Tatizo la Kukojoa Kitandani kwa Watoto - Ushauri, Tiba na Namna ya Kukabiliana Nalo

Tatizo la Kukojoa Kitandani kwa Watoto - Ushauri, Tiba na Namna ya Kukabiliana Nalo

Pole sana mkuu,kwakuwa unakabaliwa na tatizo fuata ushauri mzuri pia achana na wale watakao kukejeri.

Wewe muulize mtu kabila la mpogolo na mila zao za kumuashisha kikojozi kukojoa kitandani. wao uamini kuwa, kama mtu nakojoa kitandani, basi muamushe asubuhi, mvalishe mishanga na kimsuli cha haibu halafu mpitishe mitaani ukimuimba, kikojooozi na nguo kaitia moto! Kindumbwe ndumbwe chaliaaa! mchafu kunuka kagogeeee! basi ukimaliza hilo hata kojoa tena kitandani!!!!!! wakazi wa ilala kota mwaka 1971, kweli mimi nadanganya?

Kabila langu wanaamini mtu akibalehe tu na huo utani wa jadi na kitanda unakoma mara moja!
 
Whilst bedwetting is a very common problem, people are reluctant to discuss what is perceived to be an embarrassing subject.

A number of children will outgrow bedwetting but for others this condition might persist into adulthood. Unfortunately this condition may interfere with social activities, relationships and performance at school. In addition their self-esteem may also suffer. Bedwetting may be caused by several factors and it is encouraging to know that this condition can be managed in several ways. Dont give up and dont delay take the bedwetting challenge today to enable you to start a conversation with your doctor

Mtoto mzuri wa kizungu ana miaka 19 anakojowa kitandani pole sana .
Bed Wetting, bedwetting
 
Last edited by a moderator:
Dawa ya Kumtibu Mtoto kukojowa Kitandani Vifaa vyake upate hivi: Upate Kwato La N'gombe tiya ndani yake Kaa La Moto kisha yule mgonjwa wa kukojowa Kitandani alinuse lile kwato la N'gombe lilio na Kaa la Moto ndani yake,kisha Avue nguo zake awe uchi Apande juu ya mti kisha juu ya huo mti akojoe mkojo ushuke chini afanye hiyo Dawa kwa Muda wa siku 7 atapona kabisa. Hakuna dawa Mahospitalini ya kutibu mtoto kukojowa kitandani
 
Kukojoa kitandani ni dalili ya matatizo makubwa ya kudhalilishwa mhusika hususani alipokuwa bado kinda.
 
Naomba kusema pole sana na tatizo la mwenzio

DAWA

Usimzuie mwenzio kunywa maji usiku kwani maji ni dawa kisa kumwaga maji usiku cha kufanya mnapoenda kulala hakikisha anatumia asali vijiko vitatu hadi vitano vya asali mbichi kila siku mnapoenda kulala hatapata tatizo hilo tena inshallah. Naomba nunua asali mbichi na sio ile iliyochujwa kwa kutumia moto/joto na iwe ni halisi isiwe yenye maji
Asali yenye maji tumia njiti ya kiberiti tumbukiza ndani ya asali kisha washa ikiwaka haina maji ikishindwa jua ina maj.

Asali yenye kuchujwa kwa moto/kuchemshwa inuse ina harufu ya moshi na kama haina harufu ni nzuri
Asali ya kuchakachua tumia karatasi sugua katika karatasi na itaonesha maji au karatasi kulowana basi jua asali imechakachuliwa na haifai kwa tiba hiyo.

Au ukindondosha inatengeneza kitu kama mpira au inajizungusha kama gurudumu na haisambai katika vumbi jua ni asali nzuri na ikisambaa katika vumbi jua ni mbaya na imechakachuliwa

"NADHANI NIMEKULEZA JINSI YA KUPATA ASALI BORA NA ASALI MBICHI NA ISIYOCHAKACHULIWA NA WAFANYABIASHARA. WATU WATUMIE ASALI KWA AFYA ZAO BADALA YA KUTUMIA SUKARI YENYE KULETA KISUKARI KWA KASI AJABU!"
 
Whilst bedwetting is a very common problem, people are reluctant to discuss what is perceived to be an embarrassing subject.

A number of children will outgrow bedwetting but for others this condition might persist into adulthood. Unfortunately this condition may interfere with social activities, relationships and performance at school. In addition their self-esteem may also suffer. Bedwetting may be caused by several factors and it is encouraging to know that this condition can be managed in several ways. Dont give up and dont delay take the bedwetting challenge today to enable you to start a conversation with your doctor.

Request your free DVD Understanding Bedwetting and listen to other people share their experiences on bedwetting.





