naomba kujua hivi kunauhusiano wa kiasi gani kati ya kuharibika kwa mimba na fangas sehemu za ukeni, je fangas zaweza kuwa sababu ya mimba kuharibika, kama jibu ni ndio kwa kiasi gani, kama sio je kuna sababu nyingine zinazo weza kufanya mimba ikaharibika pindi ikiwa bado changa?
pole sana, ukeni kuna vijidudu ambavyo vinalinda usipate shida na hawa wanaitwa normal flora, meaning tunaishi nao ndani ya miili yetu na ni faida kuwa nao kwani ni sehemu ya kinga, vijididi hivi lactobacilus, wanaoosha ukeni sana mara na sabuni na nini, ama mapoko ya kushare in toilets, huondoa hawa vijidudu na hivyo ndivyo fungus hutokea. wakati wa ujauzito wakina mama wengi hupata fungus na huwa inatibiwa kwa dawa ya kuweka tu, hii ni kwa sababu ya mabadiliko katika uke kipindi cha ujauzito, ile acidic enviroment inayoekwa na hawa lactobacilli inapungua na kuwa alkaline inayoruhusu fungus kuishi. dalili zake ni kuwashwa ukeni, kutoka uchafu unaofanana na maziwa mgando, cudmilk like discharge.
fungus haichangii kuharibika kwa mimba.
sababu zanazosababisha mimba changa kuharibika ni:
kuwa una uvimbe ndani ya kizazi utakaoshindwa kuruhusu mimba kukua,
maambukizi ya magonjwa ya zinaa,
mama kuugua kama severa malaria na Tick born relapsing fever
kutumia dawa kama quinine wakati mwingine husababisha hili.
chromosomal abnormality kwa mimba iliyotungwa pia husababisha ikatoka, meaning chembe chembe zinazotengeneza mtoto kuwa na kasoro
luteo phase deficiency, ina maana hormone inayosaidia ujauzito kukua which is progesteerone wakati mwingine hupungua na kusababisha mimba kuharibika
pia research have shown that up to 78% of abortions cause can not be found however these people have chances of having successful futute pregnancies.
however, Tanzania bado hatujaweza kufanya mambo ya chromosomal checking including genetics hivyo nikushauri ukapimwe na dakatari atakapobaini tatizo atakutibu upasavyo.