Tatizo la Ajali za Barabarani Litatumaliza Watanzania. Je, Kweli Serikali Haiwezi Kufanya Kitu?

Tatizo la Ajali za Barabarani Litatumaliza Watanzania. Je, Kweli Serikali Haiwezi Kufanya Kitu?

Tatizo la ajali za barabarani linazidi kuitafuna taifa la Tanzania na kuwaacha wananchi wakiwa kwenye misiba mizito ya wapendwa wao, pamoja na na simanzi zisizoisha, ni jambo hilo ndilo limenifanya nitakari kwa kina kuhusu ni nini haswa huwa kinawafanya waliokabidhiwa ofisi za umma kuwa na ukakasi linapokuja suala la maamuzi yanayohusu usalama na ustawi wa watanzania kwa ujumla.
View attachment 3125950

Kwa sasa Tanzania imekuwa ni jambo la kawaida kusikia taarifa za ajali huku baadhi tukishuhudia ajali nyingi za barabarani zikitokea katika maeneo kadha wa kadha ndani ya nchi, ajali baadhi zikihusisha vifo na majeraha ya maelfu ya watu katika kiwango ambacho, ninapata hofu kubwa sana. Kwa sasa mioyoni mwa watanzania tunaishi na dhana mbovu katika akili zetu kwamba ajali ni kitu cha kawaida sana, na hivyo kufanya viwango vya kujali miongoni mwetu ndani ya jamii kupungua kwa kiasi kikubwa.

Ni ajabu ila ndo uhalisia, kutokusikia tamko lolote au watu kujitathimini kuhusu ajali iliyotokea kule Mbeya Juni 5, 2024, na kupelekea vifo vya watanzania 16 na kuacha majeruhi wengine kadhaa, tukio hili limechukua nafasi ndogo sana kwenye mijadala ya Watanzania walio wengi haswa ukizingatia wengi wetu ni watu wa kupuuza, kwenye vijiwe vya kahawa, mitandao ya kijamii, ni kama vile hakuna kitu kilichotokea ndani ya ardhi ya Tanzania.
View attachment 3125951

Ajali hii, tumepata kuambiwa kuwa ilitokana na lori ambalo lililogonga gari nyingine mbili baada ya breki zake zote kufeli, ni ajali ambayo imetokea wiki chache tu baada ya ajali nyingine huko Kilwa, mkoani Lindi, ajali ambayo iliondoka na roho za watu 13 na kujeruhi wengine kadhaa hapo Aprili 22, 2024.

Hatufahamu ni wastani wa watu wangapi wanaporwa zawadi zao za uhai au kiwango cha ulemavu ambacho watu hupata wakiwa kwenye barabara zetu kila siku, na nimefanya jitihada za kutafuta takwimu na taarifa mtandaoni kuhusu hili nmetoka mtupu, lakini bila shaka yoyote, hii inatosha kuwa ni ishara zinazonesha kwamba hili ni tatizo kubwa sana ambalo kwa mtu mwene utimamu anaweza kuthutubu kusema linahitaji utatuzi wa haraka, ikibidi hata litangaziwe hali ya dharura na vyombo vya usalama.
View attachment 3125952

Fikiria, katika siku 12 tu ndani ya mwezi Disemba 2023, Tanzania ilipoteza watanzania 46, wastani wa watu wanne kila siku, kwenye ajali za barabarani. Kwa nini hii isiwe ni taarifa ya kupuuza? Ni kwamba RTO za mikoa hawaoni kinachoendelea, je ni kweli SACP Ramadhani Ng’azi ameshindwa kutoa maagizo kwa RTO na kuja na namna ya kuzuia hivi vifo?

Hiki ndio kitu ambacho kinanipeleka kwenye hoja yangu ya msingi, kwamba je, kama wananchi, tumerudhika na kinachoendelea haswa pale ambapo ajali zinatokea?
View attachment 3125955

Tumetosheka na kusema kuwa mapenzi ya Mungu yatimie kwa matatizo na ajali ambazo zinaepukika? Tumekosa imani kuhusu usalama wetu tunapokuwa barabarani kiasi kwamba hata taa zikiruhusu watembea kwa miguu kuvunja barabara basi bado utavuka kwa hofu, ukiogopa bodaboda asije kupita na roho yako?

