Pole sana mpendwa kwa mateso haya, elewa tu wewe si wa kwanza, kwa tatizo hili. tatizo hili solution yake ipo sana usihofu! yaweza kuwa dawa, ushauri (kama wa wachangiaji waliotangulia hapo juu endapo ukiufanyia kazi), lishe na imani.
Je, tatizo hili linakupata usiku tu, au hata mchana unapolala usingizi unakojoa pia? kama hujawahi kukojoa kitandani mchana ila usiku tu, basi tatizolako nilakiroho zaidi. yaani sawa mtu yule mwenye tatizo la kufanyishwa mapenzi usingizini anapoamka akajikuta ameloa uchafu ukeni na hata matandiko kuchafuka. Kwa shuhuda za waliowengi jambo hili huwatokea usiku usingizini na hushuhudia picha yote katika ndoto wakifanya tendo la ngono na mtu fulani mweupe! hii ni roho kamili na tiba yake niya kiroho pia, si ya hospitali.
Kama hata mchana unakojoa ili mradi tu usingizi umekolea basi muhimu umuone daktari kwa ushauri maana bila shaka pana shida ya mawasiliano baina ya ubongo husika na sfinkta za kibofu cha mkojo uwapo usingizini, kama si tatizo la kurithi. Nashauri fanya yafuatayo;
1. Tumia Vitamin B-12 kwa wingi, kisha angalia mabadiriko (zingatia maelekezo ya matumizi yake. waweza kurudia dozi mara kwa mara.
2. Tumia Green Tea ya mlonge kiwe kinywaji chako kutwa (asubuhi, mchana na jioni - mwisho saa 11 jioni) kwa mwezi kisha angalia mabadiriko
3. Punguza sana kufanya mapenzi na fanya zoezi la kubana mkojo kama ulivyoshauriwa na mchangiaji, kisha lala mapema.
4. Kwa tatizo la kiroho, tiba ni maombi katika Kanisa lolote la Walokole mahali ambapo matendo ya ishara na miujiza vinafanyika. Utaenda siku hiyo na utapona dakika hiyo ya maombi, shuhuda zipo ila uamini kwamba Yesu anaweza kukuponya.