Tathmini: Hofu ya Zanzibar kumezwa kwenye Muungano yaongezeka kwenye awamu hii ya tano

Tathmini: Hofu ya Zanzibar kumezwa kwenye Muungano yaongezeka kwenye awamu hii ya tano

Kuna mwenye kujua matumizi ya kitambulisho cha mzanzibar?
 
KISHADA,
Awamu hii ya 5 muungano umeimarika sana.

Angalia bungeni kuko shwari kabisa hata CUF wenyewe wameshaona umuhimu wa kuelekea kwenye serikali moja badala ya tatu.
Ndiyo mbavyojidanganya, wale wabunge wa CUF waliochaguliwa na wananch mliwavua ubungu mkaweka wabunge wenu wa viti maalum. Mkiona watu wako kimya msifikiri wanafuraha.
 
Zanzibar ni wanafiki waache wamezwe na ikiwezekana Rais Magufuli aiwafanye kuwa mkoa kabisa,wazanzibar kipindi cha bunge la katiba nao walichangia sehemu kubwa ya kutokupatikana katiba mpya iliyokuwa inawapeleka kwenye serekali yao halisi ambayo isingekuwa serekali tegemezi kwa serekali ya Tanganyinga, wao ndio waliokubali kuwa daraja la akina Meghiji na mamuruki wenzake kupiga kura kama wazanzibar Wakati siyo wanzanzibar hata wazanzibar waliotaka kwenda pamoja na wananchi waliwafukuza bungeni na kuwafuta kazi kabisa.
 
Tatizo Kuu la Wazanzibar kupewa Uhuru wao sio Tanganyika bali ni CCM.Sisi Watanganyika hatuna tatizo kabisa Zanzibar wawe huru,wajitegemee.Figisu zipo kwenye chama dola CCM!
 
Kati ya jambo la maana ambalo Magu atalifanya ni kufutilia mbali huu muungano wa kijinga na kuifanya Zanzibar mkoa wa Tanganyika, japo simkubali nitaunga mkono atawale hata miaka 20

Wazanzibari wanamiliki ardhi kwetu huku, sisi haturuhusiwi kumiliki kwao, sasa hapa atakayemmeza mwenzake ni nani?

Na bado wanatulalamikia kila mara
 
Zanzibar haitakuwa mkoa abadan ila itaendelea kutawaliwa na Tanganyika kwa mgongo wa Muungano mpka pale wazanzibar watakapokuwa wamoja. Hakuna chengine chochote kitakachoipa Zanzibar uhuru wake zaidi ya Umoja. Lakini kuna kazi kubwa sana ya kupatikana umoja wa Zanzibar maana Watanganyika wanatumia mbinu ya divide and rule. Wazanzibar wanagaiwa kwa siasa, ukabila na dini. Kwenye nyanja ya siasa CCM wa Zanzibar wanaaminishwa kuwa Zanzibar ni milki yao maana wao ndio waliopindua hivyo hakuna chama chengine chochote chenye hali yakushika dola, hata hivyo pamoja na kuaminishwa hivyo bado hali inakuwa ngumu sana siku za uchaguzi na wanashindwa kwa kura lakini Mtanganyika anatumia nguvu kukibakisha chama cha Mapinduzi (Rejea uchaguzi wa 2015). Pia Watanganyika wanatumia ukabila wa kuwagawa wazanzibar kwa kutumia upemba na Uunguja. Wanaleta propaganda ya kuwa wapemba ni hizbu na kukinasibishwa CUF ambayo sasa ni ACT wazalendo kuwa ni chama cha mahizbu hivyo hawana haki ya kutawala. Pia wanajaribu kujenga hoja ya kuwa CUF now ACT kuwa una wafuasi wake pemba tu ili waweze kuhalisha wizi wa kura katika majimbo ya Unguja kitu ambacho sikweli kwani 2015 CUF na CCM walipata majimbo sawa ya uchaguzi. Mwisho kabisa wanaendelea kuitawala Zanzibar kwa kigezo eti Zanzibar ikiwa huru inaweza kuwa kituo cha kigaidi kwa sababu tu 99% ya watu kule ni muslims fikra ambayo ni dhaifu sana. So siku wazanzibar wakiungana pamoja wanaweza kujikomboa katika dimbwi la ukoloni na kuwa huru.
Zanzibar ikiwa huru , hakuwezi kuibuka Muslim extremists? Sasa hivi japo tupo kwenye muungano bado wanakamata watu wanakula mchana na kufunga biashara kibabe

Muungano ukifa nadhani watachoma makanisa na kufukuza watanganyika wote waliopo kule
 
.
Hili sio kweli. Kumbuka kanisa la mwanzo katika ukanda huu lilijengwa Zanzibar katika miaka ya mwisho ya 1800. Iweje leo 2019 makanisa yachomwe? Tunapaswa kufikiri vyema.
 