Fikiria, kama wahalifu wangeingia barabarani na kuwaua watu 13 huko Lindi Aprili mwaka huu, kisha mwezi Mei wakaua watu saba Morogoro, halafu mapema mwezi Juni wakaua watu wengine 16. Je, tungebaki kwenye hali kama ya sasa inayoashiria kutokuwepo kwa utashi wa kufikiria njia za utatuzi wa kitu miongoni mwa wale waliokabidhiwa dhamana ya kulinda maisha na usalama wetu kama raia?
View attachment 3125956

Je sababu ya mwanadamu kupoteza maisha inaweza kuweka uzito katika kutoa maamuzi na ufutailiaji kiasi kwamba maafisa polisi waone kesi ipi inatakiwa ipewe kipaumbele kuliko kesi nyingine?

Je Basi X likipinduka na kuua watu 10, uchunguzi na utatuzi wa tukio hili ni sawa na wahalifu wakitoa roho za watu 10 pale Kihesa Kilolo Iringa? Je udhaifu wa dereva wa basi X ukisababisha ajali na watu 10 wakapoteza maisha ni sawa na mtu mmoja aliyeingia Kariakoo na kupiga risasi na kuwaua watu 10?
View attachment 3125957

Ni mpaka mtu akutwe na mauti ya namna gani ndipo vyombo vya usalama vitaona uzito wake? Ni kifo kipi kinahuzunisha zaidi ya kingine? Kifo cha mtu ambaye amefariki kwa kunywa sumu ni sawa na kifo cha mtu ambaye amegongwa na lori akiwa anavuka kwenye zebra? Ni mazingira gani ya kifo ni ya kuogofya zaidi ya mengine?

Ni kweli Serikali inataka kutuaminisha kwamba hakuna kitu inaweza kufanya kuondokana na tatizo hili linalowajengea hofu Watanzania kuhusu kutumia usafiri wa barabara – usafiri unaotumiwa na mamilioni ya wananchi wa tabaka la chini na, kwa kiwango fulani, lile la kati? Je kuna mtu ambaye ana imani na vibao ambavyo vipo pembezoni ya barabara? Je ni watanzania wangapi wana imani kuwa gari walilopanda breki zake zipo salama?
View attachment 3125958

Je mzazi ana uhakika kuwa mtoto wake akienda shule atarudi salama ikiwa kuna madereva wanaendesha magari kwa fujo kupindukia? Ni nani ambaye ana ujasiri wa kutembea kwenye barabara zetu akiwa na imani ya 100% kuwa gari lililopo nyuma yake linatembea kwa usalama?
View attachment 3125959

Mikakati bora ya serikali inaweza kusaidia uwajibishwaji wa askari wa usalama barabarani ambao wanakula rushwa pamoja na udhibiti wa vyombo vya usafiri vinavyoingia barabarani kuhakikisha ubora. Lakini, kwa nini Serikali kila siku inasema itaifanyia marekebisho sheria ya Usalama wa Barabara na mwisho wa siku hakuna marekebisho yoyote yanafanyika?
View attachment 3125960

Kwa nini Serikali, iliyojijengea sifa ya kupitisha sheria mbalimbali bungeni kwa hati ya dharura, licha ya kulalamikiwa na wadau, inahofia sana kuifanyia marekebisho Sheria ya Usalama Barabarani? Je, inawezekana sababu ikawa ni wamiliki wa mabasi na malori ya mikoani, ambao baadhi yao wanajulikana kuwa vigogo na wafadhili wakubwa wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Bila shaka serikali wanahisi sheria mpya itakinzana na maslahi yao binafsi ya kujitengenezea faida pana zaidi na nono kwa wamiliki wa vyombo hivi vya usafiri. Ni wazi serikali kupitia wizara husika inafahamu kuwa kuna wamiliki wa vyombo vya usafiri ni viongozi wa CCM, ila je ni kweli maisha na ustawi wa viongozi wachache wa CCM ni bora kuliko maisha ya watanzania?
View attachment 3125962

Serikali, pamoja na Bunge, kwa nyakati tofauti tofauti wamekuwa wakali sana kuhusu madereva wa bodaboda nchini na ajali wanazozisababisha ambazo wamekuwa wakizihusisha na uendeshaji wao ulio wa hatari na usiofuata sheria. Sasa kwanini, hatuoni Serikali pamoja na Bunge, zikizungumza kwa hisia kali kuhusu ajali zinazosababishwa na mabasi ya abiria na malori ya mizigo ya mikoni?

