Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 143,138
- 288,731
Baada ya kufanya upembuzi yakinifu kuhusu siasa za Tanzania nimeona kwa macho yote kwamba Chama cha siasa cha kisasa cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Ndio chama kilichotamba mitandaoni kwa kujadiliwa mara nyingi zaidi kuliko chama chochote cha kisiasa nchini Tanzania, huku kwa mbali kikifuatiwa na chama cha ACT WAZALENDO , hasa baada ya kumsajili Jabali Maalim Seif, kilichoshangaza ni nafasi ya 3 kushikwa na Jeshi la Polisi hasa kutokana najeshi hilo kuvunja katiba ya nchi makusudi kwa kuwakamata wanasiasa hata kwenye masuala halali ya kisiasa , kitendo ambacho kimetafsiriwa kama ni jeshi hilo kuchukua nafasi ya CCM, hasa baada ya chama hicho kuishiwa hoja na kubaki na vitisho pekee.
Je ni kwanini mara zote Chadema inatamba kwenye mijadala mingi kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari dunia nzima?