Tatizo la Manchester United ni nini haswa?

Tatizo la Manchester United ni nini haswa?

Timu ambayo haitaki kusajili wachezaji wa maana wameweka Uingereza mbele kwa kuwanunua bei ghali bila sababu yaani Utd ndo ya kulipa mileha kibao kwa Mount halafu unasubiria wachezaji wa mikopo timu iendee sasa ni bora liende bila mgomo wa mashabiki haitoboi
Hivi kweli Mount alicheza kweli? Mbona hakuonekana kabisa ndo kipaji kinakufa hivo.
 
Kuna moja kati ya mashabiki wa Manchester United aliniambia maendeleo mabovu ya Man UTD yanatokana na uongozi mbaya wa mmiliki wa timu ambao ni familia ya Glazer (yenye makazi yake England). Mmiliki wa klabu ameridhika kuwa klabu yenye mauzo makubwa ya jezi lakini ameamua kutoipambania timu.

Kocha wa Man UTD yupo kama boksi lakini linapokuja suala la usajili hata akitaka kumnunua mchezaji fulani analetewa mwingine. Timu ni kama inajiendesha, hadi Carlos Casimiro ananukuliwa na magazeti mengi ya England akitoa lawama kwa timu hasa hasa kwa wamiliki na menejimenti.
Kweli kwa makocha waliopita LVG, Mou, Ole etc. Ila huyu wa sasa wachezaji karibia wote kasajili mwenyewe.
 
Usajili mbaya

Antony
Amrabat
Hodjullund
Evans
Hizo zote hapo juu ☝️ Ni taka taka
 
Toka enzi za furgason bado wana usajili wa kudunduliza wanasahau Alex alikuwa ni kocha bora na siraha kubwa ni muunganiko mzuri wa timu na mastaa wengi nyota yao kung'aa ilianzia ndani ya timu.Sasa hivi makocha uwezo mdogo na bado usajili ni wa kuchungulia hela.
 
Man u jana ni kama team ya watoto wakicheza na wakubwa zao, kwa mara ya kwanza niaamua tu nishike simu nijisomee habari za dunia maana hawakuonesha kitu katika kupigania team. Unaweza kuwa usiwe na wachezaji bora lakini ile jinsi ya kujituma hakuna kabisa. Ukitaka kujuwa ubovu wa Man u, hakuna hata mchezaji mmoja anaweza kupata number Man city, Arsenal, Liverpool, Spurs labda moja au wawili Newcastle. Huu ndio ubovu wa Man u. Ila pamoja na kuwa na wachezaji sio wazuri walitakiwa kucheza kama team ndogo yenye jihad ya uwanjani.
 
Hata msemeje! hata mfukuze kocha mlete carlo Ancelotti na Guardiola ni kwamba wachezaji wa pale kwa ukubwa wa timu hawastahili hata timu ya chelsea.

Ukileta kocha mkubwa lazima atawatimua karibia asilimia 90% ,hao madogo wengi uwezo ni mdogo na wanasajiliwa plus kulipwa pesa ndefu ila sio wapambanaji.
 
Laaana
Hivi karibuni kumekuwa na hali ya kukera inayotokana na Manchester United kupoteza kwa mfululizo na malalamiko kutoka kwa wachezaji ambayo yamekithiri.

Kiundani sababu ya Manchester United kuwa hivi ni nini? Ni coach? Management? Sera? Wamiliki? Au ushindani wa EPL umekuwa mkubwa?

UPDATES:
Katika msimu huu wa mwaka 2023/24 Manchester United imecheza mechi 10 na kushinda mechi 5 tu na kupoteza mechi 5 zote.

Manchester ipo katika nafasi ya nane kati ya timu 20 zinazoshiriki ligi kuu ya English Premier League (EPL).

english premier league table
View attachment 2797739
 
Back
Top Bottom