Tatizo la Gonjwa la Sukari (Diabets Mellitis): Fahamu chanzo, aina na ushauri wa tiba ya tatizo hili

Tatizo la Gonjwa la Sukari (Diabets Mellitis): Fahamu chanzo, aina na ushauri wa tiba ya tatizo hili

Acha bia,kula konyagi tu ,pia jitahidi japo kupiga push ups japo 20 asubuhi na jioni na pia punguza stress kama unamke piga sana mechi utoe jasho na maji kunywa hasa
 
Asante ila sijawa mkaidi@Zamiluni Zamiluni.
Mpendwa Simba
sijakusukusudia uwe mkaidi... ila nikujuze mapwma tu kuwa ugonjwa huu huleta ukaidi na ujenga hoja kuwa wewe ndiyo mwenye haki ktk kila jambo ( mwenye kisukari) hukaidi ushauri wa nje !! ( hii ni nature)
Nakuombea amani na afiya njema
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ni afadhali upate HIV kuliko kupata diabetes mellitus.

Hiyo kitu ni balaa,it has lots of complications.
 
Juzi nilienda hospitali, katika kuchukua vipimo, dokta akaniambia nilikuwa nakaribia kupata ugonjwa wa kisukari, kwani alianiambia kwamba kipimo kilionyesha 18 badala ya 5,6 au 7 ambayo ni ya kawaida sana. Sasa akaniambia nibadili utaratibu wa kula na kunitaka kula wali na ugali kwa uachache sana huku mbogamboga na maji yakivipa nafasi kubwa, akasisitiza nitumie sana jamii ya maharage na samaki na tunda la tango. Na pia kuachana na sukari yenyewe na kufanya mazoezi ya mara kwa mara.

Miye nilikuwa mnywaji mzuri wa juice ya miwa, machungwa na juice ya tende ambayo imechanganywa na maziwa. Bahati mbaya sikumuuliza vitu kama tende na juice ya muwa inafaa tena?
Kama kuna mtu ana uelewa wa ulaji wa matunda naomba anifahamishe hapa, ninaamini na wenginen wataweza kupata taarifa na kuwa na uelewa jinsi ya kuepukana na ugonjwa huu ambao unawatafuna Watz wengi, natanguliza shukrani.

Nimeona swali lako, Na ningependa kupa ushauri wangu kama mtaalamu wa madawa na tiba.

1. Daktari wako kakushauri vizuri sana juu ya mabadiliko ya maisha. Ni vyema ufanye mazoezi. Unaweza kutembea kwa muda wa nusu saa kila siku.

2. Ni kweli inabidi upunguze vyakula kwenye jamii ya "carbohydrates" kama wali, ugali, mahindi, viazi na viazi tamu.

3. Inabidi upunguze juice na vitu vyote vya sukari kama miwa, juice ya tende na juice za matunda. Ni bora ule hizo matunda kuliko kunywa juisi yake, Hii ni kwasababu juisi inaingia ndani ya damu haraka zaidi. Matunda inachukua mudaa. Hivyo basi, unaweza kula matunda kwa kiasi. Alafu pia, ni vizuri kunywa maji kati ya lita 3 mpaka 4 kila siku. Inakuwa glasi 6 mpaka 8.

Asante.

Majibu juu ya maswali ya magonjwa, dawa na tiba
 
Juzi nilienda hospitali, katika kuchukua vipimo, dokta akaniambia nilikuwa nakaribia kupata ugonjwa wa kisukari, kwani alianiambia kwamba kipimo kilionyesha 18 badala ya 5,6 au 7 ambayo ni ya kawaida sana. Sasa akaniambia nibadili utaratibu wa kula na kunitaka kula wali na ugali kwa uachache sana huku mbogamboga na maji yakivipa nafasi kubwa, akasisitiza nitumie sana jamii ya maharage na samaki na tunda la tango. Na pia kuachana na sukari yenyewe na kufanya mazoezi ya mara kwa mara.

Miye nilikuwa mnywaji mzuri wa juice ya miwa, machungwa na juice ya tende ambayo imechanganywa na maziwa. Bahati mbaya sikumuuliza vitu kama tende na juice ya muwa inafaa tena?
Kama kuna mtu ana uelewa wa ulaji wa matunda naomba anifahamishe hapa, ninaamini na wenginen wataweza kupata taarifa na kuwa na uelewa jinsi ya kuepukana na ugonjwa huu ambao unawatafuna Watz wengi, natanguliza shukrani.
Mpendwa Simba
sijakusukusudia uwe mkaidi... ila nikujuze mapwma tu kuwa ugonjwa huu huleta ukaidi na ujenga hoja kuwa wewe ndiyo mwenye haki ktk kila jambo ( mwenye kisukari) hukaidi ushauri wa nje !! ( hii ni nature)
Nakuombea amani na afiya njema
Hii video inatoa elimu na maarifa juu ya kisukari. Ifuatilie kwa makini.



