chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
Kwa maoni yangu, Lissu angejikita katika kujiimarisha katika kugombea nafasi ya urais (japo asingeshinda).
Hata watu wake wa karibu wanasema Lissu ana nguvu sana nje ya chama kwa wananchi wa kawaida ambao wanapiga kura za urais. Kwa nini aliamua kujidhoofisha kwa kugombea Uenyekiti wa chama, hatimaye kusababisha mpasuko? Angebaki na umakamu, na kama angekuwa Rais (hatakuwa Rais) Uenyekiti ungekuja tu
Mpasuko huo unadhoofisha hata nguvu yake katika kugombea nafasi ya urais kwa sababu mahasimu wake ndani ya chama wanamsubiri wahujumu kura zake za urais. Ni mtandao mkubwa wa mahasimu wake ndio anautegenea ulinde kura zake za Urais. Watamshughulikia vilivyo.
Kama sasa hivi tu anawatukana, akiwa Rais? Hakika watapambana kuhakikisha hawi Rais japo ni chadema mwenzao.
Nadhani alipata washauri wasio sahihi, na sasa atakuwa na majuto, japo hatajionyesha hadharani.
Sasa hivi Mbowe yupi atawapa chadema fedha kufadhili urais wa mtu anayemtukana? Mbowe atawekeza kwa wabunge tu, naa Lissu ataachwa ajijue.