Je, sababu inaweza kuwa ni vile hakuna kigogo wa CCM au viongozi wa waliopo serikalini ambao ni wamiliki wa bodaboda na hivyo ni rahisi kuwashambulia bodaboda kila siku na kwa hisia hasi muda mwingine?
View attachment 3125963

Nadhani ifike wakati Serikali iache kurusha mipira yote kwa boda boda kuendeleza visingizio na kuanza kubuni na kutekeleza hatua madhubuti zinazolenga kukomesha ajali za barabarani nchini. Kama watanzania hatuwezi kuendelea kuishi na kufanya mambo yetu kama vile suala la ajali za barabarani ni kama ni suala ambalo Mungu amepanga litokee, kwamba lazima litokee haijalishi hali iliyopo na binadamu hawezi kuzuia.

Ni wakati sahihi sasa kwa serikali kutazama kwa jicho la tatu vifo vya watanzania vinavyotokana na ajali zisizokwisha za barabarani na kujiuliza kama ingeendelea na mambo mengine kama kawaida endapo kama vifo hivyo vingetokana na matukio ya kigaidi, uhalifu au ajali za ndege, na kama jibu ni hapana, ianze kuchukua hatua stahiki sasa na sio kupuuza.
View attachment 3125967

Sehemu ya kuanzia ni kwa Serikali kutimiza ahadi yake ya kuifanyia marekebisho Sheria ya Usalama Barabarani, hatua itakayowezekana tu kwa Serikali kutoa kipaumbele kwa maisha ya Watanzania badala ya maslahi ya kifedha ya wamiliki wa mabasi na malori, pamoja na kushirikiana na wadau wengine katika kutekeleza mikakati mingine imara ya kutokomeza kabisa ajali za barabarani Tanzania. Huku elimu ikitolewa kwa watumiaji wa barabara mara kwa mara ili watu wafahamu wajibu na haki zao wakiwa barabarani.​
Kumbuka hiyo ndo nguvu kazi unapungua yaani walipa Kodi hao ni kitu kidogo cha kufikiria kwa wenye mamlaka lakini mtu akiona familia yake iko salama anapotezea kama vile walokufa mifugo tu
 
Kumbuka hiyo ndo nguvu kazi unapungua yaani walipa Kodi hao ni kitu kidogo cha kufikiria kwa wenye mamlaka lakini mtu akiona familia yake iko salama anapotezea kama vile walokufa mifugo tu
Umeongea jambo la msingi sana
 
Mpaka kila mtu akifahamu nafasi yake
Ni kweli chief,kulaumu nafsi ya tatu (askari wa usalama barabarani,miundombinu mibovu,vilevi n.k) haitoshi, jambo kuu na la msingi ni kujali usalama wako kwanza. Mathalani unapanda gari chakavu, dereva anaendesha huku kashaugwida ugimbi, kunyamazia dereva akiendesha bila kutii sheria za usalama na mengine ya kufanana na hayo.
 
Wazi mkuu
 
Ila Jeshi la polisi usalama barabarani hawakwepi lawama moja kwa moja. Linalo jukumu kubwa la kuhakikisha usalama wa raia barabarani ikiwamo kuhakikisha vyombo vya moto chakavu visiingie barabarani, dereva anaendesha kwa kufuata sheria na bila kutumia vilevi na mengineyo! Ila badala yake wote tunaona mambo ya hovyo tu wanayofanya.
Tunaendelea kungoja siku ile ambayo atatokea amiri Jeshi aliyechoshwa na huu uozo wao atoe kauli ambayo itawarudisha kwenye mstari sio mambo ya kubrashi viatu.Wanyooke kama rula na sisi tutapone.
 
