Tatizo la kushindwa kuongea(kupoteza kauli)

Tatizo la kushindwa kuongea(kupoteza kauli)

Wasomi humu wanakuambia uchawi haupo, na utaambiwa unapigia promo mganga wako au ulipoenda, pole mkuu..usielezee zaidi ulimpeleka wapi kupata tiba
Kwa Mujibu wa Sensa ya Tanzania ya Mwaka 2022, Msomi wa Tanzania anachukuliwa mtu mwenye Shahada Moja na kuendelea, ambazo binafsi ninayo

Ukichukulia Kila jambo usomi unaweza kumpoteza Kijana wako, ama wewe mwenyewe maisha yako kupotea.

Kuna watu Nchi hii, kazi zao ni kuhakikisha wanakurudisha nyuma Kwa Kila hatua unayopiga. Wakikusgindwa wewe Baba wa Familia, basi familia yako inakuwa next target.

Bahati nzuri, Ushauri wa kumpeleka Kijana wangu upande wa pili nilipewa na Daktari kabisa (MD) baada ya wao kushindwa kubaini tatizo.

Ukiona watu wanapinga hizi habari, nina uhakika hawajawahi kupigwa na kitu kizito
 
Wasomi humu wanakuambia uchawi haupo, na utaambiwa unapigia promo mganga wako au ulipoenda, pole mkuu..usielezee zaidi ulimpeleka wapi kupata tiba
Kwa mtaalam bado zaid ya hospitali
 
Wasomi humu wanakuambia uchawi haupo, na utaambiwa unapigia promo mganga wako au ulipoenda, pole mkuu..usielezee zaidi ulimpeleka wapi kupata tiba
Kwa mtaalam bado zaid ya hospital
 
Badili hospital mkuu huenda kuna vipimo hawana hapo.

Fanya hvyo kabla hawajafika PM kukupa namba zao wazee wa TAWILE.
 
Ni mapepo mkuu na bila shaka atakuwa alikuwa anatoa udenda au kungata meno au kuzungumza akiwa usingizini.
 
Pole sana Mkuu

Binafsi mwanangu wa miaka 4 aliwahi kupata tatizo ambalo lilitaka kufanana na la mwanao.

Yeye aliamka ghafla akawa amepata kigugumizi, akawa anapata shida ya kuzungumza Kwa ufasaha

Tatizo ambalo, hadi anafika huo umri, hatukuwahi kuliona kwake.

Baada ya vipimo vya hospitali, pamoja na dawa pasipokuwa na mafanikio.

Niliamua kwenda upande wa pili.

Kuna sehemu nilimpeleka, baada ya Siku Moja ya matibabu akaanza kuongea vizuri kama awali

Kwenye hii Dunia, tuishi tukijua pande mbili za Dunia.

Wakati wewe unawaza mwanao umsomeshe vizuri, yupo mtu anawaza namna ya kumrudisha nyuma.

Mungu atusaidie
Umeshauri kutokana na wewe ulivotatua tatizo la mwanao lakini jiandae Kwa Mashambulizi kutoka Kwa diaspora na graduate wanaoenda interviews za PSPR
 
Umeshauri kutokana na wewe ulivotatua tatizo la mwanao lakini jiandae Kwa Mashambulizi kutoka Kwa diaspora na graduate wanaoenda interviews za PSPR
Ni kweli Mkuu

Kama umepitia hizi changamoto za kuuguza, lazima utakuwa umekumbana na haya mambo

Alert ya kwanza ni kumwona mtoto wako uliyemlea tangu amejua kuongea

Over suddenly, anakuwa na kigugumizi ambacho hajawahi kuwa nacho tangu amezaliwa

Kama Mzazi lazima ujiulize mara mbili mbili
 
Shida ni hiyo imempata binti yangu mkubwa tu gafla hawezi zungumza kabisa hospitali wanasema hawaoni tatizo
Je yawezekana kupona hii shida
Pole sana kwa hali ambayo binti yako anayopitia. Kushindwa kuzungumza ghafla, huku vipimo vya hospitali kuonesha hakuna tatizo la kiafya lililo wazi.

