Tatizo la Mabaka, Mba na Fungus (Fangasi) sugu na kuwashwa sehemu za siri kwa wanaume na wanawake- Fahamu chanzo, Dalili na Matibabu yake

[h=2]Dawa kiboko ya minyoo na fungus sugu (home made)!![/h]
Habari zenu wadau.Nimeona nitoe elimu hii hapa kwa sababu ni watu wengi sana wanaosumbuliwa na minyoo na fungus sugu kila maeneo kuanzia miguuni mpaka sehemu nyeti!Hii imekuwa kero sana.Haijalishi umezunguka hospitali ngapi bila kupata nafuu.Cha kufanya ni:-

Nunua kitunguu swaumu.Menya chote kama vile uandaavyo kwa ajili ya kupikia.Twanga ama saga,vikishasagika changanya na maji ya uvuguvugu kidogo kipimo cha kijiko cha chai ili vilainike.Chota msagiko wote wa vitunguu na uvimeze.
Tahadhari,jitahidi uwe na mfuko ama sehemu ya maliwatoni maana kama hauna tumbo zuri unaweza tapika.(Mara chache sana hutokea kutapika)

Ukishakaa kama dk 15 hali yako itarudi kawaida.Baada ya SIKU 1,utaona minyoo hakuna tena na fungus wote wamekauka!Kwisha kabisa!!!!

Pia kama una presha ya kushuka usitumie hii dawa maana huwa inashusha sana presha,labda unywe na kahawa baada ya kuinywa dawa hii ili kuipandisha tena presha!

Msisite kuja kutoa ushuhuda wenu hapa wakuu.Ni hayo tu.

chanzo. https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/346213-dawa-kiboko-ya-minyoo-na-fungus-sugu-home-made.html
 
Kuna dawa nimeitumia nimepona ugonjwa wa mba wa kichwani, rafiki aliniambia nikakununue dawa inayoitwa kibiriti upele. ile dawa inauzwa kwenye maduka ya dawa za kiswahili ni ya ungaunga na kama ya njano hivi ikiwa kwenye kifuko cha plastiki. Nikaiweka kwenye chupa ndogo ya maji ya uhai na kuichanganya na mafuta ya nazi... basi nikawa napaka kichwani kila ninaponyoa kipara.
Lakini rafiki yangu aliniambia inatibu hata fangasi wa kwenye pachipachi za mapaja na kwenye vidole vya miguuni. Nimeitumia kwa kweli imenisaidia sana... na kuna watu wengi nimewapa na wamesema imewasaidia sana... huwezi kuamini inauzwa shilingi mia tano mpaka buku.
 
Tatizo Wabongo tunadharau vyetu kwani kiasi kikubwa Madawa KARIBU yote ni matokeo ya utafiti wa Haya Haya tunayoyadharau. Tatizo kubwa ni Biashara na Ajira inayolipa wakati ni usiri MTUPU. AHSANTENI mliotoa matibabu bure!!!!
 
paka spirit inatosha
 


Mkuu kwa Dar es salaam naweza kupata wapi exactly hiyo dawa? Maana nahisi mimi ni too much mpaka kucha za miguuni zinaathiriwa na hawa fangas sugu. Kama unacontacts za hao wauzaji naomba unisaidie kama hautajari mkuu.
 
Wadau nina tatizo la fungus kwenye ngozi ya mwili, usoni kwenye ngozi chini ya macho, kwenye miguu na sehemu za paja! Naomba msaada tafadhali nifanyeje
 
Dah pole sana, ikiwa unatumia antbiotics sana punguza, ni mojawapo ya visababishi vya hayo maneno
 
Wadau nina tatizo la fungus kwenye ngozi ya mwili, usoni kwenye ngozi chini ya macho, kwenye miguu na sehemu za paja! Naomba msaada tafadhali nifanyeje

umejuaje kuwa ni fungus? we tuambie nini kinaonekana na kinasumbuaje?
 
Mkuu kwa Dar es salaam naweza kupata wapi exactly hiyo dawa? Maana nahisi mimi ni too much mpaka kucha za miguuni zinaathiriwa na hawa fangas sugu. Kama unacontacts za hao wauzaji naomba unisaidie kama hautajari mkuu.
Kuna maduka yanaitwa ya asili yapo mengi sana Kariakoo.
 
Wadau naombeni msaada ninatatizo la fugus zaidi ya miaka 12 sasa iliyopo chini ya ngozi za kende zangu na mpaka mapajani inawasha sana mpaka inafika kipindi najikuna natoja na vidondo na kuna mda vinakauka na kuacha magamba na maumivu makali nimejalibu vidongo wapi dawa za tube kupakaa wapi sasa naombeni msada wadau niaibu kwa shem wenu naona so kweli....
 
Kuna dawa inaitwa LIFE inatangazwa sana kwenye Star TV nunua na ufuate masharti yaliyoandikwa. naamini dawa hii itakusaidia sana.
 
Nenda kwa specialist wa magonjwa ya ngozi,a mpenzio nae atibu fungus,muanze upya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…