Mtoto mzuri wa kizungu ana miaka 19 anakojowa kitandani pole sana .
Bed Wetting, bedwetting


Dawa ya kukojoa kitandani ni KWATO YA NG'OMBE
IKOSHE VIZURI KISHA ICHEMSHE,KISHA UMPE SUPU YAKE MHUSIKA MILS 100 MARA 3 KUTWA BAADA YA SIKU 2-3 ATAKUWA KAPONA. NINA USHAHIDI NILIELEKEZWA NA NIKAMPATIA BINTI YANGU WA KAZI MIAKA 5 ILIYOPITA HADI SASA NI MZIMA
 
Last edited by a moderator:
nisaidieni dawa ya kukojoa kwani mwanangu wa miaka 13 bado anakojoa hadi leo ameshindwa kwenda boading school
 
Dawa ya Mtoto kukojowa Kitandani Fanya hivi Mkuu@[/COLOR]J mubago

Pata Kwato la N'gombe tiya ndani yake kaa la Moto kisha huyo Mtoto wako alinuse hilo kwato lililo na Moto kisha Avue nguo awe uchi apande juu ya Mti kisha huko juu ya Mti akojee Mkojo na akisha maliza kukojowa ashuke avae nguo zake Afanye hiyo Dawa kwa muda wa siku 7 atapona inshallah kwa uwezo wake Mwenyeezi Mungu . Fanya hivyo Mkuu J mubagokisha utanijibu baada ya Siku 7 Hakuna Dawa ya Kutibu mtoto anaye kojowa Kitandani Mahospitalini. Usikose kunipa FeedBack.
 
Nini maana ya Enuresis?

L_April05_BedWetting.jpg


Enuresisi ni neno la kitaalamu linalomaanisha hali ya kutoa mkojo bila ridhaa ya muhusika(involuntary),aina mojawapo tuliyoizoea ni ukojozi kitandani wakati mtu akiwa amelala hasa wakati wa usiku.

Ukojozi kitandani huwapata zaidi watoto na mara nyingi ni hali ya kawaida tu katika ukuaji wao. Ukojozi kitandani hutokea zaidi kwa watoto wa kiume kuliko wa kike.

Vitu gani husababisha ukojozi kitandani?

Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha ukojozi kitandani. Baadhi ya njia hizo ni hizi zifuatazo:


Kurithi (Katika familia)
Kushindwa kuamka kutoka usingizini
Msongo wa mawazo
Ukuaji wa taratibu wa mishipa za fahamu kutofanya kazi inavyotakiwa ( hali ambayo humpunguzia mtoto uwezo wa kuzuia kibofu kutoa mkojo)
Matatizo ya homoni (kuzalishwa katika kiwango kidogo kwa homoni zinazopunguza kuzalishwa kwa mkojo wakati wa usiku)
Maambukizi katika njia ya mkojo
Matatizo katika mrija wa mkojo kwa wavulana au kwenye njia ya mkojo kwa wavulana na wasichana.
Matatizo kwenye uti wa mgongo
Kibofu cha mkojo kuwa kidogo
Ukojozi kitandani sio tatizo la akili au tabia. Tatizo hili halitokei eti kwa sababu mtoto ni mvivu kiasi kwamba hawezi kuamka kitandani na kwenda msalani.

Je ni kipindi gani watoto wengi huweza kudhibiti hali ya mahitaji ya kukojoa?

Watoto huweza kudhibiti kibofu cha mkojo katika umri tofauti. Wakifikia umri wa miaka 6, watoto wengi huacha kukojoa kitandani. Ukojozi wa kitandani hadi katika umri wa miaka 6 siyo kitendo cha ajabu, ingawa inaweza kuwanyima amani wazazi na walezi wengi.Kama mtoto yuko chini ya umri wa miaka 6, tiba kwa tatizo la ukojozi kitandani kwa kawaida siyo mara nyingi watoto wengi huacha kukojoa bila aina yoyote ya matibabu.

Daktari anaweza kusaidia lolote?


Ingawa watoto wengi wanaokojoa kitandani hawana tatizo lolote la kiafya, daktari anaweza kusaidia kugundua kama tatizo la mtoto wako kukojoa kitandani linasababishwa na matatizo mbalimbali ya kiafya. Kwanza daktari atakuuliza iwapo mwanao hukojoa mchana na usiku. Halafu daktari atampima na anaweza kuchukua vipimo vya mkojo kuangalia kama kuna maambukizi au kisukari au matatizo mengine.

