Tatizo la kuchangisha walimu mchango wa mwenge

Tatizo la kuchangisha walimu mchango wa mwenge

siyo walimu tu.. ni wafanyakazi wa halmashauri, walio chini ya Mkurugenzi wakiwepo wauguzi , madaktari mpaka madereva.

Sasa ukilalamika sana mwalimu itaonekana walimu walalamishi, na itaonekana unataka hiyo michango iondolewe kwa walimu tu..
hoja ya ku discuss hapa
1 . Nini umuhimu wa mwenge kwa kizazi cha leo.?

2. je ni kweli mwenge ni zindiko la nchi, kana kwamba hata CHAUMA wakiingia madarakani hawawezi kuugusa .. si umeona Jiwe, shujaaa. aliona bora afute hata ajira za ualimu lakini hajawahi gusa gharama za mwenge.
soma kuhusu F.Ganze Masta mchawi wa Taifa.

3. vipi kama kuna CAG, kuna viongozi , kwa nini hasa mwenge uzindue miradi?

Mi naona mwenge ni kama sherehe flani za kitaifa, ni kama Carnival festival za kule Brazil, ama ma dragon ya kule china. sema wabongo wengi tuna potezea...

NYONGEZA. NJE YA MADA KIDOGO.
Njiani porini huko ni kweli mwenge huwa una zimwa ku save wese?

baada ya kukimbiza mwenge hawa wakimbizaji huwa "wanapotea"?

Nakujibu hilo la mwisho eti wakimbiza mwenge wanapotea!
Hakuna kitu kama hicho! Humu jf wapo waliokimbiza mwenge miaka na miaka mbona hawajapotea...!?
Ni nani unayemfahahamu aliyewahi kimbiza mwenge na akapotea....!??
Acha tuwazoom tu, mnavyodanganyana!
 
28 May 2023
Nsimbo, Tabora
Tanzania

Tundu Lissu aanika madudu, afichua siri nzito kuhusu tozo na kodi za kimabavu



Operasheni 255 ya CHADEMA Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo, Tabora Tanzania madudu mengi ya tozo na michango isiyo halali kisheria na ya kimabavu .
 
Back
Top Bottom