Kabsa Mkuu
 
polisi wanapojaribu kuwa wakali watu wanaleta siasa.juzi kuna traffic kapigwa kapasuliwa uso kisa kusimamisha gari na kutaka kuwashusha abiria waliokuww wamepangwa kwenye coridor isiyo na siti ndani ya bus.
kilichonisikitisha zaidi ni mpaka wanaharakati wetu tunaoamini wameenda shule na wameelimika kule X wanashangilia kwamba ni dalili kwamba raia uoga unawatoka sasa,wanapiga askari wajinga wajinga,sawa.

ujinga wa watanazania wengi umewafanya kuwa shamba la kuvunia umaarufu kwa wajanja,mtaji wa kisiasa kwa wanasiasa wahuni,kichaka cha wahalifu kujificha,na ngazi ya kupanda kuufuata ukwasi kwa wenye nia hiyo.

ni bongo tu magari yatakimbizana kuwahi kufika kituo B ukute kuna watu walibeti nani mshindi.

ni bongo tu bodaboda ataendesha piki piki kichwa wazi akikimbia sana huku anapigiwa miruzi,abiria wake akiulizwa kwanini havai kofia anasema ina chawa.

ni bongo tu,ambapo speaker atasisitiza mabus yasafiri usiku pamoja na maroli na yeye hapandi mabus,akijua kabisa barabara zenyewe ni metre 6 tu two way.

bongo tu kosa la barabarani fine ni elfu 30 hata ukiendesha umelewa,huna break,au tyre vipara unawezalipa fine yakaisha,kwa wenzetu kuna makosa hawataki kabisa kihela chako utaenda mahakamani.

kifupi tuna kazi ya kumuomba Mungu atulinde halafu tuna kazi ya kuwa makini pia.wenzetu wameamua tu kuwa makini moja kwa moja na kushughulika na wanayoyaweza.
 
Maua yako mkuu 🌹
 
Barabarani, hatua itakayowezekana tu kwa Serikali kutoa kipaumbele kwa maisha ya Watanzania badala ya maslahi ya kifedha ya wamiliki wa mabasi na malori, pamoja na kushirikiana na wadau wengine katika kutekeleza mikakati mingine imara ya kutokomeza kabisa ajali za barabarani Tanzania. Huku elimu ikitolewa kwa watumiaji wa barabara mara kwa mara ili watu wafahamu wajibu na haki zao wakiwa barabarani.
Tuanze na ripoti kamili za ajali. Ajali itolewe taarifa kamili kutoka kwenye 'tume' maalumu. Na sio tume iwe ndio utaratibu wa kawaida wa polisi na usalama barabarani kuhusiana na ajali.

Baada ya hiyo ripoti yenye majibu kamili wa ajali na jinsi ilivyotokeatokea na uhisika wa wote waliowajibika kuanzia fundi wa gereji aliyetengeneza breki, mmiliki aliyegoma kurekebisha kioo, dereva ambaye hakukata kona labda wooote (hadi nafasi ya wahanga kutovaa mikanda, helmenti na kujaa) kila mmoja na uhusika wake WAWAJIBISHWE!
 
Ukweli ni kwamba Sheria ya Usalama Barabarani Sura ya 168 inahitaji marekebisho makubwa sana.
Mfano tu;
Baraza la Taifa la Usalama barabarani litaongozwa na Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti na wajumbe wasiopungua 10 wanaoteuliwa na waziri anayehusika na masuala ya usalama barabarani. Kazi kubwa ya Baraza ni kutoa mwongozo juu ya kuongeza maarifa na njia mbali mbali zitakazoweza kuimarisha hali ya usalama barabarani.
Hili baraza linatakiwa lichaguliwe na watumiaji wa barabara sio waziri kwa sababu waziri kuja kukutana na ajali ni nadra sana!​
 
Media hazitumiki vizuri kunufaisha jamii, elimu elekezi ya Matumizi ya Barabara (pamoja usalama katika sector nyingine,) sio lazima itolewe chuoni, media zinasaidia kwa sababu udereva ni maisha endelevu kama media zenyewe.
 
Media hazitumiki vizuri kunufaisha jamii, elimu elekezi ya Matumizi ya Barbara (pamoja usalama katika sector nyingine,) sio lazima itolewe chuoni, media zinasaidia kwa sababu udereva ni maisha endelevu kama media zenyewe.
Media zetu zipo busy kuonesha nyimbo na shows pekee mkuu
 
Kipindi nimechapisha andiko hili kuna watu waliniambia kuwa halina point wala mashiko!
Kinachoendelea sijui ni kitu gani!? 😔
Tanzania Traffic mna kazi kubwa sana
 
Back
Top Bottom