Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapana sio mimbaMimba
Nimekupata mkuu nashukuru kwa ushaurHiyo itakuwa ni Amenorrhea(Absence of menstruction)""
Inabidi uende kwenye vituo vya afya upewe maelekezo mkuu
Poa poaKama ni mtumiaji wa dawa za uzazi wa mpango kuogopa mimba inawezekana hiyo
Asante sana bossKUKOSA MZUNGUKO WA HEDHI AU HEDHI KWA MUDA MREFU(AMENORRHEA)
>UTANGUKIZI,KWA kawaida mwanamke au msichana huwezi kupata hedhi kabula ya KUBALEHE,WAKATI WA UJAUZITO NA BAADA YA KUFIKIA UKOMO WA KUINGIA KUNAKO HEDHI(MONOPAUSE).kama mwanamke hatopata hali hii wakati ameshabalehe,hana mimba,na hajafikia ukomo basi kuna dalili tosha kuwa anahitaji matibabu ya kitabibu kutatua tatizo hili.
[emoji256]KUKOSA HEDHI NI NINI?,ni ile hali ya mwanamke kutokuona siku zake kwa muda mrefu kinyume na matarajio ya kawaida au mzunguko wa kawaida yapata miezi hata 3 HADI 6 au amebarehe lakini mpaka anafikisha umri wa miaka 16 hajaona hedhi.
[emoji95] KUNA AINA KUU MBILI ZA KUKOSA HEDHI[emoji95]
1.PRIMARY AMENORRHEA,hii ni hali inayompata mwanamke kwa kutokuona hedhi kwa Mara ya kwanza katika umri wa miaka 12,14,16 NA kuendelea,
☄sababu kubwa ya hali hii husababishwa na aiza mabadiliko ya organs,tezi na homoni zinazojihusisha na maswala ya hedhi.
☄SABABU AMBAZO ZINAWEZA PIA KUCHANGIA NI KAMA
1.kushindwa kwa ovaries (ni organi inayoshikilia mayayi)
2.matatizo ya mifumo ya fahamu(ubongo na ugwe mgongo au tezi za pituitary(hii ni tezi katika ubongo inayofanya homoni ya hedhi kutoka)
3.utengenezwaji hafifu wa wa organ katika mwili uhusuo HEDHI, lakini Mara nyingi sababu hasa za hii primary hazijajulikana sana yawezakuwa tatizo la kimazingira au kuzaliwa nalo(natural factor).
2.SECONDARY AMENORRHEA,hii ni hali ambayo mwanamke anaweza kutokupata hedhi wakati hapo awali alikuwa anapata yaani kusimama au kutokuona kwa muda usiopungua miezi 3 HADI 6 nakuendelea.
[emoji95]SABABU YA SECONDARY AMENORRHEA INAWEZA KUSABABISHWA NA
1.UJAUZITO
2.KUNYONYESHA
3.KUACHA MATUMIZI YA UZAZI WA MAPANGO
4.KUFIKIA UKOMO WA KUPATA HEDHI(MONOPAUSE)
5.MATUMIZI YA UZAZI WA MAPANGO KAMA DEPO-PROVERA.
[emoji95]SABABU ZINGINE NIKAMA
1.musongo wa mawazo (stress)
2.mlo hafifu(kutokupata chakula IPASAVYO)
3.huzuni(depression)
4.matumizi ya dawa kama dawa za kutibu CANCER,PSYCHOSIS OR SCHIZOPHRENIA NK.
5.kupungua uzito kwa haraka
6.kufanya mazoezi kupita kiwango
7.kuwa na magonjwa endelevu au ya Mara kwa Mara
8.kunenepa ghafula(overweight-obesity)
9.mvurugiko wa homoni inayisababishwa na matatizo ya uvimbe kwenye ova (PCOS-POLYCYSTIC OVARIAN SYNDROME)
10.matatizo ya tezi ya thyroid
11.uvimbe kwenye ovaries
12.kiwango kidogo cha homoni ya ESTROGEN na kiwango kikubwa na TESTOTESTRONE
[emoji95][emoji95]DALILI ZA AWALI ZA MWANAMKE MWENYE SECONDARY AMENORRHEA
☄acne(chunusi)
☄uke kukauka(vagnal dryness)
☄sauti kunyon'gonyea
☄nywele kutoa kwa kiwango kikubwa mwilini
☄kichwa kuuma
☄mabadiliko ya kuona
☄bubu kutoa Maji au chuchu kutoka Maji kama Maziwa
[emoji269]Mara upatapo dalili HIZI au tiari unatatizo hili basi usiwe na wasiwasi tatizo hili linatibika,ila ...
[emoji269]NENDA HOSPITALI UKAFANYIWE UCHUNGUZI WA KINA KAMA VILE
~VIPIMO VYA MRI,CT SCANS,KIPIMO CHA KIWANGO CHA testosterone NA ESTROGEN,ULTRASOUND,KIPIMO CHA UVIMBE AU KITUCHOCHOTE KINACHOKUWA KATIKA OVARIRS AU MLANGO WA UZAZI
Pia vipo vipimo vingi kulingana na Maelezo na historia ya tatizo.