Habari, naomba mnijuze kitu maana ninahofu mwenzaenu, m ni muathirika wa kula udogo ,yaan ni zaidi ya miaka kumi Sasa nimejaribu kuacha Sana lakini imekuwa ngumu ,Sasa najiuliza mmh ninapatag kinyesi kigumu ,vipi kuhusu wale wanaofanya mapezi kinyume na maumbile ,huku nyuma sehemu ya haja kubwa si kunakuwaga kumepanuka? Vipi kwa mtu anayekula udongo c kinyesi kinakuwa kigumu sana haiwezi kuwa athari ni sawa na ya mtu anayefanya kinyume na maumbile? Naogopa maana Kuna wakat hadi naskia sehemu ya hajakubwa kunawasha mno jaman, msinipopoe ,jibuni tu kistaarabu nami niondokane na janga hili
ULAJI WA UDONGO NA MADHARA YAKE:
Kwa kawaida ulaji wa udongo husababishwa na mambo yafuatayo:
1.Upungufu wa madini ya chuma na zinc mwilini.
Hii ni kutokana na lishe duni au kupoteza damu nyingi wakati wa hedhi au upungufu wa madini chuma kutokana ugonjwa wa minyoo na safura.
2.Unywaji chai yenye majani ya chai au kahawa wakati wa kula,ambayo huzuia madini ya chuma kufyonzwa au kuharibiwa inapoingia mwilini.
3.Upungufu wa dawa ya kuyeyusha chakula tumboni (hydrochloric acid) pia husababisha tatizo hili.
MADHARA YA KULA UDONGO:
Kula udongo na vitu vingine ambavyo si chakula kunaweza kusababisha madhara ya kiafya kama ifuatavyo:
*Kwa kuwa udongo unaweza kuwa na sumu za dawa za mimea na mbolea kama vile lead, dioxin na madini mengine yenye hatari yanayopatikana kwenye udongo uliochafuliwa, hivyo inaweza kusababisha matatizo ya kiafya mwilini mwako.
*Husababisha mikwaruzo, michubuko na kupata majeraha ya ndani kwenye utumbo.
*Ugonjwa wenye homa na maumivu makali unaojulikana kama appendicitis ambao tiba yake ni upasuaji.
*Kupata minyoo aina ya safura.
*Kukosa choo na tumbo kuuma kwa siku nyingi bila sababu.
*Bawasiri
*Saratani ya utumbo
*Kwa kuwa mara nyingi udongo huchafuliwa kwa vinyesi na mikojo ya binadamu, ndege na wanyama kama mbwa nk, basi hali hii husababisha udongo kubeba vimelea vya magonjwa.
NIFANYAJE ILI NIWEZE KUACHA KULA UDONGO??
Ifuatayo ni namna ya kukabiliana na tatizo hilo:
*Kula vyakula vyenye madini chuma na zinc kwa wingi kama vile maharage, korosho, mboga za majani hasa spinach, mayai, nyama, samaki, mbegu za maboga na matunda
*Kutibu minyoo kwa kumeza dawa za minyoo angalau mara moja kwa mwezi.
*Kunywa juice ya spinach na karoti bilauli moja kutwa mara tatu kila siku.
*Kunywa supu ya mbogamboga na mchele.
ANGALIZO
Usinywe vinywaji vyenye caffeine wakati wa kula chakula.