CCM wanadhani Maalim Seif ndiye tatizo lao, kumbe ni wazanzibari wote hata walioko ccm.
 
Tatizo la Zanzibar ni CCM.
Hii ni sahihi kwani ASP+TANU=CCM
lakini African Associatin(AA)+Shirazi Association (SA)=ASP
sasa hawa AA waliwazidi wenzao kete ,kwani wao asili yao ni Tanganyika na ni Wakristo kwa asili,na wengine walibadili majina na dini kimtindo ili kuwazuga wenzao.
Hatimae wakaichukua ASP wakaipeleka Tanganyika na kuwa CCM.
wale wote waliokuwa SA wamehamia upinzani na ndo maana hawapewi nchi.
Sasa Plan ni kuimaliza Zanzibar ili iwe Nchi moja tuu.
Pengine wamefanikiwa 80%,lakini bado pumzi ya upinzani bado ipo
1572525271021.png
 
Mkuu we unaishi wapi??? ZANZIBAR
Kwa takribani wiki moja na ushei hivi, tulipiga kambi Zanzibar na kubahatika kupata udadisi wa kinachoendelea. Zanzibar kunaonekana kuko shwari kwa nje nje lakini kwa ndani utapata kujuwa hasa nini kinaendelea.

Maelezo yafuatayo yatasaidia kutoa picha halisi kwa tahmini ya Mwandishi na kile alichokiona.

Tathmini hii ibaki kuwa ni ya Mwandishi mwenyewe na haihusiani na taasisi au mamlaka yoyote.

HOFU YA ZANZIBAR KUMEZWA KWENYE MUUNGANO KWENYE AWAMU HII.
Hio hofu ipo juu sana. Mwandishi alipata ufafanuzi mbali mbali kutoka vyanzo tofauti na kubaini kuwa kuna hofu kuu. Hofu hii iko ndani ya SMZ yenyewe na hata kwa wananchi wa kawaida.

Kupitia vyanzo hivyo kuna malalamiko kwa baadhi ya Viongozi ndani ya SMZ na watendaji kulalamikia kuhusu Zanzibar kupoteza nguvu zake ndani ya Muungano na kukosa baadhi ya mashirikiano licha ya mapambio yaliyopo. Mifano ya wazi iliyotolewa kwa siku za karibuni ni SMT kushindwa kusaini mkopo ambao ungeisadia Zanzibar kujenga Bandari yake eneo maarufu la MPIGA DURI. Bandari hii imeahidiwa kwenye ilani ya CCM ya 2015 - 2020.

SMZ kukosa mashirikiano ya JMT kuhusu uimarishwaji wa ujenzi wa uwanja wa Ndege eneo la kukaa Abiria ambapo mradi huo hadi sasa haujakamilika.

Kuna malalamiko mengine mengi kuhusu ushirikishwaji wa Zanzibar kwenye mambo kadhaa ambayo maamuzi yake huathiri moja kwa moja mamlaka za Zanzibar. Kwa Mfano Mwandishi alibaini mvutano uliopo baina ya TFF na ZFF. Licha ya kuwa Michezo si suala la Muungano, TFF inalalamikiwa kwa kuhodhi Utambulisho wa Tanzania na kufaidi misaada ya maendeleo na kuiacha Zanzibar pweke.

Mwandishi alibaini kuwepo mgogoro unaofukuta kati ya TFF na ZFF. Aidha aliweza kubaini kufanyika hatua za makusudi kutoka pande mbili ili kutuliza hali.

Vile vile hofu ipo hata katika ulingo wa siasa za CCM yenyewe kama chama tawala. Mwandishi aliweza kubaini kuibuka kwa kambi za CCM Zanzibar. Kilichopo ni Urais baada ya Dr Shein. Ndani ya Serikali na kwenye Chama kuna kuwindana kwa kambi hizo.
Mwandishi amebaini kuwepo Kambi kuu mbili moja ikijinasibisha na Uungwaji mkono kutoka Bara na Moja ikijibainisha na Uzanzibari. Kwa maana kwamba CCM Zanzibar wana kilio cha muda mrefu cha kutaka mgombea atokane na maamuzi ya Zanzibar yenyewe na sio maamuzi kutoka upande wa Bara.

