Tatizo la Kukosa Hedhi (Amenorrhea)

Tatizo la Kukosa Hedhi (Amenorrhea)

Mke wangu akijifungua hapati hedhi mpaka amwachishe mtoto vipi mzizi mkavu na hii ni tatizo?
 
Pole sana ndugu ningekushauri pia uende kupima Hormone zako Hospitali. Tumia hii dawa itaweza kukusaidia inshallah.
TIBA YA HEDHI INAYOCHELEWA KUTOKA KWA SIKU ZAKE AU KUTOKA KABLA YA SIKU ZAKE KUFIKA: Hapa maana yake ni kuwa baina ya hedhi mbili huenda yakakaribiana sana au kuachana sana kinyume na ada. Yaani siku za tarehe zake haziendi sawa Chukua bakdonise (parsley) gramu 50 kisha uweke ndani ya maji lita moja, ichemshe kwa muda wa dakika tano na ikishapoa uchuje. Kunywa glasi moja kutwa mara mbili.
Mke wangu akijifungua huwa hapati hedhi mpaka amwachishe mtoto ndiyo inarudi hedhi je hiyo ni tatizo?
 
Nina siku nyingi girl friend wangu ananiuliza nn tatizo la kukosa siku zake ,yani kwake inaweza kutokea kwa miezi mitatu au isitokee kabisa yani inakuja tu kama emergence kwake
Msaada kwenu ndg zangu.
 
Habari wakuu,

Jamani nina miezi mitatu sijaona siku zangu (bleed) najiuliza nini sababu?

Natumai kuna wataalamu humu wanaoweza kunisaidia.

Natanguliza shukrani.

========


CHANZO CHA MWANAMKE KUKOSA HEDHI (AMENORRHEA)
IMG_7725317000339.jpeg

AMENORRHEA
~hii ni hali ya mwanamke ambaye amepevuka na kukomaa maumbile yake ya Uzaz kushindwa kupata siku zake (breed), tatizo hili limekua likiwasumbua na kuwaletea usumbufu wa kisaikolojia wanawake wengi
~tatizo hili la kutopata hedhi linaweza kutokea awali au baadae kabisa hivyo kuna aina mbili za amenorrhoea

(A) PRIMARY AMENORRHEA ~hii ni hali ya kukosa hedhi inay
oweza kumtokea msichana aliye katika umri wa kubalehe ambayo huweza kuendana na kutopata mabadiliko ya kimaumbile yanayotokea kipindi cha kuvunja ungo (kubalehe)kama vile kuota nywele sehemu za siri, kuota matiti Lakini pia hapati hedhi

(B) SECONDARY AMENORRHEA ~hii ni hali ya kukosa hedhi inayomtokea mwanamke ambaye si mjamzito wala hanyonyeshi na ambaye hajakoma hedhi (menopause) na wala hatumii dawa za Uzazi wa mpango ambapo pia awali alikua akipata kama Kawaida Lakini akasimama kwa muda

NAMNA AMBAVYO MWANAMKE HUPATA HEDHI
~kwa Kawaida ili mwanamke apate hedhi katika mzunguko uliosawa ni lazima tezi ya hypothalamus na pituitar pamoja na kiwanda cha mayai (ovaries) viwe vinafanya kazi kwa ushirkiano yani sawasawa

VYANZO VYA TATIZO HILI
Vyanzo au visababishi vya tatizo hili vyaweza kuwa katika Makundi matatu ambayo huhusisha mfumo wa homoni, mfumo wa njia ya Uzazi, mfumo wa mabadiliko, Vyanzo hivyo ni
matatizo katika hypothalamus ambapo huweza kusababisha matatizo ya mwanamke

Kukosa hedhi
Uvimbe katika ubongo karibu na tezi ya pituitar
ukosefu au upungufu wa homoni zinazochochea kukua na kufanya kazi kwa via vya Uzazi ugonjwa huu hujulikana kama (KALLMAN SYNDROME)
lishe Duni na utapiamlo
uzito mdogo kuliko Kawaida
pituitar kushindwa kufanya kazi baada ya seli zake kufa hii ni iwapo mama alipoteza damu nyingi wakati wa kujifungua