Kitabu kinaeleza yale yaliyosemwa kwenye video link http://biswaroop.com/wp-content/upl...re-diabetes-type-I-II-within-72-hrs-ebook.pdf



 
Pole sana mkuu,mwenye kujua exactly aina za vyakula,kiwango & muda wa kula mgonjwa w kisukari amsadie hyo ratiba
 
Juzi nilienda hospitali, katika kuchukua vipimo, dokta akaniambia nilikuwa nakaribia kupata ugonjwa wa kisukari, kwani alianiambia kwamba kipimo kilionyesha 18 badala ya 5,6 au 7 ambayo ni ya kawaida sana. Sasa akaniambia nibadili utaratibu wa kula na kunitaka kula wali na ugali kwa uachache sana huku mbogamboga na maji yakivipa nafasi kubwa, akasisitiza nitumie sana jamii ya maharage na samaki na tunda la tango. Na pia kuachana na sukari yenyewe na kufanya mazoezi ya mara kwa mara.

Miye nilikuwa mnywaji mzuri wa juice ya miwa, machungwa na juice ya tende ambayo imechanganywa na maziwa. Bahati mbaya sikumuuliza vitu kama tende na juice ya muwa inafaa tena?
Kama kuna mtu ana uelewa wa ulaji wa matunda naomba anifahamishe hapa, ninaamini na wenginen wataweza kupata taarifa na kuwa na uelewa jinsi ya kuepukana na ugonjwa huu ambao unawatafuna Watz wengi, natanguliza shukrani.
Inategemea pia na sababu za awali zilizopelekea uwe na hali ya sukari ya juu kwenye damu (kisukari ). Mzazi wangu mmoja aliwahi kusumbuliwa na hilo tatizo ila mpaka Mara ya mwisho amepimwa sukari random sio fasting ilikuwa 7 na ya wastani miezi mitatu nyuma kipimo kilisoma 5. Daktari akawa anashangaa na kisha akauliza amewezaje.
Mambo haya yalimsaidia:
1. Aliacha kutumia sukari
2. Alihakikisha digestion yake haiwi disturbed, kwa kula mboga za majani kwa wingi,anakula mapapai kiasi na matango zaidi.
3. Hatumii mahindi, anatumia ugali wa mtama mweupe size ya ngumi yake. Inasemekana mahindi yanasukari inayoachiwa haraka na kupandisha sukari kwenye damu (high glycemic index sijui wanavoita wataalamu!!) Amepunguza matumizi ya hamira na ngano pia: hivi huweza kusababisha inflammation ya tumboni na kuvuruga mmeng'enyo na hivyo kustisturb blood sugar levels.
4.Anatumia kachumbari asubuhi, inakuwa na mchanganyiko wa tango,nyanya,kitunguu, pilipili hoho, kama Kuna karoti au parachichi anaweza kula au kuongezea.
5.pia kurahisisha digestion anakula bamia mbichi moja au analoweka vipande vya bamia kwenye maji usiku asubuhi anakunywa. Inasaidia bowel movement.
6. Anakunywa maji mengi, anaanza kunywa maji toka asubuhi na anatembea nayo.
7.anafanya mazoezi ya kutembea jioni akitoka kazini.
8. Ana hakikisha analala vizuri, saa 2 usiku anakuwa amekula mlo wa usiku analala saa 4 labda awe na shughuli fulani imlazimu kuchelewa.
9. Alikuwa anaendelea kunywa dawa kwa sababu alikuwa ameshaambiwa ni diabetic.
Note: daktari mmoja mtaalamu wa kisukari clinic moja iko upanga alishauri watu kula matunda kama snack maana watu wanaogopa matunda kwamba Yana sukari. Usile mlo na matunda, matunda kula kwa wakati wake mf. Katikati ya milo miwili.
Hayo ndo niliyoshuhudia, chukua hatua zitakazofaa
 
Safi sana nahisi utakuwa umempa njia za kupambana na tatizo
 
Nina kisukari (IDDM) kwa miaka kadhaa sasa. Na unaweza usiamini, lakini the best doctor for you is actually YOU! Fahamu kinachokufaa na kisichokufaa, kwa bahati mbaya kisukari hakina formula ambazo ni applicable kwa wote. Kuna vitu utafanya na vitafanya kazi kwako na si kwa mwingine and vice versa.
 
Hili gonjwa hatari sana inaondoa mtu na afya yake. Nishapoteza ndugu wa karibu kwa gonjwa hili na mtihan mkubwa ni kufata hayo masharti ikiwemo kupunguza au kuacha kabisa yale maji ya dhahabu.
 
