arabianfalcon
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 2,285
- 584
Pole shosti, usikate tamaa hakuna lisilo wezekana chini ya jua muone doctor na utafanikiwa kuna watu watatizo kubwa kuliko lako na wamepona,vuta subra utapona.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Habarini za jioni, kwa mara ya kwanza najitokeza hapa kuomba ushauri.
Nina miaka 31, nina mtoto mmoja na sijaolewa. Kitu kinachoninyima raha ni kukojoa kitandani, cna mtu wa kumwambia maana ni aibu kubwa sana. Japo nina kazi ya kuniwezesha kuishi mjini, sometimes naona sina thamani yoyote. Kuna movie moja ya kibongo inaitwa mrembo kikijozi, sijawahi iangalia maana inaniumiza mara elfu moja zaidi sababu kama haijakupata hutaelewa inaumiza kiasi gani. Mwanangua aliacha kukojoa kitandani tangu ana miaka minne basi huwa namtamani. Hivi naweza tibiwa wapi, nimechoka huu mzigo
Mkuu,kwa niba ya mtoa mada nakushukuru sana tena sana.Bichwamaji,
Kuna mdogo wangu alikuwa ana tabia kama yako mpaka akawa hata chuoni halali bali analala nyumbani. Tulimfanyia dawa zifuatazo zikamsaidia:-
a. Kwanza tulimshauri asiwe anakunywa maji kwa wingi usiku.
b. Alishauriwa awe anajaribu kupima diebatic thank god alikuwa hana ila nakushauri na wewe nenda kamuone daktari upime kwani kwenda chooni kila mara ni dalili za kisukari.
c. Jaribu kumtafuta bwana moja zanzibar anaitwa bwana madawa yuko zanzibar market anauza dawa za mitishamba kuna dawa moja nzuri sana itakusaidia kuacha kukojoa. Yuko zanzibar market sehemu moja nyuma ya zanzibar market vimtaa vya ndani kwa ndani sikumbuki jina lake vizuri nikilikumbuka nitakuja kukuambia. (This should be a last resort).
d. Vile vile inaweza kuwa woga na wasiwasi na kwahiyo unavyoenda kulala unakuwa mishipa na mwili unakuwa umerelax. Jaribu kuwa unalala kama alivyosema mchangiaji moja kuwa uwe unajiamsha kila mara inasaidia.
e. Kuna tiba nyengine waislamu tunayo hasa kutoka wanazuoni wetu kuwa ndoto unazoziota unaweza kutambua kuwa kama wakati huu unataka kwenda chooni mfano katika ndoto ukiona unataka kwenda kujisaidia basi amka haraka sana uende chooni. Vile vile ndoto kama vile unataka kwenda kuogolea na mkojo umekubana amka haraka uende kukojoa. Pia ndoto za kukimbizwa na kitu jitahidi uamke kwani mkojo unakuwa umebana hapo.
Hivyo ndoto za kujiona umebanwa na mkojo na kujisaidia hata kama unaona ni kweli hiyo ndoto jiamshe nenda chooni. Ndoto za kuogelea au kufanya mapenzi na mwenza pia zinaweza kuwa ni dalili ya kukaribia mkojo jiamshe. Ndoto za kukimbizwa zinakufanya utokwe na jasho na dehydration na kupelekea kutaka kukojoa amka haraka uende chooni.
I hope zitakusaidia.
Mkuu,kwa niba ya mtoa mada nakushukuru sana tena sana.
wabillah tawfiq
You ARE a complete woman dear, toa kabisa mafikiri ya kua less than any other woman. Hujui wengine wana matatizo gani na wenyewe.Asante, will try. Nilihitaji watu wa kuniondolea fear hii ili niweze hata kumweleza dokta. Maana ni aibu jamani. Uwe na gari, nyumba, hela kuna wakati unatamani kuwa hata mwanamke anayepika kambi ya fisi lakini uwe a complete woman
Mkuu, wa niba ya mtoa mada nakushukuru sana tena sana.
wabillah tawfiq
Mdondoaji. Bichwamaji (na wengine wataohitaji msaada wa dawa za miti shamba)
Jina la duka la dawa za Mitishamba Zanzibar ni kwa "Saleh Madawa"
Bichwamaji
Kukojoa kitandani wakati mwengine kunasababishwa na tatizo la kisaikolojia na si lazima iwe abuse utotoni na mara nyingi wewe mwenyewe unaweza usijue tatizo hasa ni nini bila ya kumuona mtaalamu.
Nenda kwa mtaalamu usijiskie vibaya kwani hili ni tatizo Kama tatizo jengine lolote tu na watu wenye tatizo Hilo ni wengi tu mbona.
Btw niliona wakitangazia dawa za kuzuwia kukojoa sana kwa wanawake waliowahi kujifungua. Kama tatizo limeongezeka baada ya kupata mtoto unaweza kuanzia kwa daktari Wa akina mama na watoto kwanza
kuna mtu humu anaitwa Mzizi mkavu
hebu m pm umueleze ana jua dawa za tiba mbadala....