Tathmini hotuba ya Rais Samia miaka 60 ya Jeshi la Polisi: Uzuri, ubaya, utata na mapendekezo mahsusi

Tathmini hotuba ya Rais Samia miaka 60 ya Jeshi la Polisi: Uzuri, ubaya, utata na mapendekezo mahsusi

Doctor Mama Amon

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2018
Posts
2,089
Reaction score
2,725

1. Utangulizi

Akiwa katika Chuo cha Polisi Tanzania kilichooko mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro, mnamo tarehe 17 Septemba 2024, Samia Suluhu Hassan, alivaa kofia zake zote kama Rais, Amiri Jeshi Mkuu, na Mkuu wa Nchi katika Jamhuri ya Muungano wa Kidemokrasia ya Tanzania.

Akiwa amevaa kofia hizo alitoa hotuba ya dakika 57 kwa ajili ya kufunga Mkutano Mkuu wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi kwa mwaka 2024 uliofanyika sambamba na Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Polisi Tanzania.

Katika andiko hili nafanya tathmini ya uzuri, ubaya, na utata kabla ya kujadili hotuba hiyo, kuhitimisha na kutaja mapendekezo mahsusi.


Moshi-02.PNG


2. Matamko mazuri yenye sura ya kujenga

  • Jeshi letu la polisi linapaswa Kwenda na wakati.
  • Jeshi la polisi lilete bajeti kwa ajili ya kujiimarisha tekinolojia ya kufanya “saveilansi” kwa kutumia mbinu za kisasa na nitatekeleza mahitaji yao mara moja.
  • Jeshi la polisi liboreshe mbinu zake za kuzuia vifo vinavyotokana na ajali za barabarani zinazoweza kuzuilika.
  • Kwa mujibu wa majukumu yake ya kisheria Jeshi la polisi halipaswi kuwafumbia macho wale wote wenye nia ovu ya kuleta vurugu na uvunjifu wa amani.
  • Jeshi la polisi lijitazame na kujisahihisha ili kurudisha Imani yake mbele ya jamii ili kuzuia aibu iliyotokea kule Mwanza jana ambapo ni wazi kuwa umma hauna imani tena na jeshi hili.
  • Bado nina nia ya kuendeleza utekelezaji wa falsafa ya 4R, yaani, “Reforms, Resilience, Reconciliation, and Rebuilding.”
  • Damu ya kila mtanzania ituume tusiwe tunamwaga damu bila sababu maana uhai wa kila binadamu hauna bei.
  • Hatutaruhusu kamwe mataifa ya nje kuingilia uhuru wetu wa kujiamulia mambo yetu ya ndani.
  • Kwa kuwa uchaguzi ujao utapita lakini Tanzania itabaki, nalitaka jeshi la polisi linakuwa macho kabla, wakati na baada ya uchaguzi dhidi ya mtu yeyote mwenye nia ya kuhatarisha amani kwa kisingizio cha uchaguzi.
  • Sikubaliani na matukio ya mauaji yanayohusisha wazazi, viongozi wa dini, wapenzi na waganga wa jadi.
  • Jeshi la polisi liandae mpango kazi wenye kuonyesha vigezo vya kupima ufanisi ili tuweze kupima kasi ya utendaji wa kazi zenu.
  • Maisha ya mwanadamu yeyote yule yana thamani isiyomithilika. Huwezi kutia thamani maisha ya mwanadamu. Huwezi. Huwezi kufananisha uhai wa mwanadamu kwa ubora wa hadhi ya mtu, kabila la mtu, asili na jinsia, umri au majukumu yake, yuko kwenye kundi gani, ni mwanachama wa wapi, anashiriki wapi. Hakuna thamani hiyo kwenye maisha ya mtu. Katika hali yoyote ile uhai wa mwanadamu ni jambo adhimu sana.
  • Na ndio maana uhai wa Mtanzania unalindwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ilivyoelezwa katika ibara ya 14 ambayo inasema, 'Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata kutoka kwa jamiihifadhi ya maisha yake, kwa mujibu wa sheria.'
  • Sasa, kwa wote tunaotumikia wananchi katika nyadhifa mbalimbali serikalini huwa tunapitishana kwenye kiapo cha kulinda Katiba ya nchi katika kutimiza majukumu yetu. Sasa nimtake kila mmoja wetu tuwajibike kwa viapo tunavyoapa.
Moshi-03.PNG


