Tatizo la kukohoa usiku

Tatizo la kukohoa usiku

Nilienda makete kipindi fulani aisee ile baridi ni kali na nahisi nilipata numonia, je kwa mtu miaka 27 anaweza pata numonia ndo bado nawaza hapa?
 
Habari wakuu naomba kutanguliza shukrani kwa wote watakao changia uzi huu na kutoa msaada. Nina changamoto ya kukohoa wakati wa usiku ninapoanza kulala tatizo hili lilianza mwaka jana kama mwezi wa 11 hivi lakini lilikuwa linanitokea kwa baadhi ya siku ila kwa sasa linatokea kila siku. Tatizo hili huanza hunitokea pale tu ninapotaka kulala lakini nikifanikiwa kupata usingizi huwa sikohoi tena mpaka kesho yake.

Kikohozi hiki kuwa kinaambatana na makohozi machache ambayo nikiyatema ndo huwa napata nafuu. Mwanzo nilidhani ni nyumba nayoishi kuwa na vumbi lakini nmejitahidi sana kuisafisha ila hali bado inaendelea. Pia kwa mchana kuna muda kila nikicheka huwa kama napaliwa na kupata kikohozi naomba msaada wa ushauri wenu wakuu.
Minyoo
 
Je, unapolala unapata kuhisi Hali ya uchungu mdomoni? Unatumia mto wakati wakulala? Je unatumia zulia?
 
Unaweza kuwa allergy,, mf mafuta ya kula au vyakula vya Ina fulami
 
Back
Top Bottom