Tatizo la kutokwa Jasho lisilo la kawaida katika sehemu mbalimbali za mwili (Hyperhydrosis)- Fahamu Chanzo, tiba, ushauri

Tatizo la kutokwa Jasho lisilo la kawaida katika sehemu mbalimbali za mwili (Hyperhydrosis)- Fahamu Chanzo, tiba, ushauri

Jamani naombeni msaada kwan hili tatizo la kutoka jasho kwapani linaninyima raha na ata uhuru wa kuvaa nguo.

Je nitumie dawa au deodrant gani..?msaada plz.

jamani kwapa zangu zinatoa jasho mpaka nakosa uhuru wa kuvaa nguo., navaa nguo nyeusi tu.,naombeni msaada nitumie deodorant gani au dawa gani.,msaada tafadhali.

Mwenye ujuzi atoe msaada hapa
MziziMkavu na wengine
 
Last edited by a moderator:
Tumia deodorant ya NIVEA inaitwa DRY COMFORT. . Hii ni kama unatokwa na jasho au hata jasho lenye harufu mbaya. Sh.5000 tu ina kopo jeupe, jitahidi kuipata itakusaidia
 
Jamani naombeni msaada kwan hili tatizo la kutoka jasho kwapani linaninyima raha na ata uhuru wa kuvaa nguo.

Je nitumie dawa au deodrant gani..?msaada plz.

Tumia deodorant ya NIVEA inaitwa DRY COMFORT. . Hii ni kama unatokwa na jasho au hata jasho lenye harufu mbaya. Sh.5000 tu ina kopo jeupe, jitahidi kuipata itakusaidia
 
Jamani naombeni msaada kwan hili tatizo la kutoka jasho kwapani linaninyima raha na ata uhuru wa kuvaa nguo.

Je nitumie dawa au deodrant gani..?msaada plz.
kamulia limao kwenye hilo kwapa lako jasho litakatika mercy heart

1024px-Lemon.jpg
 
Last edited by a moderator:
Jaribu hii kitu labda itakusaidia.



 
Last edited by a moderator:
habari ndugu zangu. kuna rafki yangu iwe ni baridi. iwe ametoka kuoga iwe amevaa nguo ya wazi. ye anavuja jasho kwapani na tumbon sometime.. msaada plz wa jinsi ya kutatua hilo tatizo
 
Sioni kama ni tatizo, ni maumbile, ni vile tu joto lake la mwili limejikita sana maeneo hayo. Kuna wale ambao wanatokwa na jasho kwenye viganja vya mikono masaa yote akiandika kitu karatasi yote huloana. Wapo wanatokwa makwapani, mgongoni, usoni, Viunoni. Ni maumbile tu.
 
Tumia deodorant ya NIVEA inaitwa DRY COMFORT. . Hii ni kama unatokwa na jasho au hata jasho lenye harufu mbaya. Sh.5000 tu ina kopo jeupe, jitahidi kuipata itakusaidia

Ni kweli lakini mbona baada ya kuitumia ikichanganyikana na jasho ndiyo inakua balaa au kwanini wengine hata wakikaa kwenye Ac wanatoka jasho kwenye kwapa na wakitoka humu jasho linakuwa balaa kama jasho la chokolaa
 
mwanangu ana tatizo la kutokwa jasho pindi anapolala, naomba wadau mnishauri, nini tatizo?
 
Hyperhidrosis ni ugonjwa wa kutokwa na jasho jingi kuliko kawaida. Kutokwa na jasho ni hali ya kawaida kwa binadamu na wanyama na kazi kubwa ya jasho ni kupoza mwili unapopata joto kubwa. Kwa kawaida mwili wa mwanadamu hutengeneza wastani wa lita moja ya jasho kila siku.

Kiwango cha jasho huweza kutofautiana kutokana na mazingira na hali ya mwili kwa mfano kipindi cha joto ama maeneo yenye joto kali, au kufanya mazoezi ya mwili kama kukimbia hufanya mwili kutoa jasho jingi zaidi ya kawaida ili kupooza mwili.
what-is-botox-how-does-botox-work-axillary-hyperhidrosis.png


Ugonjwa wa hyperhidrosis hutokea pale mwili unapotengeneza jasho jingi zaidi ya linalohitajika kupoza mwili. Mfano ni kutoka jasho ukiwa umepumzika sehemu isiyo na joto au kutoka na jasho jingi unapoingiwa na hofu nk

Kitaalamu ugonjwa huu umegawanyika katika makundi mawili. Kuna primary hyperhidrosis na secondary hyperhydrosis. Primary hyperhydrosis huanza mara nyingi kipindi cha balehe na husababishwa na urithi wa vinasaba (genetics). Secondary hyperhidrosis huanza kipindi chochote cha maisha na husababishwa na magonjwa mengine ya mwili mfano kisukari, magonjwa ya tezi ya shingo na kadhalika.


Hyperhydrosis ni kilema kilichojificha

Mgonjwa wa hyperhidrosis hupata shida kuendana na shughuli za kawaida za maisha. Wengi hupatwa na aibu pindi jasho jingi linapolowanisha nguo au kushindwa kushikana mikono pindi viganja vinapolowa jasho jingi. Pia kuna baadhi ya shughuli humwia vigumu mfano jasho jingi mikononi husababisha ugumu wa kushika vifaa kipindi cha kazi. Ugonjwa huu huweza kusababisha msongo wa mawazo.

