Pole Sana! Mie tatizo hilo linanikuta hasa nikioga maji ya baridi. Nafuu yangu ninapooga maji ya moto. Kushindana na hali hiyo mara baada ya kuoga huwa navaa jacket zito ili mwili kupata joto haraka. Hospitali zote nilizopita sijapata majibu ya kutatua tatizo wala kuweka hapa. Narudia kukupa pole maana shida hiyo ninaiishi.
Ndugu zangu huu ni mwaka wa 10 tangu tatizo la kuwashwa kila nikioga linianze nishazunguuka mpaka sasa nimechoka yoyote anae weza kunisaidia jinsi ya kupona naomba anisaidie
Kumbe tuko wengi mimi nikoga maji baridi nawashwa sana ila maji moto aaahh napeta tu hujasema waoga maji gani
ni ushauri mzuri.
Sidhani kama kuna dawa hospital, nilizunguka wewe but dawa ni hii ukimaliza kuoga jikaushe fasta paka mafuka then vaa nguo, hayo yote yafanye ktk muda mfupi maybe utasaidika, mimi ndivyo ninavyofanya japo wakati mwingine nikipigwa na baradi hasa ile ya jioni jioni nawashwa pia so muda mwingi nakuwa na mtandio au jacket nikijifunika tu siwashi. Ni shidaaaaa yaani
Nafikiri naweza kuwasaidia katika hili wale wote wenye tatizo la kuwashwa watumiapo maji ya baridi au ya chumvi: Tatizo hili mara nyingi linasababishwa na mambo makuu mawili
1) kuwa na minyoo
2) kuchafuka damu, yaani damu kuchafuka na wengine wanaota majipu kabisa.
SOLUTION: Hebu tumieni dawa moja ya kienyeji inaitwa Oloodwa(kwa kimasai) inachanganywa kwny chai ya rangi au kula hivyo hivyo japo inawasha sanaaa kwny koo.Tatizo likiwa chronic kuna nyingine wamama wa kimasai wanamix na hiyo kwa pamoja.
Hiyo ni dawa specifically kwa ajili ya kusafisha damu tu na pia kuupa mwili joto hata kama hali ya hewa nje ni ya baridi.
Nawatakia mpole salama.
Unatumia maji ya chumvi mkuu?
Mkuu hiyo itakuwa ni Water allergy au Aquagenic urticaria. Ni allergy dhidi ya maji ya moto au baridi au yenye chlorine au yasiyowekwa chlorine. Ni kitu kinachotokea watu wachache sana. Tiba yake inaweza ikawa ni supportive zaidi, kama:
1. Ikiwa chanzo chake ni maji ya moto basi oga ya baridi, kama ya baridi tumia maji ya moto na kama shida ni chlorine inayowekwa kwenye maji basi huwa kuna shower gel ya kuondoa chlorine mwisho wa kuoga au utafute purifier ambayo itatoa chlorine. Hapo kwenye chlorine ni issue kubwa.
2. Ikiwa unapata allegy ukigusa tu maji, basi waweza tumia oily cream au gel kupaka mwilini kabla ya kuoga au kuogelea. Hupunguza muwasho kiasi kikubwa.
3. Epuka kukaa muda mrefu ndani ya maji.
4. Nguo za pamba na linen husaidia kupunguza dalili. Tumia taulo lenye pamba asilimia 100.
5. Epuka kutumia vyakula vyenye viungo vingi na vyakula vinavyokaangwa. Pia epuka kunywa pombe na kahawa, maana vitu hivyo vitaongeza tatizo.
6. Muone daktari wa magonjwa ya ngozi.
Ahsante kwa ushauri naomba nichk kwa namba hii ili unielekeze kwa kuipata +258845418066
Pole Sana! Mie tatizo hilo linanikuta hasa nikioga maji ya baridi. Nafuu yangu ninapooga maji ya moto. Kushindana na hali hiyo mara baada ya kuoga huwa navaa jacket zito ili mwili kupata joto haraka. Hospitali zote nilizopita sijapata majibu ya kutatua tatizo wala kuweka hapa. Narudia kukupa pole maana shida hiyo ninaiishi.
Mkuu hii namba ya nchi gani?
Utakuwa na tabia za Mwigulu...
Duh!! Hadi nilikuwa naona aibu kusema!! Yaani hili tatizo limenitesa kwa miaka mingi,nimejaribu dawa kadhaa za hospitali bila mafanikio,ila niligundua njia moja ambayo kidogo inanisaidia,nikioga asubuhi tatizo linakuwa kubwa zaidi,ila nikioga jioni/usiku huwa napata nafuu kidogo,hasa nikioga na kuwahi kujifuta na kuingia kitandani ASAP na kujifunika gubigubi,huwa pia nikiwa katika hali hiyo ya kuwashwa napata kichefuchefu sana,sitki nione kitu chochote kichafu wala sitaki niguswe na kitu nilicho na mashaka nacho,hali hiyo huwa inadumu kwa dakika kumi hadi thelathini!! Ni shida wakuu.
Ahsante kwa ushauri naomba nichk kwa namba hii ili unielekeze kwa kuipata +258845418066
Mkuu hii dawa Oloodwa inapatikana kiurahisi kuliko zingine,sehemu zingine wanaita Ngesi, kwa Arusha mjini nenda soko kuu kule nyuma kbs karibu na wanapouza samaki
Wale wazee wa kimasai wanajua na jinsi ya kutumia,Nafikiri pia maeneo mengine nchini ipo sisi tulikuwa tunapewa toka tukiwa primary...For sure they helped us alot.