Tatizo la kutosikia vizuri na body balance

Tatizo la kutosikia vizuri na body balance

Hata mimi nina hiyo shida kwa zaidi ya miaka 10 sasa,nilitibiwa Muhimbili kwa madawa haikuwezekana at last nikaambiwa nitumie hearing aids,nimezitumia lakini zina adha zake ukikaa nazo muda mrefu zikiwa ON masikio yanakuwa hayasikii kabisa,nimeachana nazo ninaishi ninavyojua mwenyewe.

Kifupi masikio naona hayana tiba,ila ni kumuomba Mungu,hakuna linaloshindikana kwake ,nina matumaini kuwa siku moja masikio yangu yatasikia tena,niko kwenye maombi na sitarudi nyuma kwa hilo,mpaka nimepokea muujiza wangu.
Daah!! Noma pole sana mkuu
 
Mimi naomba kuuliza wakuu.

kama kimfano ngoma ya Sikio ndio imekufa kunauwezekano wa kusikia kweli au ndio basi tena..??
Msahada plzzz
 
The same history kama mm,

Mwaka 2009 nipo form two nikaanza kuisi miungurumo katika maskio nikajua ni jambo la kawaida but kadri siku zilivyokuwa zinaenda huwezo wa kuskia ukaanza kushuka hasa rafiki zangu walikuwa wanaliona hili na kuniambia ilikuwa ili niskie lazima uongee mara mbili mbili.

Likizo nilipo rudi home nikafikisha suala hili kwa wazee tukaamua kuattend clinic Bugando hospital nakumbuka dokta aliyekuwa clinic yetu alikuwa anaitwa SOPD bhasi tukafanya med8cal check..including sound checking..huwezo wa kuskia ukaonekana kuwa na dosari baada ya vipimo vyote ikabainika chanzo cha yote ni dawa ya QUININE(zile sindano za kutibu malaria)inasemekana huwa zina athiri mfumo wa fahamu nadhani serikali ilipiga marufuku matumizi ya Quinine.

Nikapewa dawa za Neuros(vidonge flan hivi vya rangi mbili nyeusi na nyekundu) ilikuwa dose ya miezi mitatu kila siku vidonge vinne asee nilitumia kwa miezi sita.

Nikapewa na ratiba ya kurudi bugando kila mwisho wa mwezi kucheki maendeleo lakini haikusaidia kitu.Bhasi nikashauriwa kwenda Dsm kwa matibabu zaidi mwaka 2010 nikaenda dsm hospital ya kwanza kufikia ilikuwa pale EKENWA dispensary pale Magomeni.Baada ya vipimo nikaandikiwa dawa na kushauriwa kutumia Machine za kusaidia kuskia lakini nili KATAA KABISA ingawa mzee alikuwa tayari kulipia ilikuwa kama 300k.

Nikasema potelea mbali hata shule nitasoma hivyo hivyo wala sikujari shule ikawa mm ni kujisomea nipe notice tu basi inatosha maana darasani mwalimu sikumskia vizuri kilichosaidia nilikuwa na msingi mzuri wa elimu toka primary sikuwa kuwa nje ya top 15 ya darasa nikaua up to now nina degree

Lakini nilipewa utaratibu hospital kama kula matunda sana..kuacha kula nyanya nyanya na vitu vibichi pamoja na kutumia mashuka safi na kuacha kukaa mazingira yenye vumbi vumbi asee maisha haya nilihisi kuwa mpweke nikwa nakaa mbali na watu kuogopa kuchekwa kuwa sis8kia vizuri.Nikabadili mfumo wa maisha nilikuwa mcheza mpira mzuri nikaacha maana uwanja wa shule ulikuwa gumbi tupu .Maisha yakaendelea kwa namna hii.

Kadrii miaka ilivyokuwa inaenda kidogo nafuu ikawa inakuja ingawa sijawahi kuwa normal kabisa lkn sasa na nafuu napiga story kama kawaida ni ngumu kunifahamu.

