Habari za Asubuhi Jf members, Mnisamehe kwa wale watakaoguswa moja kwa moja na hii topic, lakini natafuta suluhu ya hili tatizo. Nianze na Mada tajwa hapo juu.
Mimi kwa nature ya kazi ninayoifanya huwa nacollide na wateja wengi kwa siku, kero ninayokutana nayo ni baadhi ya wateja kuwa na Vinywa/midomo inayotoa harufu kali sana mpaka nashindwa kuhimili,
inanibidi nimwambie mteja 'subiri kule', huku nikiwa nimepinda shingo.
Hali kadhalika katika Discussion Chuoni nimekutana na watu wa aina hii (ofcourse wapo wanawake na wanaume), hali kadhalika ukimpa mtu lifti bahati mbaya unakuta yuko vile, safari inakuwaga chungu, na ndiyo chanzo kikuu cha kutokutoa lifti kiti cha mbele. Kidogo inanipa shida kuelewa, TATIZO NI NINI?
Hebu tuwasaidie, inawezekana hii ikawa kama Marudio, lakini naomba Majibu.