Kwa nyongeza tu... hivi ndivyo entertainment business inavyoenda! Ukiwa msanii ukaingia kwenye mkataba wowote wakati hujui utapata nini na utapoteza nini na compensation ya unachopoteza itakuwa vipi... basi hesabu umeumia!
Usipofahamu hilo, ndipo pale utasikia Mzee Mutta (wa FM) ni mtu wa dhuluma... kumbe tatizo sio Mzee Mutta bali watu walioingia Mkataba na Mutta hawakufahamu watapata nini na watapoteza nini!!!
Pole sana Saida Karoli, ulikuwa na watu wasiofahamu haya mambo yanaendaje!!!
Mkataba wa Diamond na Vodacom as brand ambassador tayari ulishaingiza mgongano wa kimaslahi kwa shughuli zote ambazo zingefanywa na Washindani wa kibiashara wa Vodacom.
Case study hapa ni Fiesta!
Kwavile Fiesta mwaka huu ilidhaminiwa na Tigo; tayari ilishaleta mgongano wa kimaslahi kwa Diamond kwa kuwa Tigo ni mshindani wa Vodacom!!!
But Diamond nae muziki ndio kazi yake... sasa kama asishiriki Fiesta kwavile tu mdhamini ni mshindani wa kibiashara wa Vodacom... what next?! Nami nazitaka pesa za Fiesta halafu wewe unaniambia nisishiriki!
Jibu ni very simple: Tunakuandalia show ya kwako! Unakosa Fiesta na pesa zake unapata Vodacom Beach part na pesa zake!!
Tunapiga hatua kubwa hivi sasa kwenye tasnia ya burudani na kwa hilo ni wakati sasa wa kuwa na entertainment lawyers vinginevyo wasanii wataendelea kukosa haki zao nyingi sana huku wenyewe wakidhani wanapiga pesa!