Kilichobainika CCM Zanzibar inaona hatari iliyopo ya kupatiwa mgombea kutoka Bara na hivyo kutokuwa na Uzalendo wa Maslahi ya Zanzibar kwenye Muungano. Pamoja na kwamba wote wana itikadi moja na ilani moja liunapokuja suali la utashi ndipo hofu ilipo.

Lengine ni hofu ya Utawala uliopo kwenye Muungano na maamuzi yasiyotabirika. Hili nalo lipo. Kuna hofu ndani ya watendaji SMZ na kwenye CCM kwamba Zanzibar kunahitajika Kiongozi Imara na shupavu ambaye atakuwa na uthubutu wa kuipigania Zanzibar. Taarifa zinabainisha kwamba kwa miaka ya hivi karibuni kumekosekana haiba hio na kila kitu kuhusu Zanzibar kukosa nguvu. Jambo hili linaleta lawama hata kwa Uongozi wa SMZ uliopo sasa. Hali hio inazidisha uvumi kwamba sasa Zanzibar inakwenda kuwa Mkoa moja kwa moja.

Utawala wa Rais Magufuli wa Kufanya Maamuzi ya Haraka nao unatia hofu wanasiasa wa Zanzibar kwa baadhi ndani ya CCM na nje ya CCM.

Kwa upande wa WANANCHI WA KAWAIDA, nako kuna hofu za aina hio. Wananchi wengi wengi wanakutajia moja kwa moja mtazamo wao. Ukigusa suali tu nafasi ya Zanzibar kwenye Muungano ni ipi ? unakutana na majibu yaliyofanana. HAIPO. na hicho kidogo kilichokuwepo kinakwenda kupotea . Hayo ndio majibu. Wananchi wengi mwandishi aliokutana nao wanatoa mifano ya Kutotambuliwa Kitambulisho cha Mzanzuibar Mkaazi kwenye mambo ya kitaifa kama Passpoprt na Usajili wa Laini za Simu na hivyo kuhitimisha kudhoofu kwa utambulisho wa Zanzibar kwenye Muungano na kupoteza hadhi yake. Mambo ni Mengi muda NI MCHACHE.

Lengine linalozungumzwa ni kukosekana Sauti ya UPINZANI Zanzibar kuwa nalo linazidisha HOFU ya Zanzibar kumezwa kwenye Muungano. Hapa kila mmoja anamlaumu Mwenzake. Mwandishi alibaini baadhi ya Wananchi kuwalaumu viongozi wa Upinzani kwa kususia na kuwaacha CCM peke yao jambo ambalo wanabainisha kuwa hawana nguvu za kuitetea Zanziubar. Wengine wanawalaumu CCM kwa kushindwa kuisimamia Zanzibar kwenye Muungano.

Kwa ufupi Zanzibar kuna Hofu kubwa ya Kumezwa na kupotea kwenye Muungano na Mwandishi amebaini tiketi muhimu kuelekea chaguzi za 2020 ni Kuhusu ; Uzalendo wa Zanzibar" hili liko ndani ya CCM na upinzani vile vile.

Hio ndio tathmini ndogo ya hali ya Zanzibar kuhusu Muungano kwa sasa na wanavyoichukulia awamu ya Tano.

Kishada.
ILISHAMEZWA ZAMANI SANA ,kifupi Zanzibar ni Koloni la Bara TANGANYIKA!
 
