Tathmini ya kisayansi juu ya matokeo ya uchaguzi mkuu Novemba 2020

Mtoa post point hii utakuwa uliifikia ukiwa mahututi kimawazo ,edit aisee
👇
Tangia siku ya kwanza ya Raisi Magufuli kuingia madarakani, makundi tofauti ya wanachi kuanzia wachuuzi, wafanyakazi, wakulima, vijana na kina mama wamepewa fursa na uhuru mkubwa wa kufanya kazi halali zinazowaingizia kipato.

NAKUKUMBUSHA wafanyakazi wapo hoi hawana amani na utawala huu kama huamini tazama zoezi la uandikishaji walivyolisusa.
 
Sayansi na Teknolojia vikitumika vizuri vina uwezo wa kutoa majibu ya wakati ujao,uliopo na uliopita kwa uhakika wa asilimia 99.9%.

Katika andiko langu hili nitatumia taarifa za kisayansi zilizopo kuweza kutoa matokeo ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Novemba 2020.

Tathmini hii isitumike kuwabwetesha wale ambao tathmini itawaonesha wanaweza kushinda ila iwe chachu ya kuwafanya wafanye vizuri zaidi.

Pia kwa wale ambao itaonesha watashindwa nao iwe chachu kwao kujiandaa na kujitahidi kushinda katika maeneo ambayo wananguvu ya kushinda na endapo itatokea kushindwa, kushindwa huko kuwe kwa kiwango cha kawaida.

Lengo kubwa ni kuhakikisha tunakuwa na viongozi waliochaguliwa na wananchi kupitia mfumo ambao sote tumeuridhia wa demokrasia ya vyama vingi.

Mazingira ya tathmini hii, yamezingatia kuwa vyama vya upinzani vitaungana vyote nchini na kumsimamisha mgombea mmoja chini ya mwamvuli wa Muungano wa Vyama vya Upinzani Tanzania (MVUTA) dhidi ya chama tawala CCM.

Tukumbuke kuwa uchaguzi mkuu wa Octoba 2015 ulihusisha baadhi ya vyama vya upinzani (UKAWA).Pili tume ya uchaguzi ifanye kazi zake kwa uadilifu na umahiri mkubwa kuhakikisha uchaguzi ni wa amani,huru na wa haki.

Tathmini yangu ina anza na idadi ya Watanzania wanaokadiriwa kufikia milioni hamsini na nne nukta mbili (54.2 milioni).

Idadi hii ina asilimia 50% (27.1 milioni) ya watoto ambao ni chini ya umri wa miaka 18,na watu wazima wanaoruhusiwa kupiga kura asilimia 50% (27.1 milioni) ambao kati yao asilimia 70% (18.97 milioni) wanaoishi vijijini na wanajishughukisha na kilimo na ufugaji pamoja na uchuuzi.

Asilimia 30% ambao (8.13 milioni ) wanaishi mijini ambao wengi wanajishughulisha na kazi mbalimbali.

Kwa mantiki hii ni wazi kuwa chama ili kiweze kupata ushindi mkubwa kinatakiwa kijiimarishe zaidi vijijini ambapo kuna idadi kubwa ya watu ukilinganisha na maeneo ya mijini ambapo kuna idadi ndogo ya watu.

Kwa taarifa na takwimu zilizopo CCM imejiimarisha zaidi vijijini ukilinganisha na muunganiko wa vyama vyote vya upinzani.

Hii inatokana na mambo mengi,moja uwepo wa wajumbe wa nyumba kumikumi,uwepo wa ofisi za chama katika maeno ya vijijini, uwepo wa viongozi wa chama na wale wa serikali wanaojishughulisha na kazi za chama, uwepo wa sherehe mbalimbali kama mwenge, uchumi wa chama na kadhalika.

Katika maeneo ya mijini kwa mijibu wa takwimu na hali ya kisiasa kwa kipindi cha nyuma, wimbi kubwa la vijana hasa wachuuzi (kwa jina maarufu la wamachinga) walivutiwa na sera za upinzani.