Daktari anaweza kutaka kujua mwenendo wa kimaisha wa mwanao anapokuwa nyumbani na hata shuleni.Ingawa unaweza kuogopa mtoto wako anapokojoa kitandani, tafiti zimeonyesha kuwa sio rahisi kwa watoto wanaokojoa kitandani kuwa na matatizo ya hisia tofauti na watoto wengine wasio kojoa kitandani.Daktari pia atakuuliza jinsi mnavyoishi katika familia kwa sababu m matibabu yanaweza kuhusisha mabadiliko kadhaa ya kimaisha hapo nyumbani.

Je kuna matibabu yoyote kwa tatizo la ukojozi kitandani?

Watoto wengi huacha kukojoa kitandani bila kupata matibabu yoyote.Ingawa wakati mwingine wewe na daktari wako anayemuona mtoto wako mnaweza kuamua kwamba mtoto anahitaji tiba fulani.Kuna aina 2 za tiba: kumbadili mtoto kitabia, na kumpatia dawa. Kumbadili mwanao kitabia husaidia kumfanya mwanao aache tabia ya kukojoa kitandani.Baadhi ya njia za kumbadili mwanao kitabia ni hizi zifuatazo:

Mzuie mwanao asinywe vinywaji/maji kwa wingi kabla ya kulala
Hakikisha mwanao anenda msalani kila mara kabla ya muda wa kulala na pia mara tu anapo anza kusinzia.
Tumia kengele itakayolia pindi kitanda kinapolowa ,hii humfundisha mtoto kufahamu pindi kibofu kinapojaa wakati wa usiku
Mpe zawadi mtoto anapoamka bila kukojoa kitandani
Mwambie mtoto wako kubadili matandiko mwenyewe kila anapokojoa kitandani
Mpe mwanao mazoezi ya kibofu: muelekeze mwanao akae muda mrefu bila kukojoa kipidi cha mchana, ili kibofu kiwe na uwezo wa kutunza mkojo mwingi zaidi

Ni dawa gani zinazotumika kutibu ukojozi kitandani?

Daktari wako anaweza kumpa mwanao dawa kama ana umri wa miaka zaidi ya saba(7) iwapo njia za kumbadilisha kitabia zilizotajwa hapo hazijasaidia. Hata hivyo dawa hazitibu ukojozi kitandani, Aina mojawapo ya dawa husaidia kibofu kutunza mkojo zaidi, na dawa nyingine husaidia figo kutengeneza kiwango kidogo cha mkojo. Dawa hizi zinaweza kuwa na madhara kiafya kwa mfano, mdomo kukauka na mashavu kuwa na rangi nyekundu.

UJUMBE WA KUPELEKA NYUMBANI:

Ukojozi kitandani unaweza kusababisha matatizo ya kitabia kwa sababu mtoto anaweza kuhisi ana makosa na kujisikia aibu. Ni kweli kwamba mwanao anatakiwa kuwajibika kwa kitendo hicho cha kukojoa kitandani (hii ina maana mwanao anatakiwa kufanya usafi). Lakini usimfanye mwanao ahisi kwamba yeye ndio mwenye makosa.Ni muhimu kwa mwanao kujua kwamba ukojozi kitandani siyo kosa lake. Kitendo cha kumuadhibu mwanao kwa kosa la kukojoa kitandani haitasaidia kutatua tatizo.

Itamsaidia mwanao kujua kwamba hakuna anayejua sababu kubwa inayopelekea ukojozi kitandani.Muelimishe kwamba mambo hayo hutokea katika familia (Kwa mfano, kama mwanao akikojoa kitandani, unatakiwa kujadiliana naye na kumhaidi kumsaidia kupambana na hali hiyo).

Msisitizie mwanao kwamba anatakiwa aende msalani wakati wa usiku. Muwekee taa kuelekea msalani ili imuwie rahisi kuona njia ya kuelekea msalani. Unaweza pia kumfunika na blanketi pamoja na tandiko lingine la plastiki ili iwe rahisi zaidi wakati wa kufanya usafi.Endapo mwanao atajaribu kukusaidia, msifie kwa kujaribu na kwa kusaidia kufanya usafi.

Imeandaliwa na Dkt. RAYMOND BANDIO (MD)
UKOJOZI KITANDANI KWA WATOTO (Bed-Wetting) -Enuresis
 
Asante na mungu akubariki maana hiyo imekuwa issu kubwa kwenye familia yangu
 
Lakini kuna swala la kuweza kurekebisha hali kwa kuongezea tu.

Kwa watoto wenye miaka 6> basi waeuke kula vitu aina ya vimiminika baada ya saa kumi na mbili jion. hali hii itamfanya mtoto awe ameshakojoa japo mara 3 kabla ya muda wake wa kulala saa mbili usiku. hii inapunguza kiwango cha mkojo utakao tengenezwa usiku na pia kama mzazi akifanikiwa kumwamsha saa 7 usiku ili akoje basi over time tabia hii itastop.
 
Back
Top Bottom