Hivyo vitu vyote vya sukari; tende, maziwa, miwa kwa sasa ungeacha, katika chakula chako kwa mfano wali kama utaweza kuweka vijiko 3/4 vya chakula kwenye sahani na vingine ikawa mchicha na mfano maharage, kimbia asubuhi au jioni kwa lisaa limoja, unaweza kuanza na dakika 20 na kuongeza mpaka zifike 60 lakini mazoezi, kunywa maji angalau lita 2 kwa siku na kupunguza vyakula vya wanga ni njia nzuri ya kucontrol sugar mwilini.
menu hii mbona ni kama ya kimiss!
 
Ugonjwa wa kisukari unasababishwa na under secretion ya insulin kazi ya insulin ni Ku convert excess sugar into Glycogen na kuhifadhi under muscles
 
madhara-ya-kisukari.jpg




Tuliona katika ukurasa mwingine kuwa kisukari ni ugonjwa ambao humsababishia mtu kuwa na kiwango kikubwa cha sukari katika damu na kushindwa kuitumia sukari hiyo ipasavyo ili kumpa nguvu na hivyo sukari hiyo kutoka nje ya mwili wa mgonjwa kupitia njia ya mkojo. Ugonjwa huu pia huitwa Diabetes Mellitus, maneno yanayotokana na kigiriki na kilatini. Diabetes linatokana na kigiriki likimaanisha kijibomba kinachonyonya maji na mellitus linatokana na neno la kilatini “Mel” lenye maana ya asali, hivyo diabetes mellitus ni “kunyonya maji yenye utamu kama asali” baada ya madaktari wa enzi hizo kugundua kuwa mkojo na damu ya mgonjwa wa kisukari vilikuwa na glucose kwa wingi sana.

Wachina wa zamani nao waligundua kuwa mchwa walijaa kwa kwingi kwenye eneo la mkojo wa mtu mwenye kisukari kutokana na mkojo huo kuwa mtamu na wakatoa neno “Sweet Urine Disease” -Ugonjwa wa kutoa mkojo mtamu.



Insulin Na Kongosho


Insulin ni homoni inayotoa ishara kwa seli za mwili ili ziweze kuchukua glucose kotoka kwenye damu na kuitumia katika kuupa mwili nguvu na kuujenga. Kama kiwango cha insulin mwilini ni kidogo au hakuna insulin kabisa katika mwili, glucose haitachukuliwa na seli za mwili hivyo kusababisha mwili kuyeyusha mafuta yaliyomo mwilini ili upate nguvu.

Insulin karibu za wanyama wote hufanana, tofauti ni katika nguvu ya ufanyaji wake wa kazi. Kwa mfano, insulin ya nguruwe “Porcine insulin”, inafanana sana na insulin ya binadamu, hii ikiwa na maana kuwa binadamu anaweza kutumia insulin ya wanyama. Lakini kwa bahati nzuri, insulin inaweza kutengenezwa kwenye maabara.

Kongosho ni sehemu ya viungo vilivyo katika mfumo wa uyeyushaji (mmeng’enyo) wa chakula na kinapatikana sehemu ambapo mbavu hukutana kwa chini. Kongosho lina umbo la jani na lina urefu upatao kama nchi sita. Kongosho ina kazi ya kutengenza insulin na homoni zingine za kusaidia uyeyushaji wa chakula.



Dalili Za Kisukari Ni Zipi?


Baada ya kujikumbusha hayo, sasa tutazame mambo ambayo yakikutokea ujue kwamba ni dalili za kuwa na ugonjwa huu wa kisukari. Watu wengi wanakuwa na ugonjwa huu bila kujijua kwa sababu dalili za awali za ugonjwa huu hazimsababishii mtu kushindwa kuendelea na shughuli zake za kawaida, lakini ni vizuri kuugundua ugonjwa huu katika hatua zake za awali ili kuepukana na madhara makubwa yanayoweza kutokea baadaye. Tutaorodhesha hapa dalili zinazojionyesha mara nyingi zaidi:

Kukojoa mara kwa mara: Jee, umekuwa na tabia ya kwenda kupata haja ndogo mara kwa mara? Kama jibu ni ndiyo, basi figo zako sasa haziwezi kuirudisha glucose kwenye mfumo wa damu na badala yake zinachukua maji kutoka kwenye damu na kusababisha kibofu kijae mara kwa mara.

Kiu Isiyoisha: Kama unakojoa mara kwa mara, utapata kiu isoisha kwa sababu mwili unahitaji kurudisha maji uliyopoteza kwenye mkojo.

Njaa Kali: Kama isulin yako haifanyi kazi au kama huna insulin, mwili wako unakosa glucose ya kuupa nguvu. Katika kutafuta njia nyingine ya kupata nguvu, mwili utakuwa na njaa ili uupatie chakula.

