Tatizo la kula udongo: Fahamu visababishi, madhara yake na mbinu za kuacha

ram

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2007
Posts
9,326
Reaction score
8,505

BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA KUHUSU TATIZO HILI
Kwenu madoctor wa JF

Nomba minisaidie, nina tatizo moja, nina kula sana udongo (huku kwetu kanda ya ziwa zinaitwa pemba) nahitaji kujua zaidi ya kupata minyoo na kuumwa ugonjwa wa Amoeba, je kuna madhara gani mengine ya kiafya yanayotokana na kula udongo.

Pili naomba mnisaidie nitumie njia gani ili niache kula hizo pemba, ninakula sana sometimes hadi naogopa, nimeshajitahidi kuacha lakini najikuta ile hamu ya kula udongo iko palepale.
---
---
---
===
UFAFANUZI WA JUMLA KUHUSU TATIZO HILI
Ulaji wa udongo kitaalamu hufahamika kama geophagy. Kitendo cha kula udongo huhusishwa na upungufu wa madini ya chuma mwilini na mara nyingi huonekana kwa wajawazito.
Ukiangalia dunia kwa upana, ulaji wa udongo umefanyika kwa miaka mingi sana mpaka sasa ingawa hutofautiana nchi na nchi, na imeonekana kuwa tabia ya kawaida hasa kwa wajawazito

Ni mara chache sana daktari kumshauri mgonjwa au mjamzito kula udongo, lakini imetambuliwa na wataalamu wa lishe kwamba ulaji wa udongo kiuhalisia una faida mwilini. Ijapokuwa udongo unaweza kubeba sumu hilo nalo wataalamu wa lishe walilitambua.

Watafiti na wataalamu wa afya waliamua kufanya tafifi ili kugundua kama kwenye udongo kuna madini yenye umuhimu hasa kwa mjamzito. Iligundulika kuwa udongo hutumika kama kitu chenye kumuongezea mwanamke mjamzito madini mwilini kwasababu uhitaji na utumikaji wa madini huongezeka zaidi katika kipindi cha ujauzito.

Kiwango cha madini katika udongo hutofautiana sehemu na sehemu lakini mara nyingi udongo hubeba madini ya calcium, iron, magnesium na copper. Madini haya ni ya muhimu zaidi hasa kipindi cha ujauzito ingawa umuhimu wake unahitajika kuwepo katika chakula

Ulaji wa udongo sio hatari labda utolewe sehemu hatarishi. Kwa mfano udongo uliochanganyika na kinyesi cha mwanadamj au uchafu wa kiwandani

KWANINI WAJAWAZITO HULA UDONGO SANA?
* Ulaji wa udongo huwasaidia wajawazito kupunguza athari za ugonjwa ufahamikao kama “morning sickness” na huongeza madini yenye uhitaji kwa mtoto. Morning sickness huwa na dalili kama kichefuchefu, uchovu, kizunguzungu, kujisikia kulala sana. Hii hutokea kwa ukubwa zaidi hasa asubuhi
* Ulaji wa udongo husaidia kulinda tumbo dhidi ya wadudu kuathiri kuta za tumbo
* Wanawake wajawazito hula sana udongo kwasababu wamepungukiwa madini ya chuma

NINI MATOKEO YA ULAJI WA UDONGO KWA MAMA MJAMZITO?
Matokeo ya ulaji wa udongo hupendelewa zaidi kama kinga dhidi ya tatizo la kuharisha.
Kuna matokeo chanya na hasi ya ulaji wa udongo kipindi cha ujauzito ni kama ifuatavyo
* Ulaji wa udongo unaweza kuwa wenye kuvutia lakini kwa muda mwingine, wanawake hula udongo karibia kilo moja kwa siku kwasababu huaminika kuwasaidia kuongeza hamu ya chakula
* Lakini yakupasa kuchukua tahadhari kwamba udongo mara nyingi hubeba bakteria aina ya anthrax ambao hukaa kwa muda mrefu
* Tatizo la kuharisha damu “Dysentery” ni tatizo ambalo huwakumba hasa akina mama wajawazito
* Ulaji wa udongo unaweza kupunguza njaa katika wanawake wajawazito lakini inaweza kusababisha magonjwa mengine
* Ulaji wa udongo unaweza kupelekea choo kigumu. Pia kuna wingi madini ya kaolin kwenye udongo mweupe
* Uwezo wa mwili kufyonza au kupokea virutubishi unaweza kuathiriwa na ulaji wa udongo ambapo hupelekea upungufu wa virutubishi