Haya mambo hutokea tu natural muhimu ni kukubali tu jinsi ulivyo

Sent from my SM-J730F using JamiiForums mobile app
 
The same history kama mm,

Mwaka 2009 nipo form two nikaanza kuisi miungurumo katika maskio nikajua ni jambo la kawaida but kadri siku zilivyokuwa zinaenda huwezo wa kuskia ukaanza kushuka hasa rafiki zangu walikuwa wanaliona hili na kuniambia ilikuwa ili niskie lazima uongee mara mbili mbili...
Pole sana mkuu
 
Kwenye simu naongea vizuri na hata mtu akiongea nasikia ila tu akiongea kwa sauti ya chini ndio napata shida kusikia mpaka nimsogelee au nimwambie aongeze sauti
Kama Mimi. Jana nimefaulu interview ya kazi,lakini kutosikia kumeniangusha. Tatizo Kama labkwako
Ni ngumu kuishi hivo asikwambie mtu nmexperience na naendelea kuxperience
sometimes unaweza ishi kama uko hell

unakuta mtu anaamua kukukejeli ,aweza kuita kukupima tu ukiitika anakwambia basi anacheeka... usiombe yakukute ungali bado shule ya msingi au secondary hayo manyanyapao utajuta.

kuna mtu alimkejeli dada mmoja alikua hasikii kabisa nilijiskia vbaya, Mungu ni mwema yule kaka mwaka juzi kaumwa sana dawa zinakaja ku affect masikio hasikii kabisa.

usiwacheke watu kilema, wengi wetu tumepata kutokana na dawa za hosp affect zake mfano mimi quinine...

imeniathiri mpaka leo sinaga marafiki,rafiki yangu huwaga ni simu tu.sitakagi kuwakera watu
Hayo yote nayapitia hata uwe na cheo kazini wanakuchukulia POA tu.
facing the same problem.quinine imeniharibia mengi maishani.
japo sikia moja ndo zito but nashindwa kuelewa speech..
nimelipata nkiwa primary taratibu linakuwa worse..
momenta zote nlizopitia.dharau..
my phone is my only friend
nimemeza hayo madawa ya neurotone miezi mitatu kila siku.nkarudi khuzema akaniambia niendelee na doz tena miez mitatu.
now nimeishia kwa muhindi na haering aid..atleast sio kama zile za mchina..hazinipiaumivu hizi.na sauti yake ni clear...tatizo kuongea na simu.

lakini tangu nichomwe hiyo quinine mwaka 2005 mpaka sasa miaka 12 sijaumwa malaria tena.ilhali n nna watu nmaoishi nao wanaumwaga.?? kwanini
Naomba Bei ya hiyo hearing device
 
Kama Mimi. Jana nimefaulu interview ya kazi,lakini kutosikia kumeniangusha. Tatizo Kama labkwako

Hayo yote nayapitia hata uwe na cheo kazini wanakuchukulia POA tu.

Naomba Bei ya hiyo hearing device
pole sana ndugu yangu
 
Dah nna mtu wangu wa karibu anapitia hii hali ye yote mawili yameziba na miguu inaishiwa nguvu (kumbe vinahusiana?) Hawez kutembea mwenyewe, vipimo wamesema apewe hearing aid

Sent using Jamii Forums mobile app
Vina mahusiano na hata ukienda hospital watakucheck masikio alafu wataenda kwenye pia, mfano mie huwa nina shida na pua (plus allergy especially ya vumbi na sometimes baridi) na nilienda Ekenywa Hospital pale Magomeni walinicheck pua na wakacheck pia masikio na koo.

Kwahiyo hata huyo ndugu yako wako karibu anavyopitia Kwa namna moja ama nyingine imechangiwa na masikio
 
Kama Mimi. Jana nimefaulu interview ya kazi,lakini kutosikia kumeniangusha. Tatizo Kama labkwako

Hayo yote nayapitia hata uwe na cheo kazini wanakuchukulia POA tu.

Naomba Bei ya hiyo hearing device
Pole sana,zinaanzia Tshs 50,000 ni za kichina na kupanda,ila ziko mpk za Miliion ni uwezo wako tu mkuu...
 
Toka 2008 , sikio la kushoto linaunguruma nikiwa chuo first yr...nimetibiwa sana lakini wapi.