3. Matamko mabaya yenye sura ta vitisho
  • Tarehe 11 Septemba 2024 Chadema walifanya mkutano huko Arusha, ambapo ajenda kuu ilikuwa ni jinsi ya kutumia maandamano kama mbinu ya kuvuruga amani na utulivu nchini.
  • Wanataka kumwondoa Rais madarakani kwa njia ya maandamano lakini Rais hawezi kuondolewa kwa njia hiyo.
  • Wamesahau misukosuko waliyopita hapo nyuma mpaka wakakimbia nchi nami kuwarejesha kwa kutumia falsafa ya 4R zangu wanayoikejeli
  • Kama Wapinzani wameota Mikia Sheria zile zile (alizokuwa anazitumia hayati Magufuli kuwakandamiza) bado zipo
Moshi-01.PNG

4. Matamko tata yenye sura ya vijembe na mkanganyiko
  • Ukimya wangu sio ujinga maana unanipa fursa ya kutafakari.
  • Kauli za wakosoaji wangu wengi ni uropokaji bila werevu maana wao ni kama debe shinda lisiloacha kuvuma.
  • Sio sawa kwa kifo kimoja tu cha Ally Mohamed Kibao wa Chadema kusababisha mtikisiko wa mwili na akili kiasi cha kuibua mihemuko ya kuhatarisha amani na utulivu wakati ni kifo kama vifo vya watu wengine waliouwawa siku za nyuma na wanaoendelea kuuawa kila siku kwa sababu mbalimbali, na katika matukio haya mengine hakukuwepo na mihemuko ya aina hiyo.
  • Balozi za kigeni zilizokemea na kutaka uchunguzi wa kifo cha Mohamed KIbao ufanyike zilifanya hivyo bila baraka za Marais wa nchi wanazoziwakilisha na kinyume cha mwongozo wa kidiplomasia wa Viena.
Moshi-04.PNG


5. Mjadala wa kutathmini kauli za Rais Samia

Baada ya uchambuzi hapo juu, kuna mambo kadhaa yanayojitokeza na ambayo napenda kuyajadili kwa kifupi. Haya ni:
  • Mkanganyiko wa kimantiki na kiitikadi (logical and ideological incoherence),
  • Mkanganyiko wa kisemantiki (semantic incoherence),
  • Mkanganyiko wa kimaadili (moral incoherence), na
  • Mkanganyiko kuhusu ukuu wa nafsi ya kiutu katika ngazi ya dola (personal state sovereignty).
Mkanganyiko wa kimantiki na kiitikadi ni kuhusu kauli za Rais Samia zinazogongana. Falsafa ya "4R" anayoinadi kama turufu yake ya kisiasa inahusisha "Resilience," "rebuilding," "reconciliation" na "reforms," yaani "mastahamala," "maboresho," "mapatano," na "mageuzi."

Tatizo liko hivi: Rais ananadi ajenda ya "mageuzi" na Wakati huo huo hataki kufanya "mageuzi" ya sheria mbaya zilizopo na zilizokuwa zinatumiwa na watangulizi wake dhidi ya vyama vya upinzani. Misimamo hii miwili haisikilizani maana ni kama maji na mafuta.

Kwa hiyo, tunaweza kusema kwa usahihi kwamba, katika suala hili, maneno ya Rais yalokosa masikilizano ya kimantiki, yaani yanao mkanganyiko wa kimantiki (incoherence). Anayo hiari ya kuchagua moja kati ya mawil, lakini yote mawili hayawezi kwenda pamoja.

Mkanganyiko wa kisemantiki ni kuhusu kauli ya Rais Samia kwamba maneno ya Chadema, "Smia must go" yanamaanisha kwamba Chadema wanataka kumwondoa Ikulu kinyume cha matakwa ya kikatiba.

Ninayo mawazo tofauti. Kauli ya Chadema kwamba "Samia must go," bila kuongezewa neno la ziada sio kauli ya kihaini.

Kwa nini? Ni hivi: Kuna njia kadhaa za kutafsiri maneno "Samia Must Go". Yaani, kauli hiyo inaweza kusomeka hivi:
  • "Samia must go peacefully by resigning after self-appraisal following peaceful demonstrations"; au
  • "Samia must go peacefully through a democratic ballot box in CCM 2025 primaries"; au
  • "Samia must go peacefully through a democratic ballot box in 2025 general elections"; au
  • "Samia must go forcibly through extra-legal public violence"; au
  • "Samia must go forcibly through extra-legal execution"; au
  • "Samia must go forcibly through parliamentary impeachment".
Mpaka hapo sioni namna ya kuthibitisha uhaini katika tamko hilo la Chadema.

