Tatizo la Kukojoa Kitandani kwa Watoto - Ushauri, Tiba na Namna ya Kukabiliana Nalo

Tatizo la Kukojoa Kitandani kwa Watoto - Ushauri, Tiba na Namna ya Kukabiliana Nalo

Mawazo yenu yote nunayapokea na nimeshaanza kuyafanyia kazi. Hv nimetoka kuongea naye. Nimejaribu kumuhoji nn kinatokea hadi anajikuta ameshakojoa anasema hakuna kitu anajikuta tayar. Nimemuuliza hujawahi kuota ndoto kama upo chooni then ukakojoa anasema wala haoti. Nikaamuuliza nilini ulishawahi kustuka kwenyewe usiku ukaamka halafu ukalala tena? Anasema hata siku moja, yaani akiangusha kama ni saa nje ni hadi aamshwe kujiandaa kwenda shule. Hapa ndo na prove kwamba usingizi mzito yaweza ikawa ni sababu kubwa. Suala la kuweka alarms nataka nilianze immediately usiku wa leo then nitatoa mrejesho
[emoji120][emoji120][emoji120]
Fanya Mkuu then leta mrejesho. Nina mdogo wangu wa Kiume yupo Kidato Cha NNE Lakini bado Anakojoa Kitandani.. Ukifanikiwa hili nipe mrejesho.
Wanywesheni maji ya mchele, yale maji yaliyo oshea mchele kwa mara ya kwanza. Sijui hii kitu inafanyaje kazi ila kuna mtu nime mshuhudia akipona wala siyo kuhadithiwa. Ingawa alichukua muda, zaidi ya miezi miwili. Hayo maji asinywe zaidi ya saa 1 ili kabla hajalala awe amekojoa. Mawazo mengine ya wadau yachukueni pia.
 
Hili jambo naweza kulitafsiri kama ndoto za utotoni yani ubongo unakuwa haujakomaa au ugonjwa,kikawaida mtu ukiwa katika makuzi ya miaka 3 na kuendelea hadi miaka 4 au mitano hadi sita, hapa mtu kukojoa anaweza ila huwa inatokea mara moja moja.

Mimi binafsi iliwahi nitokea mara kadhaa, nikiwa darasa la kwanza hadi la pili, siku zote sikojoi ila kuna siku nakojoa hadi naona aibu, ila ilikuwa inatokea katika ndoto, yani nacheza mpira kama kawaida yangu na marafiki, tena sehemu tuliyoizoea kuchezea siku zote,nawaaga marafiki kabisa nikisema "nisubirini nikojoe kwanza " wanasimamisha mpira, hii tulikuwa tukiifanya ili kuepusha kusababisha kufungwa kutokana na upungufu wa mtu mmoja.Basi bwana weeeee, kumbe ile kukojoa nakuwa nipo kitandani.

Hiyo hali ilikuja kubadilika ikawa nikianza tu ile kukojoa nashituka.

Sasa hili nalo niwaambie, kukojoa inawezekana kwa mtu mwenye usingizi mzito, yani usingizi wa pono,yani mtu akilala munaweza mbeba mkamuweka nje yeye hajitambui. Hii hali inatokea kwa mtu yeyote ambaye anaweza kuwa na dalili za upono, usingizi mzito, kwa mfano anywe pombe akalale amelewa, lazima akojoe huyo hata kama hakojoagi siku zote,utasikia watu wanamsema"akilewa anajikojoleaga huyo"

La pili hata wewe msomaji jaribu kunywa maji mengi usiku harafu ukalale, usingizi ukupitie kisha ushitushwe na mkojo kubana, sasa jikaze ukijaribu kuvumilia harafu utafute usingizi kwa nguvu tena, oohoo ile hali ya ndoto itakuijia upo chooni unakojoa harafu mwili unaruhusu mkojo kutoka, utashangaa umelowa na hali una miaka ishirini hukojoi kitandani. Sasa kwa hawa ndugu kukojoa kwa miaka hiyo ni tatizo ikizidi miaka 12+ tunaanza kuita ugonjwa. Ila unatibika
 
Halafu nakushauri usi panic na kujikuta unafuata ushauri mwingine wa kumuumiza mwanao. Usimkaripie, kumpiga au kumtisha. Pia jiepushe na madawa ya kienyeji. Nimewahi kushuhudia visa vya aina hii. Ni kuwa kama ulivyosema watoto wa namna hii wanakuwa na usingizi mzito sana. Kuna kipindi akikua hali itabadika. Vikojozi wako wengi sana wengine mpaka miaka 14 bado wanalowesha vitanda. Lakini wanakuja kuaacha. Labda kuwe na kitu serious tu. Hata wakati wa kumwamsha usiku utakuja ona kuwa ana usingizi mzito sana.
Ni kweli, ila ushauri wa kumfungia nyoka kiunoni hahahaa huo siuwezi maana watt wetu wengine hawa hata hajawahi kumuona nyoka kwa ukaribu, anamsoma kwenye vitabu tuu sasa ndo aamke amkute tupo kiunoni na kwa bahati mbaya hana uhakika kama yu hai ana amekufa, hii inaweza kuwa tukio baya sana kueahi kukutana nalo katka umri wake. Hili siwezi kulifanya, hata siwezi kumkaripia maana nikizungumza naye namuona ni kwa kiasi gani hiyo hali inamnyima raha ikiwa wadogo zake hawana hili tatizo. Ahsante kwa angalizo mkuu.
 
