Jamani kuna dogo mvulana yuko form one ana miaka 15, ni mdogo wangu, ana shida ya kukojoa kitandani, tumejaribu sana hospitali lakini ni mzima kabisa, ila ndo hivyo dogo kwa wiki mara 2 au mara tatu anakojoa.
Naombeni mnishauri au mniambie dawa yake ni nini.
Mkuu...kukojowa kitandani hakuna dawa....ila unatakiwa ucheze na akili ya dogo...jaribu kumuuliza....iweje hadi anakojowa?lazima kuna sababu inayomfanya anakojowa...mm nimeacha kukojowa nipo form two...tena naota nacheza mpira..au nipo sehemu halafu natafuta kichaka nakojowa....nikimaliza nashtuka...baba alihangaika sana mwisho...akapata jamaa akamwambiya dawa hii...na ilisaidia hadi leo sikojowi tena.
USINYWE MAJI AU CHOCHOTE CHA KIMIMINIKA kama soda..juice..maji..ikifika jioni...na kuendelea....pia kabla ya kulala hakikisha amekojowa..na pia kila baada ya masaa 4 muamshe akojowe...akizoea hivyo..atapunguza...au hatojojowa tena...jihadhari na dawa za mitishamba.
.yupo jamaa yngu mmoja Alipata AIBU ya mwaka . .TENA UKWENI..jamaa nae alikuwa anakojowa kitandani..ni mtu na shughuli zake...alikuwa kamana 32 hivi kipindi hicho..alikuja kwangu....nikampa ushauri kama huu wa kutokunywa maji mengi jioni..akaniona sifai..akapata mganga akampa miti shamba imsaidie kuzuia kukojowa mitandani....kuna sehem alitoa posa.. Wakwe wakafiwa ikabidi aende japo kwa hofu kubwa ya kukojowa kitandani lakini ilibidi aende...kwa kuamini dawa za mganga...unajuwa mkuu kila mtu anapokojowa kitandani anakuwa na style yake..
Sasa huyu jamaa alikuwa anaota kama watu wamemteka vile halafu wanamlazimisha akojowe kwa nguvu...jamaa wanakuwa na mapanga na visu wamemuwekea shingoni.. Huku wakimlazimisha akojowe.. Basi jamaa akishakojowa tu...anashtuka..ndy mganga akampa dawa akamwambiya akilala aiweke chini ya mto..ataona kitakachotokea.........basi yule jamaa yng akaenda zake msibani..huko ukweni KIPARANG'ANDA..basi siku hiyo....... alikuwa mbishi sana kulala kwa kuhofia kukojowa ukweni.
.mara avute sigara mara katia story ma mashemeji..jamaa halali. Mwishowe akajikuta peke yake hajalala saa nane za usiku...ndy akaona afadhali apumzike kwa kuamini ile dawa ya mganga aliyopewa...akaiweka chini ya mto jamaa akapitiwa na usingizi...basi jamaa akaota wale watekaji wamemfata tena... kama kawaida yao...wakaanza kumtishia....KOJOWA...leo tunakuuwa kojowa..duu..jamaa akaikumbuka ile dawa aliyopewa na mganga chini ya mto....ndy kupeleka mkono..akashangaa ile HIZIRI aloyopewa imegeuka MASHINE GUN.
tena AK 47. .. '''wale watekaji kuona jamaa ana mashine GUN AK 47 ... wakaona wamekwisha....wakaanza kukimbia hovyo huku wakipiga mayowe ya kuomba msaada...na jamaa yangu nae akasema sikubali..akaanza kuwafukuza.wengine walikimbilia porini lakini...mmoja akaingia kwenye choo cha jirani akajificha..jamaa akasema leo mm sikuachi...akamfata chooni.... yule mtekaji akaingia ndani kabisa ya tundu la choo...cha shimo.
Basi yule jamaa yangu ..... kila akifanya jitihada amtoe..yule mtekaji..jamaa kagoma kutoka..ndy yule jamaa yangu KIKOJOZI akasema leo...NAKUNYEA KABISA...mshenzi wewe..umenisumbuwa sana SIKUACHI bure..akamnyea mavi karibu YOTE...basi jamaa akajiendea zake....asubuhi anaamka amejikuta kwnza amelala peke yeke pale msibani wengine wote washaamka..ni yeye tu ndy aliyokuwa hajaamka...kujikaguwa..duu ...EBWANA KAJINYEA mavi kama YOTE...duu jamaa akaona hii sasa ni kali ya mwaka...ikabidi akusanye MKEKA na yeye pamoja akajifunga kama shuka akakimbilia PORINI...na msibani hakurudi tena maana minong'ono ilikuwa imeshaanza..SASA MKUU...mambo ya kufata dawa ya mitishamba ACHANA NAYO.. nakuomba fata ushauri wngu...umnusuru kijana