Tatizo la Mabaka, Mba na Fungus (Fangasi) sugu na kuwashwa sehemu za siri kwa wanaume na wanawake- Fahamu chanzo, Dalili na Matibabu yake

Tatizo la Mabaka, Mba na Fungus (Fangasi) sugu na kuwashwa sehemu za siri kwa wanaume na wanawake- Fahamu chanzo, Dalili na Matibabu yake

ok fanya hivi...
Huo utakuwa mchanganyiko wa magonjwa mawili au matatu au zaidi. Sivizuri kudhan ni ugonjwa mmoja

1. Nadhan ana bacteria infection kwenye vagina ambao wamechange pH ya vagina
2. Ana fungal infection kwa sababu inawezeka bacteria na fungal zika co exist sababu ya antibiotic resistant bacteria
3. Ana high infection kwenye (cervix, uterus pamoja na adnexia) kizazi ndo maana anapata mucus.
4. Ana systemic fungal infection ndo maana haponi fungas kwa kutumia gynazol pekee.

Afanye hivi
1. Antibiotic Atumie doxycilline, metronidazole pamoja cloxacilline
2. Atumie miconazole pesaries pamoja na miconazole topical ointment
3. Atumie fuluconazole tabs atleast 4 three weeks 150au 200mg bd.
4. Mwisho hzo miconazo za kupaka aka topical apake kwenye mashavu. Uvungu wa makalio wote yan kuanzia nyuma ya sehemu ya aja kubwa mpaka mbele mwisho wa mavuzi.
5. Acha kuvaa chupi na tight za linen tumia za cotton pekee.
Tupe feedback
 
na inakuaje mtu unakua unaskia kama maumvu yan kama mkojo unakuuma uma vle..alaf unatoka ute mzto mweupe lakn cyo mwng?

ok mkojo kukuuma ukikojoa kwenye mashavu ni fungus zinasababisha inflamation then unapata mchubuko ukikojo unapata maumivu mkojo ukigusa mchubuko. Tumia miconazole pesaries na topical miconazole utapona
pole
 
Mkuu Baosita kama nikimeza chenyewe bila kusaga wala kuchanganya na maji vuguvugu itafaa? Manake kikiwa kizima nahisi inakuwa poa kama umebugia peremende vile..!
 
asante kwa tiba mbadala, tupumzike na makemikali pale inapobidi
 
Hii dawa nimeitumia baada ya kupatwa na flue badala ya kunywa coldril kama nilivyozoea. baada ya masaa kadhaa nimejiskia vizuri sana. nashauri kitunguu kizuri sio vile vikubwa vyeupe. ni vyenye punje ndogo na rangi inayoelekea wekundu
 
dah ahsante sana mzee wa baosita, maana hili tatizo ni tropical Neglected disease, (NTD) iliyowekwa pembeni zaidi! usione biashara ya boxer inashamiri hadi za mitumba!!!! fungus noma!!! ila mi niliwahi jaribu kupaka aloe vera kwa fangasi za miguu, zimepona kabisa! kama vipi mtu kama ni chronic apige booster dose...
 
Mkuu samahani kwa kuchelewa napenda kujua vipi kwa mtoto mwenye miaka miwili anaruhusiwa kupewa dawa hii?
 
Habari zenu wadau.Nimeona nitoe elimu hii hapa kwa sababu ni watu wengi sana wanaosumbuliwa na minyoo na fungus sugu kila maeneo kuanzia miguuni mpaka sehemu nyeti!Hii imekuwa kero sana.Haijalishi umezunguka hospitali ngapi bila kupata nafuu.Cha kufanya ni:-

Nunua kitunguu swaumu.Menya chote kama vile uandaavyo kwa ajili ya kupikia.Twanga ama saga,vikishasagika changanya na maji ya uvuguvugu kidogo kipimo cha kijiko cha chai ili vilainike.Chota msagiko wote wa vitunguu na uvimeze.
Tahadhari,jitahidi uwe na mfuko ama sehemu ya maliwatoni maana kama hauna tumbo zuri unaweza tapika.(Mara chache sana hutokea kutapika)

Ukishakaa kama dk 15 hali yako itarudi kawaida.Baada ya SIKU 1,utaona minyoo hakuna tena na fungus wote wamekauka!Kwisha kabisa!!!!