Heshima kwako mkuu, naomba nikupe na mimi uzoefu wangu :

1. Katika hali ya kawaida mtoto akifika miezi 6 hadi 9 anapaswa kuacha kujikojolea

2. Kama atakuwa hawezi kudhibiti mkojo baada ya kufikisha mwaka mmoja basi huyo ana tatizo linalohitaji msaada wa kitaalam

3. Chukua hatua zifuatazo ili kumsaidia

• Ongea nae na mkubaliane asitumie kimiminika chochote baada ya jua kuzama,wakati wa chakula cha jioni anaweza kunywa maji si zaidi ya nusu glass

• Kabla ya kulala hakikisha anaenda kukojoa na uweke utaratibu wa kumuamsha angalau mara mbili usiku ( hapa inabidi uweke Alarm either kwenye simu yako au unaweza kununua saa maalum za mezani zenye alarm) ukimzoesha kufanya hivyo baada ya muda ubongo wake utazoea kuamka hata kabla ya alarm, njia hii ina ufanisi mkubwa sana!

• Kwa Umri wake fahamu tatizo lake linamuumiza sana kisaikolojia, nyie wazazi muonyesheni upendo na kujali na msitangaze tatizo lake kwa watu wala kumuadhibu akijikojolea, anahitaji msaada na nyie ndio mnapaswa kumsaidia

• anzisha utaratibu wa kumpongeza siku asipojikojolea, hii itaongeza self esteem yake na kumtia moyo kwamba mnafuatilia na mpo kwa ajili ya kumsaidia

Ukiweza kufanya haya kwa miezi miwili hadi mitatu tatizo litaisha nina ushahidi wa hili. Kila la heri usisahau kuleta mrejesho!
100% accepted.
 
Mkuu pole sana ,kwanza nikupongeze kwa kulivalia njuga swala la binti yako umeliwahi ,ukiliacha likaenda ukubwani laweza mletea fedheha kubwa kwenye mahusiano na ndoa yake swala hili linatatulika kwa njia mbili
1. Kidaktari
Kaka nenda hospitali kubwa kutana na daktari bingwa wa masuala ya kibofu ,sisemi dawa za kienyeji hazisaidii ila mara
nyingi ni kubahatisha kuua kindege juu ya screen ya tv waweza ua kindege ukapasua tv ,sababu za hali hiyo ni nyingi
-aweza kuwa ana kisukali cha kuzaliwa (usiogope 80% hutibika)
-Matumizi ya kupitiliza ya carboneted drinks (soda,sparkling waters etc)
-etc
UGONJWA HUU UNATIBIKA KABISA .
2.Kiroho
Huu ni moja ya ugonjwa pendwa na walozi au roho chafu kama wewe ni mkristo usimpeleke kwa wauza mafuta ya upako
au sijui maji ya uzima ,peleka kwenye makanisa yasiyo binafsi kama mlokole peleka TAG kwenye maombi usisahau kutoa
na sadaka kumsihi mungu akuhurumie ,kama wewe ni muislamu usiende kwa hawa wanaojitangaza mara wanamajini,mara nyota huo sio uislamu nenda msikiti unaosali kaongee na imamu atakupa dua stahiki ziombe huku ukifunga ,wa dini za asili usisafiri mbali nenda kaone wazee kijijini kwenu
NB ;
-Wasio wakristo au waislamu wafuate viongozi wao husika sio hawa matapeli wa mitandaoni

Karibu
Mkuu wewe ni binadamu haswa
 
Mku bint wangu kakojoa kitandani mpaka ana miaka 13, bda ya hapo kaacha mwenyewe cjamtaftia dawa ya aina yoyote hyo ilikua ushauri wa madokta hivi Sasa ana miaka 16 keshasahau kama alikua anakojoa kitandani, Sasa ww akili kichwani kwako
 
Fanya hivi nenda msitu wowote ,tafuta vijana wakusaidie kutafuta nyoka aina yoyote ndefu saizi ya mkanda wa mwanaume ipigeni mpaka ife, hapa nivizuri mkatumia fimbo kuepusha kuitoboa toboa.

Ukimaliza chukua ondoka nayo subiri hadi usiku muda wa kulala. Huyo dogo akisha lala kama masaa mawili usingizi umemkolea chukua ile nyoka mfunge kiunoni halafu wewe nenda kalale.