Kuongezeka kwa uzito (unene): Hii inatokana na dalili ya kusikia njaa kali.

Kupungua uzito kusiko kawaida: Hili huwatokea zaidi wagonjwa waType 1 Diabetes kwa sababu kwa kukosa insulin na seli kukosa chanzo cha kupata nguvu, mwili huanza kuvunjavunja misuli na kuyeyusha mafuta ya mwili ili upate nguvu hiyo hali inayochangiwa zaidi na tabia ya kisukari cha aina hiyo kujitokeza kwa ghafla.

Uchovu wa mwili: Mwili unapokosa glucose ya kuzipa seli nguvu, uchovu hutokea.



dalili-za-kisukari.png




Hasira: Hasira zinaweza kuwa ni sababu ya mwili kukosa nguvu.

Kutoona vizuri: Ugonjwa huu husababisha mtu kushindwa kuviona vitu vizuri. Tatizo hili hutibika lakini mara nyingine hali huweza kuwa mbaya kiasi cha kuwa na tatizo la kudumu au kupata upofu.

Vidonda kutopona vizuri au haraka: Unapokuwa na sukari nyingi katika damu, uwezo wa mwili kuponya vidonda hupungua.

Magonjwa ya ngozi: Mwili wenye sukari nyingi ndani ya damu huwa na uwezo mdogo sana wa kujiponya kutokana na maambukizi ya wadudu. Wanawake wenye kisukari huwa na maambukizi zaidi na hupata shida kubwa ya kuponya maambukizi ya sehemu nyeti za miili yao.

Kuwashwa kwa ngozi: Kuwashwa kwa ngozi mara nyingine ni dfalili ya kuwa na kisukari.

Kuwa na fizi nyekundu au zilizovimba: Fizi nyekundu na/au zilizovimba huweza kuwa kuwa ni dalili ya kuwa na ugonjwa wa kisukari, mara nyingine meno hulegea.

Uwezo mdogo wa kushiriki tendo la ndoa: Hili ni tatizo hasa la wanaume wenye umri unaozidi miaka 50, ambapo mara nyingi watakosa uwezo wa kushiriki tendo la ndoa kikamilifu au uwezo wao wa kufanya tendo hilo kufa kabisa (Erectile Dysfunction).

Ganzi mikononi au miguuni: Uzidifu wa sukari mwilini huweza kuharibu neva au mishipa midogo ya damu inayolisha neva, hivyo kusababisha hali ya ganzi mikononi au miguuni.





kisukari-four.jpg




Madhara Ya Kisukari


Kama ugonjwa wa kisukari hautadhibitiwa ipasavyo, madhara makubwa huweza kutokea. Baadhi ya madhara ambayo yamehusishwa na ugonjwa huu ni kama ifuatavyo:

  • Matatizo ya macho-glucoma, cataracts na mengineyo.
  • Matatizo ya miguu-vidonda na gangrene ambavyo mara nyingine husababishwa miguu ikatwe.
  • Matatizo ya moyo-pamoja na upungufu wa damu inayoelekea kwenye misuli ya moyo.
  • Hypertension-ambayo huweza kulsababisha figo kushindwa kufanya kazi, matatizo ya macho, magonjwa ya moyo na kiharusi.
  • Matatizo ya kusikia-kisukari husababisho tatizo la kushindwa kusikia vizuri.
  • Gastroparesis-misuli ya tumbo kushindwa kufanya kazi yake vizuri.
  • Kiharusi (Stroke)-endapo blood pressure, cholesterol na sukari havitadhibitiwa, uwezekano wa kupatwa na kiharusi huwa ni mkubwa sana.
  • Ugumba-kisukari humfanya mgonjwa ashindwe kufanya tendo la ndoa.
Katika ukurasa unaofuta tutajadili chakula na mazoezi ya mgonjwa wa kisukari na ukurasa mwingine wa mbele utajadili tiba ya kisukari kwa kutumia insulin.

Usisite kuuliza swali au kutoa maoni yako kuhusu mada yetu ya leo, tutafurahi sana kukujibu.
 
Kunywa maji mara kwa mara,kukojoa mara kwa mara pia huitaji wa kinywaji cha sukari mfano unaweza ukawa unahitaji sprite mostly of the tym,then about chakula inategemea uko na sukari ya aina gani so its better ukaenda hospital for chekup il uwe aware mapema.
HII YA KUNYWA MAJI MARA KWA MARA inatafasirika vipi? Maana kuna watu tunakunywa maji sana ili kuweka mwili sawa. Na ukinywa maji sana maana yake ni kwamba utakojoa sana pia!

Kwa mgonjwa Wa kisukari inakuwaje? Anaskia kiu Mara kwa Mara au nini hufanya anywe maji sana?
 
Back
Top Bottom