Mkanganyiko wa kimaadili ni kuhusu kauli ya Rais Samia kwamba "kifo ni kifo tu" pasipokujali aliyekufa nani, kimetoa vipi, kimetoa lini, kimetoa wapi, kimesababishwa na nini, kimesababishwa na nani, mwuaji alikuwa na lengo gani, na masuala mengine ya kimazingira.

Rais alieleza mshangao wake kwa kutamka kuwa: "Mtu mmoja tu Ally Kibao kafa, halafu kelele nchi nzima"

Kwa maneno haya alimaanisha kuwa uhai wa binadamu unapimika katika mizania fulani, dhana ambayo alipinga katika sehemu nyingine ya hoja yake. Ni mkanganyiko.

Hivyo, tathmini yangu itajikita katika swali hili: Je, Rais Samia anajua na kuelewa tofauti kati ya uhalifu na uadilifu au hapana? Swali hili kuu linazaa maswali madogo yafuatayo:
  • Rais Samia anajua tofauti kati ya kifo kinachosababishwa kwa makusudi na kifo kinachotokea kwa bahati mbaya, yaani murder versus manslaughter?
  • Rais Samia anajua tofauti kati ya uovu wa kimaadili na uovu wa kifizikia, yaani moral evil versus physical evil?
  • Rais Samia anajua tofauti kati ya tendo la jinai lenye kiima cha dhamira na kiarifa cha utekelezaji, yaani guilty mind versus guilty act?
  • Rais Samia anajua kuwa sayansi inayochunguza anatomia ya matendo ya kihalifu (criminal praxiology) inasema kuwa kila kitendo kinachofanyika kwa makusudi ni kama mnyororo wenye sehemu tatu, yaani LENGO, MBINU NA MAZINGIRA, na kwamba uadilifu au uhalifu wa kitendo hicho unapimwa kwa kuangalia pingili zote tatu kwa mpigo ili kujiridhisha kuwa hakuna pingili yoyote yenye doa la uovu au kinyume chake?
  • Mwaka 2021, siku Rais Samia alipokula kiapo cha Urais kwa mara ya kwanza pale Dodoma alituomba tumwamini kama Rais makini kwa kuwa yeye amelelewa katika familia yenye maadili mema yanayomwezesha kuwa mkuu wa nchi thabiti bila kujali jinsia, dini wala historia yake. Je, katika mazingira ya hotuba ya sasa bado anataka tuamini maneno yake yale?
  • Na swali kubwa zIdi: wasaidizi wa Rais waliosaidia kuandaa na kuandika hotuba ya Rais ya leo wanao weledi kiasi gani hadi wampotoshe Rais kwa kiwango hiki?
  • Lakini pia, kama yeye Rais amepotoshwa, kwa nini amekubali kulishwa matango pori bila kuyachukua kabisa?
  • Kama hakulishwa matango pori, na badala yake yeye ndio kachepuka na kuondoka kwenye "script" aliyoandaliwa na wasaidizi, kwa nini ameamua kuchepuka katika namna ambayo inapasua badala ya kuunganisha Taifa?
  • Kwa nini ameamua kutembea kwenye nyayo za kina Musiba na Shekhe Mwaipopo?
Kwa ujumla vifo vya watu vinagawanyika katika makundi makuu manne:

  • Natural death (aging, diseases, disasters)
  • Accidents triggered by humans
  • Suicide
  • Homicide (ritual killings, murder, Manslaughter, assassination, euthanasia, genocide, etc)

Katika muktadha huu ukweli kwamba duniani kote kuna matendo ya mtu mmoja au kundi moja la watu kutoa uhai wa binadamu mwingine kwa makusudi (homicide), bila kujali kama ni tabia ya serikali au tabia ya watu binafsi haukanushiki.

Lakini hii sio leseni inayohalalisha matukio hayo yatokee Tanzania, maana uhalifu mara mbili hauzalishi uhalali (two wrongs don't make a right).

Hivyo, sio sawa kukubaliana na makosa yanayofanyika kwetu kwa sababu tu yanafanyika huko kwa majirani zetu.

Lakini, kuna aina kuu mbili za mauaji. Kuna mauaji yanayotekelezwa na watu binafsi na yanayotekelewa na vyombo vya serikali.

Mfano wa mauaji yanayotekelezwa na watu binafsi ni mauaji ya albino, mauaji ya Watoto na mauaji ya vikongwe. Katika mauaji haya watu binafsi hushitakiwa na Jamhuri chini ya sheria ya makosa ya jinai kwa kosa la mauaji ya kukusudia (murder) au kosa la mauaji ya kutokusudia (manslaughter).

