Tatizo la kupoteza uwezo wa kunusa (Kutosikia harufu): Fahamu chanzo na namna ya kutibu tatizo hili

Wiki Kama tatu zilizopita Hali hii ilinitokea,sikua naweza kunusa harufu ya kitu chochote Wala kuhisi ladha yoyote,Hali ile ilidumu Kama wiki moja na nusu bila kutumia chochote taratibu nikaanza kunusa na kupata ladha ya vyakula.Mpaka muda huu naweza kuinusa mpaka kesho
 
Wakuu msaada hapa nina siku tano sisikii harufu wala ladha ya kitu chochote, najua tatizo ni nini na nishapata nafuu homa imeisha niko fiti kabisa. Shida yangu nahitaji kama kuna mtu alipitia changamoto hii ya kutosikia harufu yoyote alitumia kitu gani cha asili au dawa gani kurudisha ladha na harufu.
 
Hali yako ya kawaida itarudi tu mkuu kuanzia kwenye siku ya 10 mpaka wiki mbili,ondoa shaka.
 
Kwa hiyo hapo anaweza kula hata mbao na ikawa poa!? kama ndivyo tatizo liko wapi na uchumu huu wa kati?
 
Kwasababu rais kaongea jana au si... Kwani ile ya mwaka jana uliponaje?
 
Pole mkuu , ngoja tuendelee kujifukiza
 
Pole sana mkuu, endelea kuvumilia. Mimi ilinichukua wiki 3 kupata ladha na kusikia harufu.
 
Fanya therapy itakayosaidia kuamsha sense kwenye ubongo pale unapokua unanusa !!!

Yalinikuta pia nikipata nafuuu ndani ya cku 3

1; kwanza nilikunywa dawa za mafua nikamalizana na mafua kbs

2;mafua yalipoisha nikaanza therapy sasa kunusa perfume yangu ninayoipenda Kisha nyungu mzeee baba nilipiga nyungu mara 3 KWA siku kwenye yale maji niliweka mafuta ya ndimu,mafuta ya mkaratuc,mafuta ya karafuuuu na vix!!!!(haya mafuta niliyapata sokoni mwananyamala kwenye duka linauza vitu vya asili)

a)Siku ya kwanza hola ila cku ya pili kuamkia ya tatu asubui nikanusa kiperfume changu kdg weeeee nikackia hrf hiiii cku nilipiga nyungu mara nne nilifurahi Sana kupata nafuuu!

a)Siku ya 4 nikaanza kuckia na hrf ya chakula!!!

4;chai ya tangawizi na limao ndo ilikua kinywaji changu kikuuuu!!!

5: Mungu akutangulie my dear!!!all the best
 
Tupo wengi mm week ya pili hii mkuu sihisi harufu yoyote.
 
Wengine hata hatufatiliagi haya Mambo lakini tunaumwaga na tunashukuru mungu twapona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…