Miunda
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 530
- 182
Jamani mimi pia nina hili tatizo, lakini mimi nikioga bila kujisugua na dodoki sipati muwasho wowote yawe maji ya chumvi sijui ya moto au baridi, lakini nikitumia tu dodoki kujisugua sehemu yeyote cha moto nitakipata kwa muda wa dakika tano mpaka pale nitakapo jifuta maji vizuri na kupaka mafuta, mwenye utashi na hili swala anisaidie tafadhali.
Hilo dodoki litakuwa linachuna ngozi yako,tafuta kitu cha kujisugulia soft.
Mimi kuwashwa kwa maji inatokezea tena sana kwa maji ya moto, na ya baridi hayaogeki huku uzunguni, hivyo huweka balance ya maji si moto wala baridi.