MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,675
- 33,583
Ndugu zangu Watanzania,
Kuna sehemu tulikosea, tunakosea na tutaendelea kukosea. Wimbo wa Machinga kufanya biashara maeneo yasiyo rasmi kama yupo anayefikiri ni wimbo wa juzi basi ana upungufu wa akili. Nani hapa ambaye anaweza kukataa kuwa kwa mfano mitaa ya Kongo ilivyo leo pako hivyo miaka mingi mno na hakuna kilichobadilika zaidi ya majengo mapya?
Serikali za awamu zote zilikuja na njia mbalimbali ambazo zingine ziliishia kuchoma fedha ambazo hazikutoa matunda yoyote ikiwemo Machinga complex kule Karume. Hivi pamoja na wastani wa wasomi nchi hii kupanda sana hadi leo tunapambana na machinga badala ya kupambana na kile kinachozalisha machinga? Mnataka kuleta usafi,mpangilio wa nchi zingine kwa muonekano wao wa nje bila kuja na takwimu za namna walivyoweza kuacha maeneo yao ya katikati ya jiji bila machinga! Tuleteeni ushahidi ufuatao ili tujue hayo madesa ya kusifia nchi za wenzetu ni sahihi kuyatumia hapa;
1) Ushahidi jinsi walivyokuwa na tatizo la machinga kama letu
2) Kama walitatua kwa kuwatimua maeneo yao, au ...
3) Namna walivyoendesha zoezi la kuhamisha machinga kwa namna yenye mfanano na Kariakoo
Pamoja na Rais wa awamu iliyopita kuwa Mkali mno lakini swala la machinga alijua hana suluhisho la kweli na serikali haina mkakati wa maana akaona hakuna haja ya "kuliamsha dude" ambalo hana suluhisho na mbaya zaidi kitu kinachogusa maisha ya watu. Hivi ni nani anapenda kukaa kwenye lile jua la Kariakoo?, Hivi nani anapenda kukaa kwenye zile barabara pengine na mtoto huku gari zikigusa makalio yako? Tusicheze na maisha ya watu kama hatujajipanga! Tunasikiliza watu ambao wana njia za kujipatia kipato na mbaya zaidi kelele zao ni kubwa kuliko wanyonge hawa ambao kelele zao za manunguniko zitaishia kwenye kuta za nyumba zao!
Hakuna serikali ya awamu yoyote imewahi kufanikiwa kwenye hili zoezi la machinga. Naomba sana viongozi wetu tutafute namna ya kutatua tatizo hili kwa hekima. Kweli Kariakoo ni tatizo kubwa lakini si la jana wala juzi hatuwezi kulitatua kwa short cut. Wale ni mama zetu, dada zetu, Kaka na baba zetu wanaohangaika tena kwa mahitaji ya chini sana pengine familia ipate ugali tu. Ile Kariakoo ndio centre ya biashara kubwa kwenye ukanda wetu huu na muingiliano ni mkubwa, ule muingiliano ndio unaovutia machinga pia kujipatia riziki.
Swala la Machinga si la kuamka na kutangaza waondoke maeneo ya Kariakoo, Ile Kariakoo ilivyo hakuna sehemu Machinga atastahili kuwepo HAKUNA! Hao wachuuzi si wa kupanga mafremu, Hao wanaenda penye watu! Hao wenye maduka pia ndio wanawapa bidhaa wakasaidie kuuza. Ni mfumo wa biashara ambazo haufutiki kwa kuwafukuza tu, ni utaratibu ambao kwa kushirikiana nao hao wamachinga tunapaswa KUWAELEWA na kutafuta suluhisho la kudumu.
Mungu atusaidie hekima, busara za viongozi ziwaongoze kusitisha zoezi la kuwaondoa wale wamachinga na kujiuliza why walifeli awamu zote na nini kipya kifanyike.
"Our life of poverty is as necessary as the work itself. Only in heaven will we see how much we owe to the poor for helping us to love God better because of them" Mother Teresa