wala hakuna kizuizi kama walivyosema kweny kampeni kuwa wapinzani wanachelewesha maendeleo".
Hiki chama badala ya kujengeka zaidi tutarajie mpasuko ndani ya chama. Nachukulia mfano ambao upo kweny maisha ya kila siku, ndugu wengi wakikaa karibu karibu huwa familia inakua na migongano sana mara huyu kamsengenya yule mara tuhuma za kulogana mara hivi mara vile.
Hizi huwa ni kutokana na kukosa mtu au watu ambao wanakua kama ndo common enemy matokeo yake wanakua adui wao kwa wao ndicho kitatokea kwa CCM awamu hii. Watokea watu wataanzisha chama chao kipya na watakua na nguvu sana kwa chaguzi zijazo. 2025 naiona CCM iliyo na makundi na iliyogawanyika kama ya 2015