Mfano wa mauaji yanayotekelezwa na serikali (state sponsored killings), ni mauaji yale yale yaliyotajwa hapo juu, lakini ambayo sasa yanapata majina mapya.

“Murder” hugeuka na kuitwa ama “Crimes Against Humanity,” au “Gross Violation of Human Rights,” au “Genocide.” “Kidnappings” hugeuka na kuwa “Enforced Disappearance.” Na “Rape” na “Defilement” yanageuka na kuwa “Torture,” “Genocide,” “Crimes Against Humanity,” au “War Crime.”

Makosa haya yanayofanywa na serikali yanakatazwa kwenye mikataba yote ya kimataifa ya haki za binadamu. NI Pamoja na MKataba wa Afrika Mashariki, Mkataba wa Umoja wa Afrika, na Mkataba wa Umoja wa Mataifa. Kwa kuwa serikali haziwezi kujishitaki, katika makosa haya, raia huzishitaki serikali zao katika ngazi za mahakama za kimataifa.

Katika makosa haya, serikali inashitakiwa kwa sababu ndiyo yenye dhamana ya kulinda raia wake pamoja na mali zao, kama jukumu la kwanza.

Hivyo, tunapozungumzia mauaji kama vile “albinocide,” “Gun Violence,” “kidnapping,” na “murder,” katika nchi mbalimbali lazima tujibu swali moja muhimu kabla ya kuyjadili: Je, yanaratibiwi na serikali au na watu binafsi?

Kama makosa haya yanaratibiwa na serikali, basi, haki ya nchi husika ya kutoingiliwa na mataifa mengine, kama unavyotaka mkataba wa Viena(1961), inayeyuka.

Ni kweli kuwa, wenye makosa ya kawaida ambayo wananchi huwafanyia wananchi wenzao kila Taifa linayo kinga ya kutoingiliwa, maana serikali ina haki na uwezo wa kushughulikia wahalifu kwa kuwapandisha kizimbani.

Lakini, kwenye mauaji ya mtu yanayoonekana kufanywa chini ya uratibu wa serikali, kama inavyoonekana kwa marehemu Mzee Mzee Kibao, kwa maana ya uhalifu wa dola dhidi ya mwananchi wake, haki ya kutoingiliwa inayeyuka.

Na kuhusu mkanganyiko kuhusu ukuu wa nafsi ya kiutu katika ngazi ya dola, yaani “personal State Sovereignty”, ukweli uko hivi:

Kwenye jinai inayofanywa na dola, yaani State Sponsored Killings, State Sponsored Violence, Genocide, Crimes Against Humanity, na Gross Violations of Human Rights, hoja ya “personal State Sovereignty” inabatilika.

Ni hapa ambapo, sheria za kimataifa zinaruhusu mataifa mengine kuzikemea, kuzikosoa na hata kuziwajibisha serikali za nchi nyingine zinazofanya makosa haya.

Kwa ufupi, basi, hii wakati hotuba ya Dkt. Nchimbi juzi iliunganisha Taifa dhidi ya genge la wahalifu dhidi ya uhai, hotuba ya Rais Samia imeiweka serikali kundi moja na watuhumiwa wa uhalifu huo, kiasi kwamba ni sahihi kusema kuwa Mwenyekiti wa CCM na Katibu wake sasa ni maji na mafuta.