Vipimo vya damu husaidia kutambua endapo kuna upungufu wa madini au vitamin
Ulaji wa udongo hupelekea ulevi wa kula udongo muda wote

MAONI MBALI MBALI KUHUSU ULAJI WA UDONGO
Wanawake wengi wanaokula udongo, madaktari hutoa tahadhari kwamba ulaji wa udongo usio salama, tabia ya ulaji wa udongo hutokana na upungufu wa madini ya chuma

Dr Lungi Masuku alitoa tahadhari kwamba inaweza kuwa ni dalili za upungufu wa damu uliosababishwa na upungufu wa madini ya chuma
— Kwa wanawake wanaokula udongo yafaa zaidi kufanyiwa vipimo na ikiwezekana aanzishiwe vidonge vyenye madini ya chuma, magnesium au zinc.

Pia Dr Lungi Masuku alipendekeza kuwa wanawake wote wanaokula udongo waanzishiwe vyakula vya maini ambavyo vina wingi wa madini ya chuma. “Udongo ni kitu kigeni ambapo umebeba vitu vichafu na vitu hatarishi hasa minyoo, choo cha ng’ombe na fangasi.

Kuna matatizo mengi ambayo hutokana na ulaji wa udongo ambayo hupelekea mchafuko wa tumbo au utumbo kufunga. Wanawake wanahitaji kuambiwa kwamba kile wanachokula ni hatari”

MAJIBU NA UFAFANUZI ULIOTOLEWA NA WADAU WA JF
---
---
---
 
Pole usipende kuhatarisha afya yako kwa kurithisha mwili pembe is so risk factor for appendicity. Achana nayo usije ukapelekwa operation laparatomy kuwa mwangalifu
 
Hata hayo uliyotaja si madhara tosha au wewe unataka madhara yepi zaidi.Yaelekea labda una upungufu wa madini chuma ,ebu kachek na madokta.
 
Pole usipende kuhatarisha afya yako kwa kurithisha mwili pembe is so risk factor for appendicity. Achana nayo usije ukapelekwa operation laparatomy kuwa mwangalifu

hicho kidole tumbo unakuta umeshatolewa.....what next....
coz hii tabia ya kula udongo....naona inawapata watu wengi siku hizi.....hasa wadada....
 
Kuna mdada alikuwa anakula sana mkaa akaenda kwa TB Joshua kuombewa, kumbe yalikuwa mapepo. Nakushauri ukaombewe.
 
hicho kidole tumbo unakuta umeshatolewa.....what next....
coz hii tabia ya kula udongo....naona inawapata watu wengi siku hizi.....hasa wadada....

ni kweli wadada wengi sana kinawapata asante kuelezea kiswahili chake
 
hicho kidole tumbo unakuta umeshatolewa.....what next....
coz hii tabia ya kula udongo....naona inawapata watu wengi siku hizi.....hasa wadada....
Ukosefu Wa madini ya chuma mwilini pia huwa sababu ya kula udongo, get to see the doctor and have a full blood picture done
 
GEOPHAGY ni dalili ama ya upungufu wa madini fulani mwilini au ni Psychological. Sometimes ni temporary only during pregnancy.

Vyote hivyo ni lazima ufanyiwe vipimo. Kuangalia ni madini gani ama yamepunguwa au huna enzymes za kuyafanya hayo madini yatumike mwilini. Ama kama ni Psychological dependance juu ya huo udongo, basi utahitaji psychotherapy. Bugando hospital vipimo vyote vinawezekana. Goodluck.
 
Reactions: ram
Udongo ule una kuwa un-sterilized na hivyo uwezekano wa kupata maambuziko ni mkubwa sana.
Baadhi ni minyoo, kuna bacteria (na hatari zaidi ni TB) n.k.

Hatari kubwa zaidi inayoweza kukupeleka pabaya ASAP ni kodole tumbo. Hiki hakitibiwi kwa dawa ila operesheni pale kinapokuwa katika kiwango cha juu. Kama upo KM nyingi na hospital kinaweza kupasuka na hapo RIP inakuwa karibu nawe.