Kuwepo kwa kiwango kikubwa cha homoni ya prolactin katika damu (PROLACTINEMIA)hii prolactin ni homoni inayochangia uzalishaji wa maziwa wakati wa kunyonyesha

Kuchelewa kukomaa kwa viungo vya Uzazi eg, uke na ovary
matumizi ya dawa za Uzazi wa mpango pia ni chanzo cha tatizo hili la kutopata hedhi kutokana na homoni nyingi ya progesterone iliyopo katika dawa hizo eg,

DEPO PROVERA

Msururu wa mawazo
Ugonjwa wa kurithi wa galactosema unaoambatana na kuwa na kiwango kidogo cha sukari aina ya galactose katika damu

Mazoezi makali ya mwili na ulaji mdogo wa Chakula kwasababu tabia hii hushusha homoni ambayo inahusika na kuweka siku zako katika Hali nzuri

Kuziba kwa utando unaozunguka uke (Hymen) hivyo kukosekana tundu la kupitishia damu (IMPERFORATE HYMEN)

Baadhi ya magonjwa ya viungo vya Uzazi husababisha kusimama kwa hedhi mfano wa magonjwa hayo ni POLYCYSTIC

OVARIAN SYNDROME
Menopause (hii ni hali ambayo hutokea kipindi cha miaka 45_60 homoni zinazohusika na kupata siku za hedhi huwa Kwenye kiwango cha chini sana kiasi haziwezi kufanya kazi vizuri

DALILI ZA AMENORRHEA
Mwanamke kuwa na mhemko kuliko Kawaida
mwanamke kuwa mkavu katika uke, kutoka jasho sana wakati wa usiku au mabadiliko katika kupata usingizi vinaweza kuashiria matatzo katika ovary
matiti kutoa maziwa wakati mwanamke si mjamzito wala hanyonyeshi
mwanamke kuwa na vinyweleo vingi na kuota ndevu hii inamaanisha na kuashiria kuwepo kwa kwa wingi wa homoni za kiume za ANDROGEN
kuongezeka uzito kupita kiasi

MATIBABU NA JINSI YA KUJIKINGA NA KUONDOA TATIZO HILI
Matibabu ya kukosa hedhi yanaweza kutibiwa hospital kutokana na chanzo cha tatizo ambapo huwa ni kupewa dawa au kufanyiwa upasuaj

NOTE :::Ni vizuri kuongea na daktari ili ajue ni kwa namna gan atakusaidia pia waweza kufanya mambo yafuatayo kujitibu hili tatizo
ZINGATIA ULAJI ULIOSAHIHI AMBAO UNAHUSISHA ULAJI WA MATUNDA KWA WINGI
IMG_43654834251067.jpeg

Fanya masaji kwenye tumbo la chini kwa kutumia maji ya moto kiasi (uvuguvugu) hii itasaidia kuongeza damu nyingi kutoka
kula chakula kisichotokana na damu hivyo kula chakula chenye protin nyingi mfano nazi, maharage, na karanga tumia juice ya SOY na tikiti maji (watermelon)
 
Hata mke wangu lilimkuta hilo tuna mtoto wa mwaka mmoja na miezi kama minne, december tulikwichi kwich lkn mpaka january nae hajaona siku zake sasa sijui nnn baadaye ikarudi kumbe ni mzunguko tuu ulikaa hovyo
 
Kama ulikuwa na ligi ww ni mama kijo kwa sasa mwez wa kwanza ambapo hujaona hukujiuliza hili swali mpk imefka mitatu?
 
Mpaka umefikia kuuliza hivi naamini hakuna kitu chochote kilichotokea!!!
Pengine mzunguko umesogea mbele
 
Back
Top Bottom