Huku idadi kubwa ya kinamama na wazee ikiwa na msimamo wao na imani yao kwa CCM. Kwa baadhi ya vijana sera hizi ziliwavutia kutokana na kukithiri mambo mbalimbali ya kifisadi, kunyimwa fursa za kujipatia kipato kwa kuondolewa sehemu za mijini na kutowajibika kwa serikali kwa wananchi, mgawanyiko ndani ya CCM na kuhama kwa Mh. Edward Lowasa kutoka CCM kwenda UKAWA.

Kundi hili la vijana baada ya kuonekana ni tishio kwa CCM limekumbatiwa na linaweza kuwa na mchango mkubwa katika ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu ujao wa Novemba 2020.

Tangia siku ya kwanza ya Raisi Magufuli kuingia madarakani, makundi tofauti ya wanachi kuanzia wachuuzi, wafanyakazi, wakulima, vijana na kina mama wamepewa fursa na uhuru mkubwa wa kufanya kazi halali zinazowaingizia kipato.

Hivyo basi kurejesha imani yao kwa chama kupita uaminifu aliofanya Raisi wa kutekeleza ilani ya chama sawasawa.

Vile vile ili kuweza kupata idadi ya wapiga kura katika uchaguzi mkuu ujao wa Novemba 2020 turejee takwimu za uchaguzi mkuu uliopita wa Octoba 2015 kama ifuatavyo.

Jumla ya idadi ya Wapiga kura nchi nzima walikua ni 23.3 milioni,kati ya hao asilimia 53% walikua wanawake na 47% ni wanaume.

Idadi kubwa ya wanawake nchini walimuunga mkono Raisi Magufuli ukilinganisha na ile ya wanaume.

Katika historia ya vyama vingi nchini Tanzania, ni uchaguzi mkuu wa Octoba 2015 pekee uliokuwa na hamasa kubwa kutoka kwa vijana wanaoishi mijini juu ya mabadiliko ya uongozi kutoka chama tawala CCM kwenda muungano wa vyama vya upinzani kwa jina la UKAWA.

Uchaguzi huu ulitoa matokeo ambayo kwa tahmini ya wachambuzi wa masuala ya siasa nchini ni ushindi mkubwa kwa upinzani ambao hautaweza kujirudia.

Figure 1. Matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2015

Viashiria vya kushindwa kwa vyama vya upinzani kuelekea uchaguzi mkuu wa Novemba 2020 vinaonekana katika nyanja zifuatazo:-

1. Muundo wa serikali na mabadiliko katika utendaji wa watumishi wa umma.

Serikali ya awamu ya tano imeundwa na aina tatu za viongozi,ambazo ni viongozi vijana, viongozi wataalamu na wachapa kazi,viongozi waadilifu na wachamungu.

Tabia hizi za viongozi wa serikali zimesaidia kuleta matumaini makubwa kwa wananchi na kurejesha imani yao kwa serikali chini ya chama tawala.

Mh Rais amekuwa akisafisha mara kwa mara serikali yake bila kumuonea haya mtu yeyote kwa maslahi ya taifa. Utoaji wa huduma kwa wanachi umekuwa wa haraka na unaofuta maadili ya utumishi wa umma.

2. Maendeleo yanayoonekana katika awamu ya tano, kauli zilizokuwa zimezoeleka za serikali ipo katika mchakato zimeondoka na kauli zakiutekelezaji zimetawala.

Jambo ambalo limekua na matokeo mazuri katika miradi mbalimbali ya kijamii kama vile miundombinu, upatikanaji wa pembejeo, maji, uimarishaji wahuduma za afya na elimu, kukamilisha miradi ya kimkakati katika kuinua uchumi, kuanzisha viwanda na kuongeza ajira kwa watanzania.

3. Matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019.

Kubweteka na kupelekea kushindwa kukidhi masharti kwa wagombea wengi kutoka vyama vya upinzani na baadhi kutoka chama tawala kulipelekea wagombea wengi kuenguliwa katika nafasi za kugombea Uenyekiti wa serikali za mitaa.

Maandalizi makubwa yaliyofanywa na chama tawala yalipelekea kuwepo kwa idadi ndogo ya wagombea walio enguliwa katika mchakato hivyo kuipa ushindi mkubwa katika uchaguzi huo.

Viongozi wa serikali za mitaa wanomchango mkubwa katika kuipa ushindi CCM kwa kutoa matokeo mazuri katika kipindi hiki kabla ya uchaguzi mkuu 2020.

4. Upinzani kupoteza mwelekeo

Vyama vya upinzani vimepoteza mwelekeo na kutokua na sera mbadala za kimaendelo zitakazowavutia watanzania.

Viongozi wake wamekua wakipinga mema ambayo serikali inafanya kwa wananchi pamoja na kusukumwa na matukio.

Matumizi ya mitandao ya kijamii ambayo inakadiriwa kuwa na idadi ndogo ya wapiga kura yamekua njia rasmi kwa wapinzani kuwafikia wananchi huku CCM ikijiimarisha miji na vijijini kupitia vikao na mikutano na wanchi kusikiliza na kutatua changamoto zao.

Idadi ya watumiaji wa Intenet inakadiriwa kufikia milioni 10 kati ya watumiaji hao ni watanzania milioni 6 tu wanafuatilia masuala ya siasa katika mitandao ya kijamii.

Hivyo basi kama mgawanyo wa watu utafuata upenzi wa vyama ni wazi katika watu milioni 6 ni watu milioni moja wanapinga juhudi za serikali katika kuletea wananchi maendeleo.

5. Ushahidi katika tafiti zingine

Tafiti zilizowahi kufanyika nchini na nje ya nchi zinaotoa majibu yafuatayo katika chaguzi mbalimbali:-

No Jina la Mtafiti na Eneo la Utafiti Jina la Utafiti Matokeo ya Utafiti

1 Twaweza 2014 Kuelekea Uchaguzi Mkuu Jumla ya Watanzaia 51% wataichagua CCM, 24% Chadema, 25 % hawajui.

2 Twaweza 2017 Sauti ya Wananchi Asilimia 84% ya wananchi wamesema watapiga kura katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwaka 2020 ikilinganishwa na asilimia 67% ambao walijitokeza katika uchaguzi wa mwaka 2015

Ushindi kwa CCM ni 63% hadema ni 17%

Hitimisho:
Uchaguzi mkuu ujao wa Novemba 2020 utaipa ushindi CCM kwa asilimia zaidi ya 87% huku muungano wa vyama vya upinzani ukiwa na asilimia 13%.

View attachment 1316179
Ushindi ni upepo sio hesabu.Chochote chawezatokea.Endeleeni kuomba busara za mbowe azidi kuwa kondoo ili mbakie madarakani
 
Mkuu huu sio utafiti bali uharo kabisa!!!HUWEZI ANDIKA BANDIKO REFU HALAFU UKAWAPA USHINDI CHAMA CHA MAUAJI !!!ACHA WENGE!!!
 
Muda uliopoteza kuandika upuuzi ungeandika wazo LA biashara na kuliombea mkopo ungeipunguzia familia yako umasikini.

hao unaowasifia hawana habari nawe, wanakulipa posho ya buku 7 kwa post.

Utakufa lofa dogo unang'ang'ana na liccm lenu lichovu
 
Hitimisho:
Uchaguzi mkuu ujao wa Novemba 2020 utaipa ushindi CCM kwa asilimia zaidi ya 87% huku muungano wa vyama vya upinzani ukiwa na asilimia 13%..... Hapa ndipo ulipokosea

Jr[emoji769]
 
Nenda kasome sheria ya vyama vya siasa uone inavyokataza vyama kuungana na kuachiana baadhi ya majimbo etc...
 