Zanzibar haitakuwa mkoa abadan ila itaendelea kutawaliwa na Tanganyika kwa mgongo wa Muungano mpka pale wazanzibar watakapokuwa wamoja. Hakuna chengine chochote kitakachoipa Zanzibar uhuru wake zaidi ya Umoja. Lakini kuna kazi kubwa sana ya kupatikana umoja wa Zanzibar maana Watanganyika wanatumia mbinu ya divide and rule. Wazanzibar wanagaiwa kwa siasa, ukabila na dini. Kwenye nyanja ya siasa CCM wa Zanzibar wanaaminishwa kuwa Zanzibar ni milki yao maana wao ndio waliopindua hivyo hakuna chama chengine chochote chenye hali yakushika dola, hata hivyo pamoja na kuaminishwa hivyo bado hali inakuwa ngumu sana siku za uchaguzi na wanashindwa kwa kura lakini Mtanganyika anatumia nguvu kukibakisha chama cha Mapinduzi (Rejea uchaguzi wa 2015). Pia Watanganyika wanatumia ukabila wa kuwagawa wazanzibar kwa kutumia upemba na Uunguja. Wanaleta propaganda ya kuwa wapemba ni hizbu na kukinasibishwa CUF ambayo sasa ni ACT wazalendo kuwa ni chama cha mahizbu hivyo hawana haki ya kutawala. Pia wanajaribu kujenga hoja ya kuwa CUF now ACT kuwa una wafuasi wake pemba tu ili waweze kuhalisha wizi wa kura katika majimbo ya Unguja kitu ambacho sikweli kwani 2015 CUF na CCM walipata majimbo sawa ya uchaguzi. Mwisho kabisa wanaendelea kuitawala Zanzibar kwa kigezo eti Zanzibar ikiwa huru inaweza kuwa kituo cha kigaidi kwa sababu tu 99% ya watu kule ni muslims fikra ambayo ni dhaifu sana. So siku wazanzibar wakiungana pamoja wanaweza kujikomboa katika dimbwi la ukoloni na kuwa huru.

Kwako VPosterior ni kweli kabisa kuwa wazanzibar tumegawiwa na siasa za ccm. devide and rule ndiyo inayoidhoofisha znz. kwa utaratibu huu kama mindset yetu haitabadilika abadan tutaendelea kuwa chni ya koloni la tanganyika. Mbya zaidi ni kuwa siasa za upinzani znz zimedhoofika na hasa baada ya msajili wa vyama vyama vya siasa kuiuaCUF asili ya maalim seif. lkn jengine ni kuwa wazanzibar wamevunjika moyo sana na hususan kila inapofika uchaguzi maalimn seif hujitokeza na kuwaambia vijana wasidai haki yao, amini; trust me kuwa kama si kauli za maalim seif basi kingekuwa kimeshaeleweka , kingenuka kitambo kwani wazanzibari tunajitambua na kuwa na political consciousness kubwa na hasa pale maslahi ya znz yanapofanyiwa dhihaka bila ya staha. wengine tunaamini kuwa maalim seif ni kibaraka wa CCM na ni yeye ndo anayesababisha CCM itawale maisha znz. Kama unafuatilia siasa za znz amini kuwa kama uchaguzi utakuwa huru na wa haki basi CCM haitashinda znz. Tumeichoka ccm kutokana na siasa zake za maji taka.
 
Zanzibar ikiwa huru , hakuwezi kuibuka Muslim extremists? Sasa hivi japo tupo kwenye muungano bado wanakamata watu wanakula mchana na kufunga biashara kibabe

Muungano ukifa nadhani watachoma makanisa na kufukuza watanganyika wote waliopo kule
Fear of the unknown ni maradhi kama kensa ya damu. religious extremism itoke wapi yakhe. Inaelekea umatawaliwa na siasa za udini na una chuki binafsi dhidi ya nchi yetu ya znz. umetahiriwa lkn?
 
Hii ni sahihi kwani ASP+TANU=CCM
lakini African Associatin(AA)+Shirazi Association (SA)=ASP
sasa hawa AA waliwazidi wenzao kete ,kwani wao asili yao ni Tanganyika na ni Wakristo kwa asili,na wengine walibadili majina na dini kimtindo ili kuwazuga wenzao.
Hatimae wakaichukua ASP wakaipeleka Tanganyika na kuwa CCM.
wale wote waliokuwa SA wamehamia upinzani na ndo maana hawapewi nchi.
Sasa Plan ni kuimaliza Zanzibar ili iwe Nchi moja tuu.
Pengine wamefanikiwa 80%,lakini bado pumzi ya upinzani bado ipo
View attachment 1249963
Mkuu upo deep, nimejifunza kitu kipya, nadhani JPM anaujasiri kumalizia kazi. Mkono wa heri watu wa mkakati wakaunga juhudi,kisha kura ya maoni tubaki nchi moja,ndugu wamoja.
 
