Tatizo la kukatika umeme mara kwa mara ifikapo saa moja usiku mpaka saa nne

Tatizo la kukatika umeme mara kwa mara ifikapo saa moja usiku mpaka saa nne

Marathon day

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2020
Posts
643
Reaction score
1,016
Ndugu wahusika,

Mimi ninatatizo la hizi aina ya MITA za TANESCO Mpya, Yaani maeneo yangu IFIKAPO jioni ya saa 12 jioni mpaka saa 4 usiku ni shida Kila dakika Moja umeme unakatika na kuwaka mfululizo, cha ajabu majirani zangu umeme upo mda wote.

Nilijaribu kuulizia Taneco wanasema aina ya MITA inakata umeme pindi umeme unapokua mdogo ( low voltage) Nafanyaje nibadilishiwe Miter?

Jirani zangu ambao wamefunguwa umeme mbele yangu tatizo Hilo hawana, ila Mimi tu ndio napata shida hii, naomba msaada kwa juzi wa mambo.
 
Unapata umeme mdogo it seems line yenu imezidiwa, ongea na jamaa wakubadilishe kwenye line nyingine. Sasa Kama umesema huwa hautoi hongo nadhani endelea kuteseka.
 
Line imezidiwa, leta fundi toka TANESCo akubadilishie line na kwa kuwa umesema uhongi basi mpe fundi pesa ya chai la sivyo utaendelea kulalamika mpaka kesho.
 
Line imezidiwa, leta fundi toka TANESCo akubadilishie line na kwa kuwa umesema uhongi basi mpe fundi pesa ya chai la sivyo utaendelea kulalamika mpaka kesho.
Nitafanyia kazi ushauri wako, nibadili Jina la RUSHWA kuwa PESA YA CHAI.
 
Line imezidiwa, leta fundi toka TANESCo akubadilishie line na kwa kuwa umesema uhongi basi mpe fundi pesa ya chai la sivyo utaendelea kulalamika mpaka kesho.
@Tanesco kumbe ndo zenu?? Mshakua kama TRAFFIC??

Hongo nje nje??
 
Niko na shida kama hii, yaani ni kero, majirani wote wametulia ila hapa kwangu ndio kuna hii shida
 
Zile mita za tanesco ni uchafu kwa kweli zinakela hatari hafu umeme ukikatika kwa muda mrefu ukiludi zenyewe umeme auludi mpaka lipite saa 1 au 2.
 
Back
Top Bottom