Tiba

Kuna tiba mbalimbali ya ugonjwa huu. Secondary hyperhidrosis hutubiwa kirahisi kwa kutibu ugonjwa unaosababisha secondary hyperhidrosis kama ilivyoelezwa hapo juu. Kwa hiyo ni muhimu kumuona daktari pindi unapopata na tatizo hili na kufanya vipimo ili kugundua magonjwa sababishi mfano kisukari na Magonjwa sababisha yakitibiwa na ugonjwa huu huisha mara moja.

Nitazungumzia zaidi primary hyperhidrosis ambayo husababishwa na vinasaba. Tiba yake nimeigawanya mara tatu. Kwanza ni kubadili mfumo wa maisha, pili ni dawa na tatu ni upasuaji.

Tukianza na kubadili mfumo wa maisha. Mgonjwa mwenye hili tatizo yampasa kubadili mfumo wake wa maisha ili kuendana na tatizo.

Kwanza inashauriwa kunywa maji mengi. Maji husaidia kupoza mwili na hivyo kupunguza kutokwa kwa jasho. Pia inashauriwa kupunguza vyakula vyenye viungo vingi, vinjwaji kama kahawa, pombe, sigara na vinywaji vichangamfu(energy drinks) maana vyakula na vinywaji hivi husababishwa mwili kutengeneza jasho.

Pia inashauriwa kuoga angalau mara mbili kwa siku kwa kutumia maji safi na sabuni yenye dawa mfano dettol.

Pia paka baking soda sehemu zinazotoa jasho jingi pindi tu umalizapo kuoga. Baking soda huharakisha kukauka kwa jasho kwa sababu ya alkalini iliyonayo.

Tumia vitoa harufu (antiperspirants/deodorants) vyenye aluminium chrolide ambayo huharakisha kukauka kwa jasho.

Tumia vikinga jasho (sweat pads) sehemu zinazotoa jasho jingi mfano sehemu za kwapa na kadhalika. Unaweza kununua vikinga jasho madukani au kutengeneza mwenyewe nyumbani kwa kutumia nguo na sponji na kuvaa ndani ya nguo.
hyperhidrosis-liners.jpg


Pia chai ya mmea uitwao salvia officinalis usaidia kupoza mwili na inashauriwa kunywa kwa watu wenye tatizo hili.

Kwenye upande wa dawa, dawa ziitwazo kitaalamu anticholinergic husaidia wenye tatizo la kutokwa na jasho hasa wanaopata tatizo hili wanapoingiwa na hofu ya kitu fulani.

Pia kwenye nchi zilizoendelea huduma ya upasuaji hutumika kwa wenye tatizo kubwa ambalo haliwezi kutibika kwa njia nyingine. Tiba hii inajumuisha kuingilia na kufunga kwa njia ya upasuaji mifumo ya fahamu inayosababisha kutoka kwa jasho.

Ukiachana na upasuaji, tiba ya kubadili mfumo wa maisha na dawa husaidia kwa kiwango kikubwa kwa mazingira yetu hapa Tanzania.
 
Hyperhidrosis ni ugonjwa wa kutokwa na jasho jingi kuliko kawaida. Kutokwa na jasho ni hali ya kawaida kwa binadamu na wanyama na kazi kubwa ya jasho ni kupoza mwili unapopata joto kubwa. Kwa kawaida mwili wa mwanadamu hutengeneza wastani wa lita moja ya jasho kila siku..
Kutokwa jacho kuna changiwa na Mambo mengi.
Naomba nikukumbushe Ugonjwa ambao kwahivisasa ni Commkn unaoitwa "NASAL POLIPS"

Vinyama vya puani husababisha Hewa unayoingia kwenye Mapafu kuwa ndogo hivyo kupelekea Excessive Muscles kupush hiyo hewa kuingia kwenye Mapafu.
Wakati hilo zoezi linaendelea husababisha mtu atokwe jasho hasa maeneo ya USONI.

Tatizo hili humpata mtu hata akiwa amekaa tu ametulia na hafanyi kazi yeyote ya nguvu kwa muda huo
 
Kutokwa jacho kuna changiwa na Mambo mengi.
Naomba nikukumbushe Ugonjwa ambao kwahivisasa ni Commkn unaoitwa "NASAL POLIPS"

Vinyama vya puani husababisha Hewa unayoingia kwenye Mapafu kuwa ndogo hivyo kupelekea Excessive Muscles kupush hiyo hewa kuingia kwenye Mapafu.
Wakati hilo zoezi linaendelea husababisha mtu atokwe jasho hasa maeneo ya USONI.

Tatizo hili humpata mtu hata akiwa amekaa tu ametulia na hafanyi kazi yeyote ya nguvu kwa muda huo

Asante kwa mchango wake. Ila kwa hiyo kesi ya nasal polyps haiwezi ikawekwa kwenye kundi la hypehidrosis kwa sababu, sababu ya mwili kutengeneza jasho iko wazi kabisa... Kwamba mgonjwa anatumia nguvu nyingi kuvuta pumzi kuliko kawaida ni sawa sawa kabisa na unapofanya mazoezi ya viungo..

Pia nikukumbushe tena kama nilivyoongelea kwenye makala yangu hapo juu kuwa kuna magonjwa sababisha ya tatizo hili na ndio inayoitwa secondary hyperhidrosis....magonjwa hayo ni mengi sana na baadhi nimetoa mfano, na tiba yake ni kutibu hayo magonjwa sababishi.

Nia ya makala hii ni kuhusu tiba ya primary hyperhidrosis ambayo chanzo chake ni vinasaba (genetics)....

Nakutakia wikiendi njema.
 
Back
Top Bottom