1726663499658.png


6. Hitimisho kuhusu aliyoyasema na aliyoyasahau
  • Rais Samia ameinadi falsafa yake ya "4R" na wakati huio huo kuikana kutokana na uamuzi wake wa kuzikumbatia sheria kandamizi kwa ajili ya kuzitumia kwa ajili ya vyama vya upinzani.
  • Pamoja na kulalamika, kusikitika, kuhuzunika na kukereka, Rais hajasema jambo lolote la kivitendo lenye kueleza ni kwa vipi anapanga kutumia falsafa yake ya "4Rs" kuleta mageuzi ya kimfumo yatakayolisaidia Taifa kukabiliana na janga la uhalifu dhidi ya uhai wa binadamu wasio na hatia.
  • Rais hajakemea kabisa uhalifu unaoonekana kufanywa na baadhi ya watu katika vyombo vya dola, kama tukitembea katika misingi ya ushahidi wa kimazingira ambao mpaka sasa haujakanushika, jambo ambalo linaashiria kuwa huenda anakubaliana na utovu wa nidhamu unaofanywa na baadhi ya watu katika vyombo vya dola.
  • Rais hajasema lolote kuhusu hadidu za rejea za Kamati ya Waziri Mkuu aliyosema ameiunda kwa ajili ya kuchungiza mauaji holela, na hivyo kuleta shaka katika uhalisia wa kazi ya kamati hiyo.
  • Rais anasema kuwa kuna watu walifanya kikao kilichopanga kufanya uhalifu lakini hajaelekeza vyombo vya dola kuchukua hatua zozote dhidi yao, jambo linaloleta mashaka katika kile anachokisema.
  • Rais ametoa kauli zenye kubatilishana katika suala la kukuza na kuhami uhai wa raia wasio na hatia, maana hakutofautisha vifo kwa kuzingatia sababu zake.
  • Rais hakusema lolote kuhusu marekebisho ya sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa yam waka 2023 inayoweza kuchochea machafuko nchini.
  • Rais Samia ametoa baadhi ya kauli zinazoweza kumfungamanisha na uovu unaoendelea nchini. Kwa mfano, kauli ya Rais dhidi ya wakosoaji aliowaita “waropokaji” inaweza kutumika kama ushahidi kwamba yeye ndiye ameagiza kinaDeusdedith Soka wakamatwe na kuwekwa kizuizini. Pia inaweza kuchochea ukamataji holela kama ule uliofanyika dhidi ya Soka kwa sababu tu ya kauli zake za kuvikosoa vyombo vya dola. Video ya Soka hapa chini ni ushahidi mzito wenye kueleza kwa nini nahitimisha hivyo.

Hoja ya Deusdedit Soka kuhusu uhaba wa intelijensia katika Jeshi la Polisi
7. Mapendekezo mahsusi
  • Awali ya yote, hotuba ya leo inayo makosa madogo na makubwa kiasi kwamba weledi wa "political analysts" walioko Ikulu umepata dosari. Hivyo, Rais afanye hima kurekebisha na kuimarisha timu yake inayomsaidia kwenye "political intelligence analysis and evaluation."
  • Kwa ajili kuhakikisha maneno yake yanaaminika, Rais anapaswa kuweka bayana hadidu za rejea kwa ajili ya Tume ya Waziri Mkuu. Maneno yake kwamba "uchunguzi unakwenda vizuri" hayawezi kuaminika bila hadidu za rejea kuonekana.
  • Rais atoe tamko la kuvitaka vyombo vya dola kuacha kuwakamata watu wote wanaoikosoa serikali kwa njia ya hoja nyoofu. Kazi mojawapo ya rais ni kulinda uhuru wa raia katika suala la kufikiri na kueleza fikra zao bila hofu ya kutekwa, kuteswa, kuteketezwa au kuwekwa kuzuizini.
  • Chini ya falsafa yake ya "4Rs" sasa Rais atoe agizo la kuachiwa huru kina Soka kwa sababu kosa lao ni kuikosoa serikali kwa njia ya hoja, na jambo hili sio kosa la jinai, sio uhaini na sio ugaidi.
  • Rais aagize watu wote anaosema waliokaa kikao cha kuandaa vurugu wanafikishwa mbele ya sheria badala ya kuwa mlalamikaji na afisa propaganda. Kanuni ya kutofautisha kati ya taasisi na magenge ya wahuni ndani ya taasisi itumike hapa pia kama ilivyotumiwa na Dkt. Nchimbi kwa upande wa CCM na serikali yake juzi kupitia hotuba yake makini.
  • Chini ya falsafa yake ya "4Rs" sasa Rais amwagize mwanasheria mkuu wa serikali kusababisha marekebisho ya sheria mbaya 40 zilizobainishwa katika Ripoti ya Tume ya Jaji Nyalali mwaka 1992.
  • Chini ya falsafa yake ya "4Rs" sasa Rais amwagize mwanasheria mkuu wa serikali kusababisha marekebisho ya sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa ya mwaka 2023 kwa kuondoa dosari zilizo katika vifungu vya 3, 5(2) na 19(1). Vifungu hivi vinaweza kusababisha machafuko nchini kupitia mikono ya maafisa usalama watakaoamua kuvitumia kufanya kazi za kipolisi.
  • Chini ya falsafa yake ya "4Rs" sasa Rais aagize kutungwa kwa Sheria ya Kukuza na Kuhami Uhai (Defense of Life Act--DOLA)
  • Rais ahakikishe kuwa Sheria ya Kukuza na Kuhami Uhai inatumika:
    • Kuanzisha Mahakama ya Kushughulikia Kesi za Mauaji (Homicide Court) kama tulivyoanzisha mahakama ya kazi, mahakama ya biashara na mahakama ya ardhi.
    • Kuanzisha Tasisi ya Kupambana na Kuzuia Utamaduni wa Kifo (Mitigation and Prevention of Homicide Authority--MAPHA) nchini Tanzania kama tulivyoanzisha TAKUKURU.
    • Kukusanya taarifa za watuhumiwa wa utekaji na mauaji, kuzichambu, kuwamata na kuwashitaki katika mahakama ya mauaji.
    • Kuwapunguzia polisi majukumu ya kupambana na Kuzuia Utamaduni wa Kifo.
  • Rais ahakikishe kuwa wigo wa Sheria ya Kukuza na Kuhami Uhai unagusa maeneo yafuatayo:
    • Mauaji ya wanasiasa (politicide)
    • Mauaji yanayofanyika nje ya mfumo wa kisheria (extra-judicial political killings);
    • Mauaji ya watu wenye uzeruzeru (albinocide);
    • Mauaji ya watoto wachanga (infant killings)
    • Mauaji ya kafara (ritual killings)
    • Mauaji ya vikongwe (senicide/gerontocide)
    • Mauji ya kulipiza kisasi (retaliatory killings)
    • Mauaji ya ukoo au kabila zima (genocide)
    • Mauaji ya watu wengi kwa mpigo (democide)
    • Mauaji ya familia nzima (familicide)
    • Mauaji ya wanawake (femicide)
    • Mauaji ya mama mzazi (matricide)
    • Mauaji ya baba mzazi (patricide)
    • Mauaji ya ndugu wa damu (siblicide)
    • Mauaji ya mtoto yanayofanywa na mzazi (filicide)
    • Mauaji ya mke yanayofanywa na mume (uxoricide)
    • Mauaji ya wazazi yanayofanywa na watoto (parricide)
    • Mauaji yanayotokana na wivu wa kimapenzi (intimate partner homicide)
    • Mauaji yaliyosababishwa na polisi
    • Mauaji yaliyosababishwa na maafisa wa Idara ya Usalama wa Taifa
    • Mauji yaliyosababishwa na JWTZ wakati hakuna operesheni rasmi za kijeshi zilizoidhinishwa rasmi.
    • Na mauaji mengine kama haya.
1726736237529.png


