Ni tumaini langu wote mu wazima wa afya.
Kama mada ilivyo hapo juu,leo nimekuja kuomba msaada.
Nina ndugu,mwana mama mtu mzima. Kwa mda wa miaka 10 sasa,ana tatizo la kuanguka. Kwa siku inaweza tokea zaidi ya mara tatu. Na si kwamba ni kila siku,inaweza ikapita hata wiki au wiki mbili. Na si kifafa. Akianguka inakuwa kama vile kapatwa na kizuguzungu,lakini akirudi katika hali yake,anakuwa hakumbuki kama hali hiyo imemtokea.
Kwa yeyote anayejua mtu wa kusaidia,tafadhali naomba tuwasiliane inbox. Kila tulipojaribu wanadai watatibu,wanaishia tu kula pesa basi.
KUPOTEZA FAHAMU
Kupoteza fahamu ni kitendo kinachotokea kutokana na sababu mbalimbali kwenye mwili. Mara nyingi sababu hizi hupelekea ubongo kutokupata oksijeni na chakula cha kutosha.
Ili kufikia mwelekeo au hitimisho la sababu halisi inayosababisha mtu kupoteza fahamu ni muhimu sana mhusika kusikilizwa kwa makini sana kwani maelezo huchangia kutambua ni kiungo au mfumo gani wa mwili wenye kasoro.
1: Kupata historia kamili ya maisha ya mgonjwa
2: Mazingira ambayo hupelekea mtu kupoteza fahamu.
3: Hali ambayo mhusika hujiaikia kabla ya kupoteza fahamu.
4: Hali ambayo mhusika huwa nayo wakati wa kupoteza fahamu
5: Muda ambao mhuaika huchukua mpaka fahamu kurejea.
6: Hali ambayo mgonjwa huwa nayo baada ya kurejea kwenye fahamu zake.
7: Vipimo hutegemea na yale atakayong'amua mtaalamu wa afya.
8: Tiba hutegemea na kilichofikiwa kama tatizo la msingi.
Hapa chini ni baadhi ya kasoro kwenye mwili zinazoweza kusababisha mtu kupoteza fahamu:
1: Kasoro ya mapigo ya moyo (juu vs chini).
2: Kasoro ya maumbile ya moyo valvu.
3: Kasoro ya mishipa ya damu kuwa midogo/stenosis.
4: Tatizo la presha kuwa juu vs chini.
5: Tatizo la mishipa ya fahamu kwenye ubongo.
6: Tatizo la sukari kuwa juu au chini.
7: Kupoteza fahamu kutokana na hali au mazingira. Mfano: usipokunywa maji ya kutosha, stress, uoga vs panic, njaa, matumizi ya pombe, kujisaidia haja ndogo na kukohoa kwa nguvu nk.
8: Kubasiliaha mkao au mwelekeo wa mwili. mfano: kutoka kulala kwenda kukaa au kusimama.
9: Shida kwenye mishipa ya moyo.
10: Kutanuka kwa moyo na kufeli
11: Kipanda uso/migraine
12: Kuongezeka kwa preasure kwenye eneo la ubongo/fuvu kwa kuongezeka chochote, mfano: majimaji nk.
13: Matumizi ya baadhi ya dawa
NB: Kwa kuangalia wigo wa matatizo husika ni vyema mhusika kufikishwa kwenye kituo cha afya na kusikilizwa vyema na daktari/ukimpata bingwa wa magonjwa ya ndani(physician), kufanyiwa ukaguzi na vipimo mwafaka ni vyema sana.
Ni vizuri mgonjwa huyu kuandamana na mtu aliyewahi kumuona akipoteza fahamu kama ikiwezekana pia au anaejua vyema historia ya maisha yake.