Hata kama kimeondolewa bado madhara ya infections zitokanazo na ulaji ni kubwa ! 'The risk outweigh the benefit'
 
Oparation ya kidole tumbo nilishafanyiwa, ila sijui ilitokana na kula udongo au ilitokana na nini

Pole usipende kuhatarisha afya yako kwa kurithisha mwili pembe is so risk factor for appendicity. Achana nayo usije ukapelekwa operation laparatomy kuwa mwangalifu
 
Asante mkuu, Bugando hosp nimuone specialist wa magonjwa gani, manake oparation ya kidole tumbo nilifanyiwa na dr Gilyoma ambapo yeye ni ent surgeon, so naweza muona yeye tena au?

Asante mkuu

 
Oparation ya kidole tumbo nilishafanyiwa, ila sijui ilitokana na kula udongo au ilitokana na nini

kwani ram nawewe ulikuwa unakula udongo ? mara nyingi kidole tumbo husababiswa kuharibiwa kwa ukuta wa tumbo na kusababisha mkusanyiko wa chakula, vitu kama udongo, bacteria, virusi, minyoo iliyokufa .na kufanya kuziba, . siyo udongo tu unaowenza kuwa Umesababisha huenda ikawa bacteria infection
 
Reactions: ram
Yah! Nilikula sana udongo wakati wa ujauzito lakini hata baada ya kujifungua niliendelea kula, na bado nakula hadi sasa ndo sababu nimekuja hapa mnishauri nifanyeje ili niache kula huo udongo

 
Yah! Nilikula sana udongo wakati wa ujauzito lakini hata baada ya kujifungua niliendelea kula, na bado nakula hadi sasa ndo sababu nimekuja hapa mnishauri nifanyeje ili niache kula huo udongo


basi utakuwa na upungufu wa madini nenda hospitali ukapewe dawa kama
iron sulphate zinaweza kukusaidia tuko pamoja ram
 
Poa mtu wangu, I will go.... n thanks for advice

basi utakuwa na upungufu wa madini nenda hospitali ukapewe dawa kama
iron sulphate zinaweza kukusaidia tuko pamoja ram
 
Hii ndo JF you get answers and advice here here.
Kuna dogo langu labwia udongo mpaka kero nadhani yeye atakuwa na deficience ya iron bse hana mimba ni toka ana 10 years leo ana 17 years!
 
Hii ndo JF you get answers and advice here here.
Kuna dogo langu labwia udongo mpaka kero nadhani yeye atakuwa na deficience ya iron bse hana mimba ni toka ana 10 years leo ana 17 years!

Mkuu uko sahihi kabisa, na mie nina ndugu Wa namna hiyo ila baada ya kumpa supplements za Iron kwa kweli ameacha sasa, hebu jaribu kumpa Iron also na folic acid.
 
daaaaah! mazee hata demu wangu ana miondoko hii hii!! cjui ndo atakuwa tayari nshamwambukiza mimba!!! salaleeee!!
 
Naweza kusema ni super addict wa hii kitu inaitwa 'pemba' au udongo flani hivi ambao wanawake wajawazito hupenda sana kuutumia!

yani nikisikia ile harufu ya kimvua kikianza kunyesha kwenye ardhi kavu natamani kujigalagaza hapo chini.
hivi ninavyoandika mate yananidondoka hapa manake nimeumiss.

Nikikosa pemba ya kuuzwa naweza kula hata ule unaotengenezwa na mchwa ule wa kwenye miti, kama kuna nyumba ya udongo hapo lazima nibomoe, nitafute kichuguu etc (im not joking jamani wala sijiendekezi)

Je, kuna madhara yoyote ninayoweza kuja kuyapata?(manake so far sijakumbwa na chochote)
Je nina ukosefu wa nini mpaka nile huu udongo kiasi hichi - wakati mwingine asubuhi hata kabla ya staftahi nabugia pemba mwenzenu.

Nawezaje kuuacha? Nimejaribu sana lakini nimeshindwa.....kuna dawa ya kuacha?

Sijahawahi kuona wanaume wakila pemba - je ulaji huu unahusiana na homoni zozote labda...?
MziziMkavu na wengineo tafadhali msaada wenu ni muhimu katika hili?

Aksante!!!
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…