Nilichoweza ni kukaa na hii siri ukitoa ndugu wa familia na wazazi, chuoni&makazini hawajawai jua kuwa kuna upande sisikii,una kuna namna najipozisheni nikikaa na mtu, la sivyo anavopiga story nitakuwa naangalia face expression yake .

Ninaposafiri nahakikisha napata siti ambayo sikio zima litakuwa upande wa jirani, nikikosa navaa ear phone ili asinisumbue kunisemesha.

Huwa siona haja wajue changamoto yangu maana najua hawatonisaidia kitu, Tinnitus haina dawa.
 
Pole sana,zinaanzia Tshs 50,000 ni za kichina na kupanda,ila ziko mpk za Miliion ni uwezo wako tu mkuu...
Hizo za 50,000 cyo hearing device ni amplifier wakuu badala ya kutatua shida yako ya masikio inaenda kuharibu kabisa masikio maana hazijawa programmed kuendana na tatizo lako la uckivu lilipo yenyewe inafanya kazi kuamplify saut tu
 
Hizo za 50,000 cyo hearing device ni amplifier wakuu badala ya kutatua shida yako ya masikio inaenda kuharibu kabisa masikio maana hazijawa programmed kuendana na tatizo lako la uckivu lilipo yenyewe inafanya kazi kuamplify saut tu
Najua hujui unachokiongea,mimi nimeshatumia cha lk 5 hakina tofauti na hicho cha elf 50,tofauti ni umbo tu.Ndio maana namshauri aanze kutumia vya bei rahisi kabla hajapigwa...
 
Wakuu mimi ni kijana(19 years now) nina tatizo la kutosikia vizuri na body balance(nimesoma science kidogo naelewa masikio ndio yanayo control body balance) hili tatizo limenianza mda sana tangu nipo mdogo wa miaka kama 9 hivi sasa limekuwa kubwa kiasi kwamba nahitaji attention kubwa sana kuongea na mtu na mara nyingi nikitembea huwa siendi sawa(napepesuka mda mwingine hadi kudondoka).

Hospital nimeenda mara y kwanza muhimbili mwaka 2009 na mama nilichunguzwa nikaambiwa nahitaji hearing device na kwa kuwa gharama ilikuwa kubwa bi mkubwa alishindwa kumudu, by 2012 baba akafanikiwa kuipata hiyo hearing device ambapo niliitumia ila ikawa nikivaa sana masikio yanazidi kuuma, hii ilipelekea kwenda tena Hospital mara hii ikiwa ni CCBRT hapo tukaambiwa twende ekenwa(Hospital flani hivi ipo magomeni) tulivyofika pale na kupimwa solution ilikuwa kutumia kwanza dawa flani hivi zinaitwa neorouns(kama sijakosea) kwa miezi mitatu mfululizo then nikimaliza niendelee kutumia hearing device.

Hii haikuniletea nafuu yoyote mpaka namaliza form four na kwenda likizo ifakara kwa babu, nikiwa huko baada ya miezi kadhaa masikio yakawa ya nauma sana, nikapelekwa Hospital na babu (st Francis Hospital ifakara) baada ya kunichunguza wakaniandikia barua ya rufaa kwenda muhimbili surgery department.. Baada ya Kurudi dar na kwenda muhimbili mzee akanambia gharama ni kubwa sana kwa sasa na yeye hana pesa.

Natumai kuna madaktari humu mnipe japo ushauri wa nini cha kufanya maana nimeshindwa kwenda chuo sababu ya masikio na naona kadri siku zinavyokwenda ndivyo yanavyozidi kupoteza uwezo wake.

Natumai mtanisaidia kwa hili Doctors

USHAURI NA MAONI YALIYOTOLEWA NA WADAU


...Yaani Hospital kubwa ya CCRBT ikashindwa tatizo lako na kukurlekeza Zahanati.ya Magomeni ??? [emoji848][emoji848]
 
Najua hujui unachokiongea,mimi nimeshatumia cha lk 5 hakina tofauti na hicho cha elf 50,tofauti ni umbo tu.Ndio maana namshauri aanze kutumia vya bei rahisi kabla hajapigwa...
Kampuni gan umetumia?
 
Back
Top Bottom