Tatizo la miguu kuuma

Tatizo la miguu kuuma

Habari zenu Naombeni msaada ndugu zangu Nina tatizo la miguu kuuma kwenye visigino
Nikikaa muda mfupi bila kutembea nikiinuka tuu nianze kutembea miguu inauma sana nashindwa kukanyaga chini pia nikikaa kwenye sehemu inayohitaji nining'inize miguu nikiishusha chini ili nitembee inauma sana
Kwaanae fahamu tatizo hili na tiba yake anisaidie tafadhali nateseka sana
Asante
Tembea 10 km kila siku utakuja kunishukuru
 
Jikande mara kwa mara kwa barafu, ikiwezekana ufanyiwe masaji ya miguu na mbobezi
 
Habari zenu Naombeni msaada ndugu zangu Nina tatizo la miguu kuuma kwenye visigino
Nikikaa muda mfupi bila kutembea nikiinuka tuu nianze kutembea miguu inauma sana nashindwa kukanyaga chini pia nikikaa kwenye sehemu inayohitaji nining'inize miguu nikiishusha chini ili nitembee inauma sana
Kwaanae fahamu tatizo hili na tiba yake anisaidie tafadhali nateseka sana
Asante


Pole sana.

Maumivu kwenye visigino husababishwa na vitu vingi mfano shida kwenye misuli au mifupa ya visigino. Mfano kwenye mifupa ya visigino kuna mfupa wa kisigino, (calcaneus) huvimba na kuchongoka hivyo kusababisha maumivu kama vichomi kwenye visigino hasa unapotembea/kukanyaga. (Calcaneal spurs).

Kwa hiyo ni muhimu ukafika hospital uonane na daktari ili akufanyie uchunguzi na vipimo ili kuweza kubaini tatizo linalokusumbua na hatimaye kupatiwa matibabu sahihi.

Kila la kheri.
 
Sababu ya tatizo inaweza ikawa ni nini
inaweza kusababishwa na;-
  • uzito wako​
  • majimaji/ute kwenye kiungo cha mguu kukauka​
  • kuvaa viatu vinavyobana​
  • kuvaa viatu virefu​
  • Aina ya miondoko yako​
  • kujeruiwa mguu​
  • kama ni mtu wa kukimbia mara kwa mara​
 
Maumivu hapo kwenye visigino tuu pia si wakati wote ni ule wakati wa kutembea tuu nachechemea pia mimi sio mnene sana Nina kilo 82
Okay japo ni changamoto kujua tatizo la mtu bila kumuona au bila vipimo, ila kwa maelezo yako kuna uwezekano ukawa na calcaneal spur, ambapo kifupa huota kwenye mfupa wa kisigino kimakosa.

Nitaambatanisha na picha

images (5).jpeg


Nimekuuliza kuhusu uzito wako coz mara nyingi shida hii huwatokea watu wanene au walio na uzito kupitiliza, sababu uzito kikawaida huelekea chini na kwa bahati mbaya kwenye sakafu ya mguu, mfupa wa kisigino ndio uko prominent zaidi.. hivyo msuguano kati ya kisigino na ardhi (stress) ndio unapelekea inflammatory process na matokeo yake kuzalisha hiko kifupa.

Hivyo, cha kwanza itakubidi ufike hospitali. Utafanyiwa x-ray na vipimo vingine vya maabara.

Ila ni muhimu kujiepusha kukanyagia sakafu kwa mguu peku (bear foot), hivyo unashauriwa upendelee kuvaa yebo au open shoes zenye sakafu laini muda wote.

Upunguze uzito.

Dawa za steroids na antipain zinaweza kutumika kutibu tatizo kama size ya kifupa ni ndogo.

Mwisho kabisa, upasuaji mdogo unaweza kufanyika kusawazisha hiyo bone outgrowth.
 
Utakuwa unapoteza sana wazungu, punguza hili zoezi utakaa sawa
Sahihi kabisa na mawazo yangu nami nimewahi kuhisi hili ni tatizo, Hapo nyuma, ilikuwa napenda sana burudani hiyo, nilikuwa napenda kwichi kwichi kuliko kula.. Vingine havielezeki, ila sasa matokeo nayaona sasa hivi.
 
Unatatizo la nervous system kwa kuwa kwenye nyayo ndio Kuna ncha/mwisho wa nervous basi panapokua na hitilafu huanza kuuma maeneo hayo ili kukupa wakeup call. Hivyo weza kutibiwa eneo la ubongo ambapo ndio eneo Mama lakuzalisha umeme pili tutaenda eneo lingine ambalo ni MUHIMU bàada yakupata MAELEZO mengine, kwa msaada unaweza ni pm nikusaidie au waweza kwenda hospital iliyokaribu Yako (Nb: Mm n herbalist)
 
Back
Top Bottom