Juzi nilienda hospotali, katika kuchukua vipimo, dokta akaniambia nilikuwa nakaribia kupata ugonjwa wa kisukari, kwani alianiambia kwamba kipimo kilionyesha 18 badala ya 5,6 au 7 ambayo ni ya kawaida sana. Sasa akaniambia nibadili utaratibu wa kula na kunitaka kula wali na ugali kwa uachache sana huku mbogamboga na maji yakivipa nafasi kubwa, akasisitiza nitumie sana jamii ya maharage na samaki na tunda la tango. Na pia kuachana na sukari yenyewe na kufanya mazoezi ya mara kwa mara.
Miye nilikuwa mnywaji mzuri wa juice ya miwa, machungwa na juice ya tende ambayo imechanganywa na maziwa. Bahati mbaya sikumuuliza vitu kama tende na juice ya muwa inafaa tena?
Kama kuna mtu ana uelewa wa ulaji wa matunda naomba anifahamishe hapa, ninaamini na wenginen wataweza kupata taarifa na kuwa na uelewa jinsi ya kuepukana na ugonjwa huu ambao unawatafuna Watz wengi, natanguliza shukrani.