Hii ni hali inayoweza kusababishwa na mambo mbalimbali kama vile,

1. Tatizo la Kisaikolojia au Kiakili (Psychological Causes)
- Kisaikolojia kama Stress au Mshtuko (Psychogenic Mutism): Wengine wanaweza kupoteza uwezo wa kuzungumza baada ya kupitia hali ya mshtuko, trauma, au tukio la kihisia kali.
- Hali ya Kiakili (Anxiety or Depression): Shinikizo la kihisia linaweza kumfanya mtu kushindwa kuzungumza.

2. Masuala ya Kimwili (Physical Causes)
- Shida ya Mishipa ya Fahamu (Neurological Issues): Ingawa vipimo vya awali vinaweza kuonekana sawa, hali kama stroke ndogo au shida kwenye mfumo wa fahamu zinaweza kusababisha hali hii.
- Shida za Mazungumzo (Speech Disorders): Kuna magonjwa nadra kama selective mutism au conversion disorder yanayoweza kusababisha hali hii.

3. Matatizo ya Hali Maalum (Conversion Disorder)
- Ni hali ambapo mtu ana dalili za kimwili (kama kushindwa kuzungumza) lakini chanzo chake ni kisaikolojia. Hali hii mara nyingi huhusiana na mshtuko wa kihisia.

Jinsi ya Kusaidia na Kupata Tiba
1. Fanya Uchunguzi wa Kina wa Kiafya
- Mfuatilie vipimo vya mara kwa mara kwa wataalamu wa mishipa ya fahamu (neurologists) ili kuhakikisha hakuna tatizo dogo lililofichika.
- Hakikisha binti yako anafanyiwa vipimo vya kina vya MRI au CT scan ikiwa bado havijafanyika.

2. Fanya Uchunguzi wa Kisaikolojia
- Muone mtaalamu wa afya ya akili kama psychiatrist au psychologist. Wanaweza kufanya tathmini ya hali ya kihisia na kisaikolojia.
- Hali kama selective mutism au conversion disorder mara nyingi zinahitaji tiba ya kisaikolojia.

3. Matibabu Mbadala
- Tiba ya mazungumzo (speech therapy) inaweza kusaidia kurejesha uwezo wa kuzungumza.
- Tiba za asili kama mindfulness na mazoezi ya kupunguza shinikizo la kihisia pia zinaweza kusaidia.

Je, Inawezekana Kupona?
Ndiyo, hali nyingi zinazohusiana na kushindwa kuzungumza zinaweza kupona, hasa ikiwa chanzo chake ni kisaikolojia.

Hata hivyo, matibabu na msaada wa familia ni muhimu. Hakikisha unampa faraja, usimuoneshe hofu, na umpe muda wa kupona kwa msaada wa wataalamu.

Ikiwa una maswali zaidi au unahitaji maelekezo maalum, usisite kuniuliza.

Ova
 
Umeshauri kutokana na wewe ulivotatua tatizo la mwanao lakini jiandae Kwa Mashambulizi kutoka Kwa diaspora na graduate wanaoenda interviews za PSPR
🤣🤣🤣
Mzee mwenzangu bado hujaiona dunia ilivyo upande wa pili kuna jamaa yangu visigino vilikuwa vinawaka moto. Alihangaika sana hospital na bro wake ni mkemia wa TMDA. Tulicheki na Mtaalamu wa Tiba asilia aisee jamaa kupiga manyanga ikatokea soksi imepigwa kufuli la Solex mtaalam akafanya mambo akainguza na dawa zake ile soksi na akafanya manuva akaivuta funguo ya ile Solex akaifungua kufuri baada ya hapo Mwana akawa sawa mpaka leo anadunda tu.
 
Haya mambo mda mwingine yapo
 
Habari za leo ndugu umefanikiwa kupata msaada
 
Miaka 10 hebu mwambie aliota Nini day before hajaanza kupata changamoto hyo au week before.

Haiwezi ikaja tu hyo lazma Kuna sababu ya kimwili basi badilisha hospital mapema.
 
Back
Top Bottom