Nawasilisha.

Raia Mwema.

View attachment 3099134
 

Attachments

  • VID-20240916-WA0031.mp4
    9.1 MB
Watakamatwaje watu aliowaagiza?
Mmh! Muwe mnafikiria kabla ya kuropoka jamani! Maneno hayo Matatu yanaweza kukuletea mzigo wa kilo elfu tatu kichwani mwako.Usipende kuhemkwa na maneno ya vijiwe vya kahawa.Mwenye masikio na asikie.Una ushahidi? Mimi nimekushauri tu sio kwa ushabiki wala mahaba.
 
View attachment 3099128
1. Utangulizi

Akiwa katika Shule ya Polisi Tanzania iliyoko Moshi, Mkoani Kilimanjaro, mnamo tarehe 17 Septemba 2024, Samia Suluhu Hassan, ambaye ni Rais, Amiri Jeshi Mkuu, na Mkuu wa Nchi katika Jamhuri ya Muungano wa Kidemokrasia ya Tanzania, ametoa hotuba ya dakika 57 ya kufunga Mkutano Mkuu wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi kwa mwaka 2024 uliofanyika sambamba na Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Polisi Tanzania.

Katika andiko hili nafanya tathmini ya uzuri, ubaya na utata wa hotuba hiyo kabla ya kuhitimisha na kutaja mapendekezo mahsusi.

2. Matamko mazuri yenye sura ya kujenga

  • Jeshi letu la polisi linapaswa Kwenda na wakati.
  • Jeshi la polisi lilete bajeti kwa ajili ya kujiimarisha tekinolojia ya kufanya “saveilansi” kwa kutumia mbinu za kisasa na nitatekeleza mahitaji yao mara moja.
  • Jeshi la polisi liboreshe mbinu zake za kuzuia vifo vinavyotokana na ajali za barabarani zinazoweza kuzuilika.
  • Kwa mujibu wa majukumu yake ya kisheria Jeshi la polisi halipaswi kuwafumbia macho wale wote wenye nia ovu ya kuleta vurugu na uvunjifu wa amani.
  • Jeshi la polisi lijitazame na kujisahihisha ili kurudisha Imani yake mbele ya jamii ili kuzuia aibu iliyotokea kule Mwanza jana ambapo ni wazi kuwa umma hauna imani tena na jeshi hili.
  • Bado nina nia ya kuendeleza utekelezaji wa falsafa ya 4R, yaani, “Reforms, Resilience, Reconciliation, and Rebuilding.”
  • Damu ya kila mtanzania ituume tusiwe tunamwaga damu bila sababu maana uhai wa kila binadamu hauna bei.
  • Hatutaruhusu kamwe mataifa ya nje kuingilia uhuru wetu wa kujiamulia mambo yetu ya ndani.
  • Kwa kuwa uchaguzi ujao utapita lakini Tanzania itabaki, nalitaka jeshi la polisi linakuwa macho kabla, wakati na baada ya uchaguzi dhidi ya mtu yeyote mwenye nia ya kuhatarisha amani kwa kisingizio cha uchaguzi.
  • Sikubaliani na matukio ya mauaji yanayohusisha wazazi, viongozi wa dini, wapenzi na waganga wa jadi.
  • Jeshi la polisi liandae mpango kazi wenye kuonyesha vigezo vya kupima ufanisi ili tuweze kupima kasi ya utendaji wa kazi zenu.
View attachment 3099127