Mleta mada, mada yako ni fake. Kwanza ulitakiwa ku-declare kama kweli ndoto yako hii haina conflict of interests?

Pili, kwa mtu yeyote yule mwenye akili timamu awezi kusifia uchaguzi fake wa serikali za mitaa. Kitendo chako cha kuisifia ccm eti ilifanya vizuri kupitia uchaguzi huo kinaonyesha wewe ni punguani na hivyo kufanya mawazo yako yote uliyoyaweka hapa kuwa ya kipunguani.

Tatu, kwa mantiki hiyo hiyo ya uchaguzi fake uliopita wa serikali za mitaa inaonyesha watanzania waliowengi hawana tena imani na chaguzi chaguzi zinazoendelea hapa nchini maana ni idadi ndogo sana ya watu walijitokeza kwenye uchaguzi huo wa uongo uongo. Hivyo inashangaza unaposema eti uchaguzi wa mwaka huu 2020 unatarajiwa kuwa na wapiga kura wengi kuliko wale waliojitokeza 2015. Hizi projections zako hakika nazo ni za kipunguani zaidi.
 
Baada ya kusoma andiko lako kabla hata cjamaliza nimepata jib la moja kwa moja kuwa wewe c mtafiti bali n mwanasiasa kama wanasiasa mwingine kwa nn kwasababu pale tu ulipoanza kuorozesha makundi yanayoukubalu utawala huu kwa kutaja kundi la wafanyakaz ambao toka aingie madarakan huyu mtawala kalitenga hilo kundi utazan Luna kitu lilimkosea hafu unasema no miongon mwa makundi yanayomwunga huyu mtawala. Sasa hakuna kundi ambalo liko ktk majonz kama kund la wafanyakaz ktk utawala huu hivyo mtoa poa hapo karudie tena kufanya tafit zao ktk hili kundi hafu urud tena,kwa mfano mm na kaka yangu ambae kastafu MWAKA Jana kule kijijn tuna kampen Kali sana inayoitwa mikono isambae tusikubar arut huyu mtawala mtaumia akirud tena;
Mkuu labda umeongelea kundi hilo tu moja la wafanyakazi lakini makundi mengi yanalia hata kuliko hilo la wafanyakazi.

Wafanyabiashara hao siyo tu kulia bali wanapiga mayowe kabisa japo hawana mtu wa kuwasikiliza. Wengi wao wamelazimika kufunga biashara kutokana na utawala mbovu wa huyu jamaa. Wakulima ndiyo usiseme, kule kusini walinunua korosho zao wakakaa nazo kisha bila kuwalipa hata cent wakawaita wakulima wakachukue korosho zao tena kwa gharama za wakulima wenyewe.

Kila kundi linaumia kwa njia yake. Wasitaafu hawalipwi posho zao tena, wengine wako mtaani wana karibia miaka minne tokea wamestaafu wanadai hadi baadhi wanakufa kwa dhiki na kuyaacha mafao yao ndani ya consolidated fund ya serikali ya jiwe.

Wanafunzi vyuoni wanataabika, wakijaribu kudai walao haki yao moja tu ya mikopo ili waweze kujikimu serikali inaagiza wafukuzwe vyuoni.

Hadi raia wa kawaida siku hizi uruhusiwi kuhoji chochote, ukihoji ukafahamika umehoji basi jiandae kuozea gerezani kwa kesi za kubambikiwa za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha.

Yaani kwa ujumla hakuna raia asiyeumizwa na mfumo wa utawala wa sasa. Na kutokana na hali ya mambo ilivyo, watu tumekuwa waoga kupita kiasi. Yaani siku hizi kauli za "namwachia Mungu" zimekuwa nyingi mno. Mtu ananyanyasika lakini kwa kuogopa mfumo huu gandamizi, mtu anakaa kimya kwa kisingizio kuwa anamwachia Mungu!!

