Tatizo la LUKU limerudi tena

Tatizo la LUKU limerudi tena

"Tanzania Tanzania, nchi yenye mali nyingi, Watu wengi wa Ulaya wanaililia sana"

Hiyo inaitwa jipiganie wewe mwenyewe wala usitegemee kupiganiwa hata kama rasilimali zitandae hadi mlangoni pako.

Mwenye nacho ataongezewa....[emoji2]

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu wameahidi kuwa manunuzi ya Luku yatarudi kama kawaida?
 
Tanesco mpya imeanza kazi hofu yako ni nini? Tanesco ya akina Kalemani na Tito Mwinuka haina nafasi tena, tutegemee mambo mazuri
 
Ni siku ya pili sasa kuna tatizo kubwa ya Luku. either kwa kununua kwa njia ya mitandao ama kwa wakala wao.... Waziri mpya tulijua umeingia kuongeza kasi kumbe mambo ni yale yale...
Kama kuna shirika gumu kuliongoza nadhani TANESCO inashika namba moja.
 
Samia anaturudisha nyuma sana. Yeye anawaza kuikomesha Chadema mambo ya msingi yana mshinda
 
729BA6F7-44A0-42A8-94F0-1DD3AAE44B21.png
 
Kama kuna shirika gumu kuliongoza nadhani TANESCO inashika namba moja.
Katika manifesto ya Chadema kama sikosei walizungumzia kuligawanya Shirika hilo. Kuwepo na moja la Production ya umeme na lingine la Distribution ya umeme.

Nadhani huo ungekuwa utatuzi mkubwa sana
 
Katika manifesto ya Chadema kama sikosei walizungumzia kuligawanya Shirika hilo. Kuwepo na moja la Production ya umeme na lingine la Distribution ya umeme.
Nadhani huo ungekuwa utatuzi mkubwa sana
Hii ingesaidia sana sababu anayezalisha umeme atakuwa na threshold yake na muuzaji hivyohivyo. Ila hii ya kuliacha lizalishe na kuuza wanabweteka sana
 
Ni siku ya pili sasa kuna tatizo kubwa ya Luku. either kwa kununua kwa njia ya mitandao ama kwa wakala wao.

Waziri mpya tulijua umeingia kuongeza kasi kumbe mambo ni yale yale...
Mbona mimi nimenunua jana via airtel sijaoata tatizo kabisa.
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

Oktoba 04, 2021

TAARIFA YA KUKOSEKANA KWA HUDUMA YA MANUNUZI YA LUKU

Tunawaomba radhi wateja wetu kutokana na hitilafu kwenye mfumo wa manunuzi ya umeme wa LUKU iliyotokea leo Oktoba 04, 2021 na kusababisha wateja kushindwa kununua umeme.

Tayari wataalamu wetu wametambua tatizo na wanafanya kazi kuhakikisha linakwisha.

Huduma itarejea leo saa 9:00 Alasiri, tunaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza.

Kituo cha Miito ya Simu Makao Makuu: +255 222 194 400 na +255 768 985 100

Imetolewa na;
Ofisi ya Uhusiano,
TANESCO MAKAO MAKUU.
 
Back
Top Bottom