3. Matamko mabaya yenye sura ta vitisho
  • Tarehe 11 Septemba 2024 Chadema walifanya mkutano huko Arusha, ambapo ajenda kuu ilikuwa ni jinsi ya kutumia maandamano kama mbinu ya kuvuruga amani na kuipindua serikali.
  • Wamesahau misukosuko waliyopita hapo nyuma mpaka wakakimbia nchi nami kuwarejesha kwa kutumia falsafa ya 4R zangu wanayoikejeli
View attachment 3099129
4. Matamko tata yenye sura ya vijembe na mkanganyiko
  • Ukimya wangu sio ujinga maana ni fursa ya kutafakari.
  • Kuzungumza kwa wakosoaji wangu wengi ni kuropoka bila werevu maana wao ni kama debe shinda lisiloacha kuvuma.
  • Sio sawa kwa kifo kimoja tu cha Ally Mohamed Kibao wa Chadema kuibua wito wa “Samia Must Go” wakati ni kifo sawa na vifo vya watu wengine waliouwawa siku za nyuma na wanaoendelea kuuawa kila siku kwa sababu mbalimbali, na katika matukio haya mengine hakukuwepo na wito wa aina hiyo.
  • Balozi za kigeni zilizokemea na kutaka uchunguzi wa kifo cha Mohamed KIbao ufanyike zilifanya hivyo bila baraka za Marais wa nchi wanazoziwakilisha na kinyume cha mwongozo wa kidiplomasia wa Viena.
View attachment 3099132
5. Hitimisho kuhusu aliyoyasema na aliyoyasahau
  • Kauli ya Rais kuhusu “waropokaji” inaweza kuchochea ukamataji holela kama ule uliofanyika dhidi ya Deusdedith Soka kwa sababu tu ya kauli zake za kuvikosoa vyombo vya dola (tazama video hapo juu).
  • Rais hajasema lolote kuhusu hadidu za rejea za Kamati ya Waziri Mkuu aliyosema ameiunda kwa ajili ya kuchungiza mauaji holela, na hivyo kuleta shaka katika uhalisia wa kazi ya kamati hiyo.
  • Rais anasema kuwa kuna watu walifanya kikao kilichopanga kufanya uhalifu lakini hajaelekeza vyombo vya dola kuchukua hatua zozote dhidi yao, jambo linaloleta mashaka katika kile anachokisema.
  • Rais ametoa kauli zenye kubatilishana katika suala la kukuza na kuhami uhai wa raia wasio na hatia, maana hakutofautisha vifo kwa kuzingatia sababu zake.
  • Rais hakusema lolote kuhusu marekebisho ya sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa yam waka 2023 inayochochea machafuko nchini.
View attachment 3099134

6. Mapendekezo
  • Rais aweke bayana hadidu za rejea kwa ajili ya Tume ya Waziri Mkuu.
  • Rais atoe tamko la kuvitaka vyombo vya dola kuacha kuwakamata wakosoaji wa serikali kwa njia ya hoja.
  • Rais atoe agizo la kuachiwa kina Soka kwa sababu kosa lao ni kuikosoa serikali kwa njia ya hoja, na jambo hili sio kosa la jinai, sio uhaini wala ugaidi.
  • Rais aagize watu wote waliokaa kikao cha kuandaa vurugu wanafikishwa mbele ya sheria badala ya kuwa mlalamikaji na afisa propaganda.
  • Rais amwagize mwanasheria mkuu wa serikali kusababisha marekebisho ya sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa ya mwaka 2023 inayochochea machafuko nchini, kwa kuondoa dosari zilizo katika vifungu vya 3, 5(2) na 19(1).