Hivyo siyo siri inashangaza sana unapoona punguani mmoja anaandika vimada kama hivi vya kipunguani kabisa kama vile yeye siyo mtanzania.
 
Inauma sana kuandika makala ndefu halafu wachangiaji hupati!!
Jifunzeni kuandika bila biasness!Hapa ni mwendelezo wa kuabudu na kusifia!
 
Uwepo usiwepo mpige kura msipige cha msingi jembe jpm atashinda kwa kiwango cha 99.9

USAR

Sent using Jamii Forums mobile app
Kauli ya kipumbavu kupata kutokea. Kiongozi anayeingia madarakani bila ridhaa ya wengi ana nafasi kubwa sana ya kuondolewa kwa njia haramu vilevile, jee ndio mtakavyo iwe?
Kama unapendwa kwa nini ubake?
 
Nimesoma andiko lako, andiko lako liko ''bias'' sana. limejikita kumsifia Magufuli na CCM yake. umesahau kuwa wapiga kura wanatumia vigezo vingi hasa katika kupiga kura, je umefanya analysis ya namna gani hali ya kiuchumi imewaathiri?? pili Uwajibikaji wa serikali kwa wananchi wake kuhusu suala la usalama wao ukizingatia kukithiri kwa matukio ya kutekwa, kuteswa. Je umefanya uchambuzi juu ya ukosefu wa ajira utaiathiri vipi CCM kwenye sanduku la kura??
 
Baada ya kusoma andiko lako kabla hata cjamaliza nimepata jib la moja kwa moja kuwa wewe c mtafiti bali n mwanasiasa kama wanasiasa mwingine kwa nn kwasababu pale tu ulipoanza kuorozesha makundi yanayoukubalu utawala huu kwa kutaja kundi la wafanyakaz ambao toka aingie madarakan huyu mtawala kalitenga hilo kundi utazan Luna kitu lilimkosea hafu unasema no miongon mwa makundi yanayomwunga huyu mtawala. Sasa hakuna kundi ambalo liko ktk majonz kama kund la wafanyakaz ktk utawala huu hivyo mtoa poa hapo karudie tena kufanya tafit zao ktk hili kundi hafu urud tena,kwa mfano mm na kaka yangu ambae kastafu MWAKA Jana kule kijijn tuna kampen Kali sana inayoitwa mikono isambae tusikubar arut huyu mtawala mtaumia akirud tena;
Huyu Kama sio mama kiroboto Yule wakuzika misalaba basi sijui
 
Kama UKAWA ulishindwa,basi MVUTA utakua ,mvutano,tena watavutana dakika ya mwisho,upinzani huwa wanakosea sana hesabu zao,hilo ndilo tatizo.
HESABU ZINAKOSEWA.
 
Uchaguzi wa SERIKALI ZA MITAA ndiyo kilikuwa kipimo lakini napo MKAPORA mchakato wote. Yani hadi RC anapita Bar kuwaambia watu wajiandikishe! Jafo & Rais wanatisha viongozi wa mkoa kuwa kama wasipojiandikisha watu basi watawajibishwa! CCM imegeuka kuwa genge la uporaji badala ya ushawishi wa hoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sayansi na Teknolojia vikitumika vizuri vina uwezo wa kutoa majibu ya wakati ujao,uliopo na uliopita kwa uhakika wa asilimia 99.9%.

Katika andiko langu hili nitatumia taarifa za kisayansi zilizopo kuweza kutoa matokeo ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Novemba 2020.

Tathmini hii isitumike kuwabwetesha wale ambao tathmini itawaonesha wanaweza kushinda ila iwe chachu ya kuwafanya wafanye vizuri zaidi.

Pia kwa wale ambao itaonesha watashindwa nao iwe chachu kwao kujiandaa na kujitahidi kushinda katika maeneo ambayo wananguvu ya kushinda na endapo itatokea kushindwa, kushindwa huko kuwe kwa kiwango cha kawaida.