Pia kama una presha ya kushuka usitumie hii dawa maana huwa inashusha sana presha,labda unywe na kahawa baada ya kuinywa dawa hii ili kuipandisha tena presha!

Msisite kuja kutoa ushuhuda wenu hapa wakuu.Ni hayo tu.
Mkuu hii dawa unakunywa kwa mda gani!?
 
Mimi nna fungus kwenye miguu zaidi ya miaka 8 vinatoa vipele vya maji maji vinawasha sana nimetumia dawa kibao zinapona dozi ikiisha nikiacha baada ya muda vinarudi vinawasha balaa ngoja nijaribu mkuu ntaleta ushuhuda hapa sasa sijui baada ya muda vitarudi tena au inakuaje hapo mkuu
 
Mkuu.@Bray Pole sana kwa hayo matatizo yako mimi ninakupa dawa ya Kienyeji ya tiba Mbadala huenda ikakusaidia fanya hivi: Nunua kitunguu swaumu. Menya chote kama vile uandaavyo kwa ajili ya kupikia.Twanga ama saga,vikishasagika changanya na maji ya uvuguvugu kidogo kipimo cha kijiko cha chai ili vilainike.Chota msagiko wote wa vitunguu na uvimeze.
Tahadhari,jitahidi uwe na mfuko ama sehemu ya maliwatoni maana kama hauna tumbo zuri unaweza tapika.(Mara chache sana hutokea kutapika)

Ukishakaa kama dk 15 hali yako itarudi kawaida.Baada ya SIKU 1,utaona minyoo hakuna tena na fungus wote wamekauka!Kwisha kabisa!!!! Tumia kama Siku 3 Mfululizo ikiwa bado hujapona ongeza tena Siku 3 zingine haitafika Siku 7 utakuwa umekwisha pona jaribu kisha uje hapa utpe Feedback.
mkuu unatishaa
 
pole sana na fuata ushauri wa MziziMkavu vitunguu swaumu ni kabambe na ninashauri hata ambao hawaumwi ni bora kutumia hata kwa wiki mara mmoja inasaidia mambo mengi sana
 
Je hata MBA zinapona? kwani zimenisumbua kwa muda mrefu sana, naomba maelezo hapo kwani nikiwa sehemu za joto kama dar ndiyo inakuwa noma afadhali sehemu za baridi kidogo napumzika kupaka dawa za MBA.
 
Mkuu Bray hii dawa ni ya Kienyeji kwa sababu umeumwa miaka mingi na umetumia dawa nyingi hujapona ninakushauri utumie Dawa mpaka upone ninafikiri kwa nguvu ya kitunguu samu huwezi hata kufikisha siku 15 utakuwa umeshapona jaribu kisha uje hapa kueleza je umepona au bado? Give Me feedback.

Faida za Kiafya za Kitunguu Swaumu (Garlic) Featured

1%20garlic%20.jpg


Kitunguu swaumu ni jamii ya vitunguu ambayo kwa kitaalamu huitwa Allium sativum. Jamii hii ilianza kutumika katika mabara mbalimbali duniani hususani Asia, Afrika na Ulaya takribani miaka 6000 iliyopita. Matumizi makuu nyakati hizo yakiwa viungo katika mboga na tiba.


Kitunguu swaumu kimetajwa kwenye vitabu mbalimbali vya dini vikielezea faida zake katika kutibu maradhi mbalimbali yasababishwayo na bakteria, matatizo katika mapafu, matatizo katika mfumo wa umen'genyaji chakula, na matatizo ya kuishiwa nguvu.


Historia inaonesha kuwa, vitunguu swaumu vilianza kutumika China mwaka 510 K.K na pia vilitumiwa na wanajeshi wa Ugiriki na Roma. Aidha wasafiri wa vyombo vya baharini na vijijini pamoja na wakulima barani Afrika walivitumia sana.