Yeye muda ukifika kama kawaida yake atakojoa baada ya muda atashituka ili kutafuta sehemu nzuri tofauti na ile aliyokwisha kojolea hapo lazima ata notice kuwa anakitu kiunoni atatafuta jinsi ta kukitoa pengine atawasha taa kabisa.
Akigundua ni nyoka iko katika kiuno chake atapata mshituko kwenye akili yake ambao hatoweza tena kojoa kitandani muda utakuwa ukifika anashituka mwenyewe anaenda kukojoa.

Lakini pia unaweza kwenda hospital wakamfanyia uchunguzi kama mirija yake haija pwaya maana hiyo njia hapo juu inafanya kazi kwa mtu ambaye physically hana tatizo lolote kiafya japo ni uvivu wa ndoto na kujisahau tu.
Tiba mbovu hii.

Kama mtoto anakawaida ya kushtuka saa nane baada ya hako kanyoka je akiwa anakoja sa saba si atashtuka kila siku baada ya mkojo?
 
Hiyo issue simple sana,

Cha kwanza ikifika saa mbili asinywe maji. Kwa siku ukimuuliza anakwenda uwani mara ngapi? Aiwezi kuzidi mara tatu. Sasa hapo lazima usiku akojoe tu.

Kwa hiyo anatakiwa aende uwani kukojoa zaidi ya mara 6 hata kama

Hata kama ajabanwa na mkojo, kama ataweza zaidi ya mara sita sawa ila isipungue hapo.

Kama mchana atakuwa amekojoa mara zote hivyo,possibility ya kukojoa usiku ni ndogo sana na badala ya kufanya hivyo usiku lazima atAshituka .

Afanye hivyo kwa muda wa mwezi mmoja tu , atazoe akibanwa na mkojo tu lazima atashtuka atakama iwe mchana.

Akili tunakuwa tumeshAibadilisha taratibu. Hapo kinachotokea akibanwa na mkojo akili aimuamshi kama sisi wengine ukihisi tu mkojo lazima ushtuke unaenda uwahi.

Yeye akili yake au ubongo wake aufanyi hivyo.

Ukiweza kuibadilisha akili yake au ubongo wake anaweza tu kunywa maji muda wowote tu maana akili tumesha ibadilisha inakuwa imesha zoea,ikibanwa tu na mkojo lazima ashtuke.
Kwa maana afanye zoezi l kunywa maji mengi mchana ili akojoe sana mchana?

ili kukojoa kule kuwe kunamjenga kisaikolojia imsaodie kuamka usiku akipakabwa na mkojo ama SIJAELEWA MKUU ?
 
I write from experience

1)Apunguze kunywa maji sana, anapoona ni muda wa kulala akakojoe mala ya mwisho then ndio alale.

2)Ajiamshe mwenyewe usingizini, kukojo kunasababishwa na ndoto mtu anaota yupo kama na wenzie anaaga anaenda chooni anakojo kumbe nahuku anakojoa kweli ila ukiwa kwenye stage hii unakuwa Kama na usingizi nusu kwenye njozi unaona mkojo mbona unakojoa kiugumu kumbe huku kwenye uharisia mkojo unazuiliwa na godoro...ukiwa kwenye hali hiyo jenga mazoea yakujiuliza hapa naota au kweli utakuta unashtuka ukiendelea hivi unaacha.

Ukirudiarudia izo process tabia ya kukojoa inaondoka.
Mkuu na wale ambao wana tatizo la kukojoa kwa muda, yani inawezakupita hata miezi sita mtu siku mpja naumwaga hasaa inasaidiwaje?
 
Ni kawaida tu bhana, mimi nilikojoa kitandani hadi nafika darasa la saba

kwenye makambi kule shuleni nilikua nakojoa kila siku, ila sikuwahi kugundulika

NB: kukojoa hua ni inshu ya kisaikolojia na hua inatibika kisaikolojia.
Inatibikaje kisikolojia mkuu?
 
Dawa nikuamka na kwenda kukojoa chooni.

Kama huwezi kuamka egesha alarm/kengele kwenye simu yako kila baada ya masaa mawili ikuamshe uende kukojoa chooni.
 
kwa maana afanye zoezi l kunywa maji mengi mchana ili akojoe sana mchana..?

ili kukojoa kule kuwe kunamjenga kisaikolojia imsaodie kuamka usiku akipakabwa na mkojo ama SIJAELEWA MKUU ?

Mkuu kukojoa mara nyingi mchana kuna mpunguzia kukojoa usiku na Usiku akibanwa na mkojo lazima ashtuke tu kama sisi wengine .
 
Ampeleke hospitali akapime labda ana tatizo kwenye kibofu. Kama hana tatizo maeneo hayo basi conditioning inatosha kumponya mwanae.

Cc Unforgetable
Elezea kidogo hyo conditioning inakuwaje maana kuna kipindi ndugu yangu alikuwa mhanga nayeye. Alikuwa anakaa hata mwaka au miezi sita kisha anakojoa. Kipa mwaka lazima akojoee japo mara mbili au tatu.
 
Back
Top Bottom