Tatizo la kushindwa kuongea(kupoteza kauli)

Umri wake?
Tatizo lilianzaje?
Ana tatizo lolote lingine mbali ya hilo?
Ulimpeleka hospitali gani?
 
Shida ni hiyo imempata binti yangu mkubwa tu gafla hawezi zungumza kabisa hospitali wanasema hawaoni tatizo
Je yawezekana kupona hii shida
Pole sana.

Kushindwa kuongea (speech disorders -aphasia) ni tatizo ambalo huwa na visababishi vyake. Umesema umeenda hospital na kuambiwa hakuna shida, sijajua umeenda hospital ipi?

Ni vyema akaonwa na daktari bingwa ili kuweza kubaini chanzo cha tatizo hilo na hatimaye kupatiwa matibabu.
Kwa hiyo mpeleke hospital kubwa akatibiwe, kuna madaktari bingwa wa masuala ya kuongea (speech therapists) ambao watamsaidia kulingana na visababishi vya tatizo lake.
Kila la kheri.
 
Mdau Hajataja Mtoto ana umri gani, Tatizo hilo limemuanzaje na anapotezaje kuongea..
Zaidi ni Tabia na Ukuaji wake anatakiwa kuelezea Vipi kuhusu Intellectual Yake Imepungua au Bado ipo Intact..
Amewahi kupata Ajali au Aliwahi kumchapa kwa muda mrefu..

Aliwahi kudondoka??
Historia ya Kupata Mshtuko (Traumatic History ikiwemo PTSD)..
Historia ya Kuchalazwa Shulenii...

Kifupi maelezo hayajakamilika
Hajawahi pata na shida yoyote ile hajawahi dondoka afya yake ya akili ipo vizuri tu ,miaka 10 anasikia vizuri anaandika hospital wanasema hawaoni tatizo lolote
 
Pole sana.

Kushindwa kuongea (speech disorders -aphasia) ni tatizo ambalo huwa na visababishi vyake. Umesema umeenda hospital na kuambiwa hakuna shida, sijajua umeenda hospital ipi?

Ni vyema akaonwa na daktari bingwa ili kuweza kubaini chanzo cha tatizo hilo na hatimaye kupatiwa matibabu.
Kwa hiyo mpeleke hospital kubwa akatibiwe, kuna madaktari bingwa wa masuala ya kuongea (speech therapists) ambao watamsaidia kulingana na visababishi vya tatizo lake.
Kila la kheri.
Shukrani
 
Hajawahi pata na shida yoyote ile hajawahi dondoka afya yake ya akili ipo vizuri tu ,miaka 10 anasikia vizuri anaandika hospital wanasema hawaoni tatizo lolote
Nado hujaelezea Anashindwa Kuongea As In how Haongei kabisa (Bubu) ..
Anashindwa Kupanga Maneno vizuri yaani anayafikiria Sana maneno hata ambayo alikuwa anayajua Kutamka zamani..
Au ameanza Kupata Kigugumizii..

Au Amekuawa haongei ila kuna muda anaongea Vizuri tu sana ila kuna muda haongei (Mute)...

Ukiweza Kunichambilulia au Kunipa tatizo halisi ninaweza Kukusaidia ABC...

Bado information nyingi sana umezihold ni Ngumu kusaidika kama Utaleta Maelezo nusu..
 
Pole sana Mkuu

Binafsi mwanangu wa miaka 4 aliwahi kupata tatizo ambalo lilitaka kufanana na la mwanao.

Yeye aliamka ghafla akawa amepata kigugumizi, akawa anapata shida ya kuzungumza Kwa ufasaha

Tatizo ambalo, hadi anafika huo umri, hatukuwahi kuliona kwake.

Baada ya vipimo vya hospitali, pamoja na dawa pasipokuwa na mafanikio.

Niliamua kwenda upande wa pili.

Kuna sehemu nilimpeleka, baada ya Siku Moja ya matibabu akaanza kuongea vizuri kama awali

Kwenye hii Dunia, tuishi tukijua pande mbili za Dunia.

Wakati wewe unawaza mwanao umsomeshe vizuri, yupo mtu anawaza namna ya kumrudisha nyuma.

Mungu atusaidie
 
Shida ni hiyo imempata binti yangu mkubwa tu gafla hawezi zungumza kabisa hospitali wanasema hawaoni tatizo
Je yawezekana kupona hii shida
Huyu mtoto hana shida yoyote , jiangalie malezi yako sio mazuri.

Wazazi mara nyingi huwa tunahisi tunawapenda sana watoto wetu kumbe tunawaharibu .
 
Shida ni hiyo imempata binti yangu mkubwa tu gafla hawezi zungumza kabisa hospitali wanasema hawaoni tatizo
Je yawezekana kupona hii shida
Pole mkuu,Kwa uwezo wa M/mungu ataongea inshall'ah
 
Pole sana Mkuu

Binafsi mwanangu wa miaka 4 aliwahi kupata tatizo ambalo lilitaka kufanana na la mwanao.

Yeye aliamka ghafla akawa amepata kigugumizi, akawa anapata shida ya kuzungumza Kwa ufasaha

Tatizo ambalo, hadi anafika huo umri, hatukuwahi kuliona kwake.

Baada ya vipimo vya hospitali, pamoja na dawa pasipokuwa na mafanikio.

Niliamua kwenda upande wa pili.

Kuna sehemu nilimpeleka, baada ya Siku Moja ya matibabu akaanza kuongea vizuri kama awali

Kwenye hii Dunia, tuishi tukijua pande mbili za Dunia.

Wakati wewe unawaza mwanao umsomeshe vizuri, yupo mtu anawaza namna ya kumrudisha nyuma.

Mungu atusaidie
Wasomi humu wanakuambia uchawi haupo, na utaambiwa unapigia promo mganga wako au ulipoenda, pole mkuu..usielezee zaidi ulimpeleka wapi kupata tiba
 
Back
Top Bottom