Kitu muhimu kilichofanya Tanganyika na Zanzibar kuungana kilikuwa ni swala la usalama wa Zanzibar na Tanganyika baada ya Mapinduzi.
Ushahidi uko wazi kwa sababu hadi leo hakuna kelele zozote zinazohusu JWTZ.
Kelele zilizoko ni za tamaa ya madaraka ya Kisiasa ambazo hazizingatii manufaa mapana ya mwanainchi wa Kawaida.
Aliyekuwa Rais wa Afrika kusini , Mh. Botha aliwahi kusema " Mwafrika mweusi mwenye akili kuliko wote hawezi kufikiri zaidi ya mwaka moja"
Sisi Waafrika Weusi tunatakiwa kuthibitisha kuwa usemi huo ni wa uongo na kudhalilisha kwa kuungana na Kuifanya Afrika kuwa moja na Rais wake awe John Pombe Makufuli ili wazungu waisome namba.
Kufikiria kuwa Zanzibar itamezwa ni sawa na kuwa na akili ya kuwaza mlo wa siku moja.
Hatutaweza kuendelea kiuchumi na kiulinzi kwa kubaki Viinchi vidogo dogo.
Inchi ndogo, akili ndogo, uchumi mdogo,ulinzi mdogo, watu wadogo, elimu ndogo, maisha madogo etc.
 
Hawana hofu yoyote zaidi ya hofu ya kupungua ukubwa wa eneo la kuishi kutokana na maji kutaka kumeza hivyo visiwa acha uongo.
 
Kitu muhimu kilichofanya Tanganyika na Zanzibar kuungana kilikuwa ni swala la usalama wa Zanzibar na Tanganyika baada ya Mapinduzi.
Ushahidi uko wazi kwa sababu hadi leo hakuna kelele zozote zinazohusu JWTZ.
Kelele zilizoko ni za tamaa ya madaraka ya Kisiasa ambazo hazizingatii manufaa mapana ya mwanainchi wa Kawaida.
Aliyekuwa Rais wa Afrika kusini , Mh. Botha aliwahi kusema " Mwafrika mweusi mwenye akili kuliko wote hawezi kufikiri zaidi ya mwaka moja"
Sisi Waafrika Weusi tunatakiwa kuthibitisha kuwa usemi huo ni wa uongo na kudhalilisha kwa kuungana na Kuifanya Afrika kuwa moja na Rais wake awe John Pombe Makufuli ili wazungu waisome namba.
Kufikiria kuwa Zanzibar itamezwa ni sawa na kuwa na akili ya kuwaza mlo wa siku moja.
Hatutaweza kuendelea kiuchumi na kiulinzi kwa kubaki Viinchi vidogo dogo.
Inchi ndogo, akili ndogo, uchumi mdogo,ulinzi mdogo, watu wadogo, elimu ndogo, maisha madogo etc.
Si kweli mkuu kuna visiwa vidogo na vyenye watu kidogo zaidi ya Zanzibar na wameendelea mbali sana kama visiwa cha sheli sheli. Zanzibar ina watu takriban milioni mbili na ushei lakini umaskini wake ni mkubwa na ni kutokana na kuzibwa kwa mianya ya kiuchumi na Tanganyika kwa kutumia koti la Muungano. Leo Serikali ya Tanzania inashindwa kutia saini tu ili kuweza kujengwa bandari ya mpiga Zanzibar, yaani mkatabaa upo na wahisani wapo watie saini tu hawataki eti umeandikwa kwa kiarabu. Ukatafsiriwa kwa English lakini pia wakagoma hadi leo hii. Muungano gani huu unaonyonya na kuimeza nchi moja wakati nyengine inanufaika.
 
Zanzibar ikiwa huru , hakuwezi kuibuka Muslim extremists? Sasa hivi japo tupo kwenye muungano bado wanakamata watu wanakula mchana na kufunga biashara kibabe

Muungano ukifa nadhani watachoma makanisa na kufukuza watanganyika wote waliopo kule
Kwani unalijuwa Kanisa la kwanza hapa Tanzania ni lipi, lipo wapi na nililijengwa kipindi gani? Hii nimeilezea ni katika hizo hoja dhaifu zinazotumiwa kuhalalisha huu ukoloni. Zanzibar is tourist place tena internationally inatambulika, people from all walks of life tena wadini zote na makabila yote walikuwa wanakuja kabla ya uhuru na baada ya uhuru na hadi hiki kipindi chengine cha ukoloni bado wanakuja na wala hawabughudhiwi as long as wanafuata sheria, mila na desturi za kizanzibar.
 
Back
Top Bottom