Mwaka 1858, mtafiti na mwanasayansi wa nyakati hizo, Louis Pasteur aligundua uwezo wa kitunguu swaumu katika kuua vimelea mbalimbali vinavyosababisha magonjwa, na hivyo vikaanza kutumika kama dawa ya kusafishia vidonda na kuzuia kidonda ndugu hasa zama za vita ya kwanza na pili ya dunia. Isitoshe, mpaka sasa zipo dawa kadhaa zilizotengenewa kwa kutumia jamii hii ya vitunguu swaumu ikiwemo dawa ya kusafisha mdomo (mouth wash) ingawa watumaiji wake wengi huilalamikia dawa hiyo kwa sababu ya harufu mbaya ya dawa hiyo inayowasababishia kunuka kwa mdomo.


Faida za vitunguu swaumu


Katika tafiti mbalimbali vitunguu swaumu vimeonekana kuwa na uwezo wa kutibu maambukizi ya bakteria, fangasi na virusi vya aina mbalimbali. Aidha husaidia kuzuia magonjwa ya moyo ikiwemo kuondoa lijamu katika mishipa ya damu na hivyo kusaidia katika kurekebisha shinikizo la damu. Faida nyingine za vitunguu swaumu ni pamoja na
  • Kutibu saratani ikiwemo saratani ya tumbo na utumbo mkubwa. Tafiti zinaonesha idadi ndogo ya wagonjwa wa saratani katika nchi ambazo wakazi wake wana utamaduni wa kutumia vitunguu swaumu kwa wingi.
  • Vitunguu swaumu husaidia kudhibiti kiwango cha sukari katika damu. Hata hivyo inashauriwa kwamba wagonjwa wa kisukari wanaotumia sindano za insulin wasitumie kitunguu swaumu kwa wingi mpaka watakaposhauriwa na daktari.
  • Huzuia kusanyiko la chembe sahani zinazosaidia kuganda kwa damu (platelet aggregation)
  • Husaidia ufyozwaji wa thiamin, hivyo kusaidia kuepusha mwili na ugonjwa wa beriberi
  • Ina kiasi kikubwa cha vitamini C ambayo husaidia kuzuia ugonjwa wa kiseyeye
  • Hutumika kutibu magonjwa nyemelezi kama toxoplasmosis, hasa kwa watu wenye upungufu wa kinga mwilini.

Ushahidi wa Kitafiti


Katika utafiti uliofanyika nchini Czech ilionekana kuwa matumizi ya vitunguu swaumu yalisaidia sana katika kupunguza kusanyiko la lijamu (cholesterol) pamoja na mafuta yasiyofaa mwilini (low density

lipoproteins)
katika mishipa ya damu. Aidha, mwaka 2007 BBC iliripoti matumizi ya vitunguu swaumu katika kusaidia kumkinga mtumiaji dhidi ya aina fulani ya mafua iliyosababishwa na virusi. Mwaka 2010,

ulifanyika utafiti mwingine ambao ulijumuisha wagonjwa 50 wenye shinikizo la damu sugu ambalo lilikuwa ni vigumu kudhibitiwa hata kwa matibabu yaliyozoeleka ya dawa na njia nyingine. Kama njia ya

kuchunguza ufanisi wa vitunguu swaumu katika kutibu shinikizo la damu, baadhi ya wagonjwa hao walipewa vitunguu swaumu wakati wengine walipewa dawa isiyohusika na matibabu ya shinikizo la damu

(au placebo). Ilionekana kuwa wale waliopewa vitunguu swaumu kama dawa ya shinikizo la damu walionesha maendeleo mazuri kwa vitunguu swaumu kuweza kushusha vizuri kiwango cha shinikizo la damu, hususani systolic pressure, tofauti na wale waliopewa placebo.


Nini siri ya kitunguu swaumu?


2%20garlic.jpg




Sifa kuu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa na uwezo na faida zilizoainishwa hapo juu ni kule kuwa kwake na viasili kadhaa (ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti. Uwezo wake wa kiutendaji unatokana na mambo yafuatayo;
  • Vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides kwenye seli nyekundu za damu.
  • Husaidia uthibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine na kupunguza madhara ya kisukari.
  • Iwapo vitapondwa pondwa vizuri, vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo Allicin ambayo ni dawa dhidi ya bateria, na phytoncide ambayo huua fangasi wa aina mbalimbali.
  • Harufu mbaya ya kitunguuu swaumu hutokana na gesi aina ya hydrogen sulfide ambayo inayotolewa baada ya kuvila.

Mzizi naomba unidumbukizie chemba ya private huu utirio if you don't mind
 
Back
Top Bottom