Raia Mwema.
Hatuna rais sahihi
 
Amejitutumua kweli kuhutubia

Lakini pamoja na kujitutumua, kwa kumtazama kupitia body language yake anaonesha wazi kuwa ametikiswa, nafsi yake ina hofu kubwa na kujiamini kwake kumeshuka hadi chini ya kiwango

Na wabaya wake ndani ya serikali yake, wakamwandalia moja ya hotuba mbaya, ya hovyo na wakati huohuo inayoweza kuyafanya mambo kuwa mabaya zaidi kwake kwa sababu hajagusa kabisa kiini cha tatizo badala yake amewatia moyo wahalifu waendelee na uhalifu wao!!

Kwa kifupi, Rais Samia Suluhu Hassan ameshindwa kutumia fursa hii muhimu kuliweka sawa taifa na nchi, badala yake ameitumia fursa hii muhimu kupiga propaganda za siasa hatarishi

Huyu mama amewasha moto badala ya kuuzima. Hakuna shaka kuwa, ametangaza rasmi sasa kuwa atatumia njia na mikakati ya mtangulizi wake Hayati John Pombe Magufuli kuitawala nchi hii

Kama ni hivi, na yeye ajiandae kuanguka na kuvunjika kama mwenzake alivyoanguka na kupotea kabisa ktk uso wa dunia!
 
Mmh! Muwe mnafikiria kabla ya kuropoka jamani! Maneno hayo Matatu yanaweza kukuletea mzigo wa kilo elfu tatu kichwani mwako.Usipende kuhemkwa na maneno ya vijiwe vya kahawa.Mwenye masikio na asikie.Una ushahidi? Mimi nimekushauri tu sio kwa ushabiki wala mahaba.
Huo ndio ukweli, kinachoweza kufanyika ni kuniumiza lakini haiondoi ukweli hayo ni maagizo yake ili kulinda madaraka.
 
Tanzania inakoelekea itakuwa kama au zaidi ya Rwanda.

Kauli alizotoa SSH hazikubaliki uraiani. Na kuzitoa jeshini ni kuhalalisha uovu dhidi ya wakosoaji wake!

Kifupi wasiojulikana, watekaji, watesaji na wauaji wamehalalishwa!
 
CHADEMA NI WAPUUZI SANA TENA WASIO NA AKILI KABISA, "" HIVI NCHI HII ITAKAPOVURUGIKA HUO UPINZANI WAO WATAUFANYIA KATIKA NCHI GANI"""
N. B, Tunao maadui wengi sana wanaosubiria kwa kiu kubwa sana sisi wenyewe tuivuruge nchi waanze kumwaga fedha kwa watu na vikundi mbalimbali alimradi nchi ikibidi isiikalike kabisa

>TUWE MAKINI SANA! TUSICHEKE NA KIMA!,
 
Mmh! Muwe mnafikiria kabla ya kuropoka jamani! Maneno hayo Matatu yanaweza kukuletea mzigo wa kilo elfu tatu kichwani mwako.Usipende kuhemkwa na maneno ya vijiwe vya kahawa.Mwenye masikio na asikie.Una ushahidi? Mimi nimekushauri tu sio kwa ushabiki wala mahaba.

Punguza uoga mtu mzima. Kama JF tu wewe ni muoga kiasi hicho, je kwenye mambo mengine utakuwaje?
 
CHADEMA NI WAPUUZI SANA TENA WASIO NA AKILI KABISA, "" HIVI NCHI HII ITAKAPOVURUGIKA HUO UPINZANI WAO WATAUFANYIA KATIKA NCHI GANI"""
N. B, Tunao maadui wengi sana wanaosubiria kwa kiu kubwa sana sisi wenyewe tuivuruge nchi waanze kumwaga fedha kwa watu na vikundi mbalimbali alimradi nchi ikibidi isiikalike kabisa

Mbona CHADEMA wanafanyaga maandamano Tena Hadi mkuu wa Mkoa anahudhuria. Inakuaje Leo wametangaza maandamano mmeanza kuleta visingizio vya kuleta vurugu.
 
Kwa mtazamo wangu Rais ameonyesha hofu,kutokujiamini,kukaririshwa uongo dhahiri na mbaya zaidi kuwa easily manipulated .
Inatia hofu huenda kuna genge linalomuendesha kutikisika na kuhofia kivuli chake.
Kwa mipasho Ile walio na sikio lake wamnong' oneze sio lazima kuwa Rais na maisha ya mstaafu ni bora na stress free.
 
Back
Top Bottom