Lengo kubwa ni kuhakikisha tunakuwa na viongozi waliochaguliwa na wananchi kupitia mfumo ambao sote tumeuridhia wa demokrasia ya vyama vingi.

Mazingira ya tathmini hii, yamezingatia kuwa vyama vya upinzani vitaungana vyote nchini na kumsimamisha mgombea mmoja chini ya mwamvuli wa Muungano wa Vyama vya Upinzani Tanzania (MVUTA) dhidi ya chama tawala CCM.

Tukumbuke kuwa uchaguzi mkuu wa Octoba 2015 ulihusisha baadhi ya vyama vya upinzani (UKAWA).Pili tume ya uchaguzi ifanye kazi zake kwa uadilifu na umahiri mkubwa kuhakikisha uchaguzi ni wa amani,huru na wa haki.

Tathmini yangu ina anza na idadi ya Watanzania wanaokadiriwa kufikia milioni hamsini na nne nukta mbili (54.2 milioni).

Idadi hii ina asilimia 50% (27.1 milioni) ya watoto ambao ni chini ya umri wa miaka 18,na watu wazima wanaoruhusiwa kupiga kura asilimia 50% (27.1 milioni) ambao kati yao asilimia 70% (18.97 milioni) wanaoishi vijijini na wanajishughukisha na kilimo na ufugaji pamoja na uchuuzi.

Asilimia 30% ambao (8.13 milioni ) wanaishi mijini ambao wengi wanajishughulisha na kazi mbalimbali.

Kwa mantiki hii ni wazi kuwa chama ili kiweze kupata ushindi mkubwa kinatakiwa kijiimarishe zaidi vijijini ambapo kuna idadi kubwa ya watu ukilinganisha na maeneo ya mijini ambapo kuna idadi ndogo ya watu.

Kwa taarifa na takwimu zilizopo CCM imejiimarisha zaidi vijijini ukilinganisha na muunganiko wa vyama vyote vya upinzani.

Hii inatokana na mambo mengi,moja uwepo wa wajumbe wa nyumba kumikumi,uwepo wa ofisi za chama katika maeno ya vijijini, uwepo wa viongozi wa chama na wale wa serikali wanaojishughulisha na kazi za chama, uwepo wa sherehe mbalimbali kama mwenge, uchumi wa chama na kadhalika.

Katika maeneo ya mijini kwa mijibu wa takwimu na hali ya kisiasa kwa kipindi cha nyuma, wimbi kubwa la vijana hasa wachuuzi (kwa jina maarufu la wamachinga) walivutiwa na sera za upinzani.

Huku idadi kubwa ya kinamama na wazee ikiwa na msimamo wao na imani yao kwa CCM. Kwa baadhi ya vijana sera hizi ziliwavutia kutokana na kukithiri mambo mbalimbali ya kifisadi, kunyimwa fursa za kujipatia kipato kwa kuondolewa sehemu za mijini na kutowajibika kwa serikali kwa wananchi, mgawanyiko ndani ya CCM na kuhama kwa Mh. Edward Lowasa kutoka CCM kwenda UKAWA.

Kundi hili la vijana baada ya kuonekana ni tishio kwa CCM limekumbatiwa na linaweza kuwa na mchango mkubwa katika ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu ujao wa Novemba 2020.

Tangia siku ya kwanza ya Raisi Magufuli kuingia madarakani, makundi tofauti ya wanachi kuanzia wachuuzi, wafanyakazi, wakulima, vijana na kina mama wamepewa fursa na uhuru mkubwa wa kufanya kazi halali zinazowaingizia kipato.

Hivyo basi kurejesha imani yao kwa chama kupita uaminifu aliofanya Raisi wa kutekeleza ilani ya chama sawasawa.

