Pole sana, Mimi ilikuwa ni vice versa na ya kwako, Toka naanza kujitambua kuwa ni mtu nilikuwa sipendi baadhi ya vyakula na mboga kama vile kabichi hii ilikuwa hata upike kutokea mbinguni siwezi kula niko radhi nile wali mkavu ila si na hii mboga, tembere nalo nilikuwa silipendi Kila nikilijaribu likifika kooni linarudi mdomoni na kutoka nje, spinachi nilikuwa siipend pia, dagaa hawa wadogo wanawaita kauzu au wa mwanza pia nilikuwa sili na nyingine nyingi....ila baada ya kwenda high school, kurudi likizo nyumbani hivyo vyakula na mboga nilizokuwa sili hapo mwanza nikaanza kula na kuzipenda kama mboga nyingine Hadi Leo chochote kinacholiwa nakula.
Nilichojifunza ni kwamba, mentality inaweza kubadilika...nilibadilisha tu mtazamo na "kujisemea Kila mara kichwani kuwa lazima Nile hivi na vile sitapata kichefuchefu Wala kutapika au kujihisi vibaya" basi taratibu huko high school pesa niliyokuwa nanunulia mboga ninayoitaka Kila siku ikawa saved nikaanza mdogomdogo kula na wenzangu mboga za shule fresh tu...kumbe shida yangu ilikuwa mindset tu, niliikataa hiyo hali.
Labda unaweza kujaribu hii njia yangu ikasaidia mdogomdogo ila tu usijicheat.