Tatizo la Kukojoa Kitandani kwa Watoto - Ushauri, Tiba na Namna ya Kukabiliana Nalo

Fanya Mkuu then leta mrejesho. Nina mdogo wangu wa Kiume yupo Kidato Cha NNE Lakini bado Anakojoa Kitandani.. Ukifanikiwa hili nipe mrejesho.
Wanywesheni maji ya mchele, yale maji yaliyo oshea mchele kwa mara ya kwanza. Sijui hii kitu inafanyaje kazi ila kuna mtu nime mshuhudia akipona wala siyo kuhadithiwa. Ingawa alichukua muda, zaidi ya miezi miwili. Hayo maji asinywe zaidi ya saa 1 ili kabla hajalala awe amekojoa. Mawazo mengine ya wadau yachukueni pia.
 
Hili jambo naweza kulitafsiri kama ndoto za utotoni yani ubongo unakuwa haujakomaa au ugonjwa,kikawaida mtu ukiwa katika makuzi ya miaka 3 na kuendelea hadi miaka 4 au mitano hadi sita, hapa mtu kukojoa anaweza ila huwa inatokea mara moja moja.

Mimi binafsi iliwahi nitokea mara kadhaa, nikiwa darasa la kwanza hadi la pili, siku zote sikojoi ila kuna siku nakojoa hadi naona aibu, ila ilikuwa inatokea katika ndoto, yani nacheza mpira kama kawaida yangu na marafiki, tena sehemu tuliyoizoea kuchezea siku zote,nawaaga marafiki kabisa nikisema "nisubirini nikojoe kwanza " wanasimamisha mpira, hii tulikuwa tukiifanya ili kuepusha kusababisha kufungwa kutokana na upungufu wa mtu mmoja.Basi bwana weeeee, kumbe ile kukojoa nakuwa nipo kitandani.

Hiyo hali ilikuja kubadilika ikawa nikianza tu ile kukojoa nashituka.

Sasa hili nalo niwaambie, kukojoa inawezekana kwa mtu mwenye usingizi mzito, yani usingizi wa pono,yani mtu akilala munaweza mbeba mkamuweka nje yeye hajitambui. Hii hali inatokea kwa mtu yeyote ambaye anaweza kuwa na dalili za upono, usingizi mzito, kwa mfano anywe pombe akalale amelewa, lazima akojoe huyo hata kama hakojoagi siku zote,utasikia watu wanamsema"akilewa anajikojoleaga huyo"

La pili hata wewe msomaji jaribu kunywa maji mengi usiku harafu ukalale, usingizi ukupitie kisha ushitushwe na mkojo kubana, sasa jikaze ukijaribu kuvumilia harafu utafute usingizi kwa nguvu tena, oohoo ile hali ya ndoto itakuijia upo chooni unakojoa harafu mwili unaruhusu mkojo kutoka, utashangaa umelowa na hali una miaka ishirini hukojoi kitandani. Sasa kwa hawa ndugu kukojoa kwa miaka hiyo ni tatizo ikizidi miaka 12+ tunaanza kuita ugonjwa. Ila unatibika
 
Ni kweli, ila ushauri wa kumfungia nyoka kiunoni hahahaa huo siuwezi maana watt wetu wengine hawa hata hajawahi kumuona nyoka kwa ukaribu, anamsoma kwenye vitabu tuu sasa ndo aamke amkute tupo kiunoni na kwa bahati mbaya hana uhakika kama yu hai ana amekufa, hii inaweza kuwa tukio baya sana kueahi kukutana nalo katka umri wake. Hili siwezi kulifanya, hata siwezi kumkaripia maana nikizungumza naye namuona ni kwa kiasi gani hiyo hali inamnyima raha ikiwa wadogo zake hawana hili tatizo. Ahsante kwa angalizo mkuu.
 
100% accepted.
 
Mkuu wewe ni binadamu haswa
 
Mku bint wangu kakojoa kitandani mpaka ana miaka 13, bda ya hapo kaacha mwenyewe cjamtaftia dawa ya aina yoyote hyo ilikua ushauri wa madokta hivi Sasa ana miaka 16 keshasahau kama alikua anakojoa kitandani, Sasa ww akili kichwani kwako
 
Tiba mbovu hii.

Kama mtoto anakawaida ya kushtuka saa nane baada ya hako kanyoka je akiwa anakoja sa saba si atashtuka kila siku baada ya mkojo?
 
Kwa maana afanye zoezi l kunywa maji mengi mchana ili akojoe sana mchana?

ili kukojoa kule kuwe kunamjenga kisaikolojia imsaodie kuamka usiku akipakabwa na mkojo ama SIJAELEWA MKUU ?
 
Mkuu na wale ambao wana tatizo la kukojoa kwa muda, yani inawezakupita hata miezi sita mtu siku mpja naumwaga hasaa inasaidiwaje?
 
Ni kawaida tu bhana, mimi nilikojoa kitandani hadi nafika darasa la saba

kwenye makambi kule shuleni nilikua nakojoa kila siku, ila sikuwahi kugundulika

NB: kukojoa hua ni inshu ya kisaikolojia na hua inatibika kisaikolojia.
Inatibikaje kisikolojia mkuu?
 
Dawa nikuamka na kwenda kukojoa chooni.

Kama huwezi kuamka egesha alarm/kengele kwenye simu yako kila baada ya masaa mawili ikuamshe uende kukojoa chooni.
 
kwa maana afanye zoezi l kunywa maji mengi mchana ili akojoe sana mchana..?

ili kukojoa kule kuwe kunamjenga kisaikolojia imsaodie kuamka usiku akipakabwa na mkojo ama SIJAELEWA MKUU ?

Mkuu kukojoa mara nyingi mchana kuna mpunguzia kukojoa usiku na Usiku akibanwa na mkojo lazima ashtuke tu kama sisi wengine .
 
Mitishamba pia inasaidia hili tatizo ukitaka maelezo zaidi njoo PM
 
Ampeleke hospitali akapime labda ana tatizo kwenye kibofu. Kama hana tatizo maeneo hayo basi conditioning inatosha kumponya mwanae.

Cc Unforgetable
Elezea kidogo hyo conditioning inakuwaje maana kuna kipindi ndugu yangu alikuwa mhanga nayeye. Alikuwa anakaa hata mwaka au miezi sita kisha anakojoa. Kipa mwaka lazima akojoee japo mara mbili au tatu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…