Vile vile ili kuweza kupata idadi ya wapiga kura katika uchaguzi mkuu ujao wa Novemba 2020 turejee takwimu za uchaguzi mkuu uliopita wa Octoba 2015 kama ifuatavyo.

Jumla ya idadi ya Wapiga kura nchi nzima walikua ni 23.3 milioni,kati ya hao asilimia 53% walikua wanawake na 47% ni wanaume.

Idadi kubwa ya wanawake nchini walimuunga mkono Raisi Magufuli ukilinganisha na ile ya wanaume.

Katika historia ya vyama vingi nchini Tanzania, ni uchaguzi mkuu wa Octoba 2015 pekee uliokuwa na hamasa kubwa kutoka kwa vijana wanaoishi mijini juu ya mabadiliko ya uongozi kutoka chama tawala CCM kwenda muungano wa vyama vya upinzani kwa jina la UKAWA.

Uchaguzi huu ulitoa matokeo ambayo kwa tahmini ya wachambuzi wa masuala ya siasa nchini ni ushindi mkubwa kwa upinzani ambao hautaweza kujirudia.

Figure 1. Matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2015

Viashiria vya kushindwa kwa vyama vya upinzani kuelekea uchaguzi mkuu wa Novemba 2020 vinaonekana katika nyanja zifuatazo:-

1. Muundo wa serikali na mabadiliko katika utendaji wa watumishi wa umma.

Serikali ya awamu ya tano imeundwa na aina tatu za viongozi,ambazo ni viongozi vijana, viongozi wataalamu na wachapa kazi,viongozi waadilifu na wachamungu.

Tabia hizi za viongozi wa serikali zimesaidia kuleta matumaini makubwa kwa wananchi na kurejesha imani yao kwa serikali chini ya chama tawala.

Mh Rais amekuwa akisafisha mara kwa mara serikali yake bila kumuonea haya mtu yeyote kwa maslahi ya taifa. Utoaji wa huduma kwa wanachi umekuwa wa haraka na unaofuta maadili ya utumishi wa umma.

2. Maendeleo yanayoonekana katika awamu ya tano, kauli zilizokuwa zimezoeleka za serikali ipo katika mchakato zimeondoka na kauli zakiutekelezaji zimetawala.

Jambo ambalo limekua na matokeo mazuri katika miradi mbalimbali ya kijamii kama vile miundombinu, upatikanaji wa pembejeo, maji, uimarishaji wahuduma za afya na elimu, kukamilisha miradi ya kimkakati katika kuinua uchumi, kuanzisha viwanda na kuongeza ajira kwa watanzania.

3. Matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019.

Kubweteka na kupelekea kushindwa kukidhi masharti kwa wagombea wengi kutoka vyama vya upinzani na baadhi kutoka chama tawala kulipelekea wagombea wengi kuenguliwa katika nafasi za kugombea Uenyekiti wa serikali za mitaa.

Maandalizi makubwa yaliyofanywa na chama tawala yalipelekea kuwepo kwa idadi ndogo ya wagombea walio enguliwa katika mchakato hivyo kuipa ushindi mkubwa katika uchaguzi huo.

Viongozi wa serikali za mitaa wanomchango mkubwa katika kuipa ushindi CCM kwa kutoa matokeo mazuri katika kipindi hiki kabla ya uchaguzi mkuu 2020.

4. Upinzani kupoteza mwelekeo

Vyama vya upinzani vimepoteza mwelekeo na kutokua na sera mbadala za kimaendelo zitakazowavutia watanzania.

Viongozi wake wamekua wakipinga mema ambayo serikali inafanya kwa wananchi pamoja na kusukumwa na matukio.

Matumizi ya mitandao ya kijamii ambayo inakadiriwa kuwa na idadi ndogo ya wapiga kura yamekua njia rasmi kwa wapinzani kuwafikia wananchi huku CCM ikijiimarisha miji na vijijini kupitia vikao na mikutano na wanchi kusikiliza na kutatua changamoto zao.

Idadi ya watumiaji wa Intenet inakadiriwa kufikia milioni 10 kati ya watumiaji hao ni watanzania milioni 6 tu wanafuatilia masuala ya siasa katika mitandao ya kijamii.

Hivyo basi kama mgawanyo wa watu utafuata upenzi wa vyama ni wazi katika watu milioni 6 ni watu milioni moja wanapinga juhudi za serikali katika kuletea wananchi maendeleo.

5. Ushahidi katika tafiti zingine

Tafiti zilizowahi kufanyika nchini na nje ya nchi zinaotoa majibu yafuatayo katika chaguzi mbalimbali:-

No Jina la Mtafiti na Eneo la Utafiti Jina la Utafiti Matokeo ya Utafiti

1 Twaweza 2014 Kuelekea Uchaguzi Mkuu Jumla ya Watanzaia 51% wataichagua CCM, 24% Chadema, 25 % hawajui.

2 Twaweza 2017 Sauti ya Wananchi Asilimia 84% ya wananchi wamesema watapiga kura katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwaka 2020 ikilinganishwa na asilimia 67% ambao walijitokeza katika uchaguzi wa mwaka 2015

Ushindi kwa CCM ni 63% hadema ni 17%

Hitimisho:
Uchaguzi mkuu ujao wa Novemba 2020 utaipa ushindi CCM kwa asilimia zaidi ya 87% huku muungano wa vyama vya upinzani ukiwa na asilimia 13%.

View attachment 1316179
Ni mawazo yako!
 
Ww na huyo mwenzako mleta mada anayepiga propaganda za kizee, mwambie hakuna mwananchi anayejitambua atashiriki chaguzi za kishenzi chini ya tume hii. Kwa sasa chaguzi zetu chini ya awamu ya tano ni kipimo halisi cha ujinga wa mtu mweusi. Wananchi kwa sasa wanajitambua na wanajua fika hakuna uchaguzi bali uhayawani, ndio maana wengi tulisusia kuajindikisha kupiga kura uchaguzi wa SM. Na huo uchaguzi mkuu tunaojitambua hatutashiriki huo ushenzi, kama dalili ya kuwaonyesha hatuwakubali ccm. Kwa hiyo jiandaeni kukaa madarakani bila ridhaa ya umma bali kama mliopindua nchi, au serikali ya kijeshi. Huo utafiti mwambie akawakoge wasiojua lolote, kwani tunajua fika hamna uwezo tena wa ushawishi, wala kushinda kwa njia ya box la kura linaloheshimiwa.
kweli mkuu, eti CCM iliandaa vyema wagombea wake wote nchi nzima namna ya kujaza form - kweli ujinga wa Mtanzania ndiyo mtaji wa CCM.
 
Ukiwa unaanzisha mada flani kwa ushabiki utaonekanatu umeeanza vizuri lakini hisia zako zilivyokolea ushabiki ukaingia. Kwamfano eti wachambuzi wamesema haijawi kutokea kwa upinzani na haitatokea, what do you mean. Na wingi wa mashabiki sijui sayansi yako ili upimia wapi? Anyway ninachotaka kukisema Mimi hapa nihivi tasmini yoyote ile neutral haitakiwi kubeba ushabiki. Pia Tanzania ya leo huwezi kuigawa kwa kusema kijijini labda kama sijaelewa maana ya kijijini ni nini. Sikuhizi jambo linafanyika Dar sekunde mtu wa Nyamadoke keshajua hats were uliepo dar bado hujalijua na hatakulisikia. Kama Luna kuwa na fair kwenye uchaguzi nchini kwetu uchaguzi ni mgumu sana kama Ligi kuu ya Uingereza samahani kama nitakuwa nimewakwaza hapo.
 
Tunaelekea Uchaguzi mkuu October 28,Endapo tutapiga kura leo JPM anashinda kwa 90%
 
Back
Top Bottom