Tatizo la miguu kuwaka moto (neuropathy): Ushauri, Kinga na Tiba

Tatizo la miguu kuwaka moto (neuropathy): Ushauri, Kinga na Tiba

Kuna tiba moja niliwahi kuisoma mtandani ikielekeza namna ya kutibu tatizo la miguu kuwaka moto na kupata ganzi. Kulikuwa na tiba mbadala mbili lakini mimi nakumbuka moja ambayo ni kama ifuatavyo....

Tafuta chumvi ya mawe(sio ya unga), chemsha maji kwenye chumbo cha chuma mfamo karai(usitumie chombo cha plastiki) baada ya hapo weka chumvi yako ya mawe kisha loweka miguu yako kwenye maji ya vuguvugu kwa dakika kadhaa kisha toa. Fanya hivyo mara kwa mara na tatizo lako litakwisha.
 
Wakuu wa nchi kama Kuna mtu anasumbuliwa na miguu kuwaka moto please tuwasiliane Ninajua dawa ya kuwasaidia ,

nilikuwa na tatizo la miguu kuwaka moto Kwa miaka 4 kwa kweli nilitumia si dawa za hospitalini na za miti shamba kama debe mbili za unga bila nafuu ,

baadaye nikaja bahatika kupata dawa aina mbili za hospitalini ambazo nilitumia na kupona kabisa

.Hata kuna mwana JF nilimpatia dawa na akaja kutoa ushuhuda hapa JF . User I D ni nyamagala na amepona kabisa .

Kama uko Arusha , Manyara au Moshi tunaweza kukutana Arusha Tanzania, unaweza kuniachia number ya simu Au inbox me please. Have a good night you guys🙂
 
Kwanza nitangulize shukran kwa uzi huu,kifupi nina shida hii,
naomba malekezo yako tafadhari.
 
Wanajamvi habarini za leo

Mimi tatizo langu nasumbuliwa sana na miguu chininya nyao wakati mwingine inawasha washa,nwakati mwingine inachoma choma na kunacwakati inawaka moto, usiku silali kabisa

nimeenda hospitali jimepewa dawa mbali mbali bila mafanikio, nimejaribu dawa za kimasai bado tatizo likompale pale, nimejaribu dawa za kisuni lakini wapi.
Ombi langu kwenu kwa yeyoyote anayejua tiba ya

ugonjwa huu anisaidie karibu mwezi wa pili sasa nateseka. Asanteni nawasilisha.
TATIZO LA MIGUU KUWAKA MOTO NA MIGUU KUFA GANZI

Katika mwili wa binadamu, kuna tatizo la kiafya ambalo huambatana na dalili za mtu kuhisi maumivu, kuhisi kuwaka moto na kufa ganzi kwa viungo vya pembezoni mwa mwili

yaani miguu na mikono. Tatizo hili kitaalamu hujulikana kwa jina la Peripheral Neuropathy.
Matatizo haya ya kiafya (miguu/mikono kuhisi ganzi, baridi au maumivu) husababishwa na kuumia au kudhoofika kwa neva za pembezoni mwa mwili (miguuni au mikononi) na

hivyo kupotea kwa uwezo wa kufanya kazi wa neva katika sehemu husika, miguuni au mikononi.

Dalili zinazoambatana na ugonjwa huu ni hizi zifuatazo

1.Mtu kuhisi ganzi

2. kushindwa kushika au kunyanyua kitu, kuchoka kwa misuli na kadhalika.

3.maumivu au kuwaka moto maeneo ya miguuni/mikononi,
Miongoni mwa mambo ambayo hupelekea neva hizi za pembezoni kudhoofika na kushindwa kufanya kazi vizuri ni haya yafuatayo:

1.Kupungua kwa virutubisho mwilini,hasa mkusanyiko wa vitamini B, (Vitamin B Complex).

2.Matumizi ya dawa, mfano dawa za kutibu kifua kikuu au za kupambana na virusi vya ukimwi

3.Uzito mkubwa wa mwili,

4.Ugonjwa wa kisukari,(diabetic polyneuropathy).

5.Shinikizo la damu,

6. Maradhi ya Figo kutofanya kazi vizuri.

Nina kuuliza Swali je una uzito wa mwili kilo ngapi? Una miaka mingapi? umeowa au umeolewa?

Unao ugonjwa wa kisukari? unao ugonjwa wa Maradhi ya Presha? Kapime huenda una Ukosefu wa Kupungua kwa virutubisho Mwilini? Na ukapime Figo lako je linafanya kazi sawa? Ukifuata ushauri wa wenzangu ikiw abado hujapona unaweza kunitafuta mimi nipate kukutibia upate kupona.Ukihitaji matibabu toka kwangu

burning -feet.png
 
Dalili kama za Gaut, kwan hujazoea kutumia nyama za mbuz mara kwa mara.
 
Habarini.
Mshana Jr na Mzizi mkavu na wataalamu wengine humu ndani naombeni msaada.
Miguu yangu inanisumbua sana, inakuwa kama inaganzi wakati mwingine kama inawaka moto nikienda hospitalini napimwa naambiwa naumwa U.T.I natumia dawa lakini bado.
Sijui tatizo nini, naombeni msaada tafadhali
Umri tena huo mama yangu, ila ngoja wataalamu waje.
 
ahahaha eti umri du, kuhusu UTI aache kujisaidia ovyo kwenye public toilet na pasafishe fresh kule uvunguni if posible kuhusu miguu ngoja waje wataalam mzizi mkavu na mshana
Mbona siwaoni hawa watu
 
Habarini.
Mshana Jr na Mzizi mkavu na wataalamu wengine humu ndani naombeni msaada.
Miguu yangu inanisumbua sana, inakuwa kama inaganzi wakati mwingine kama inawaka moto nikienda hospitalini napimwa naambiwa naumwa U.T.I natumia dawa lakini bado.
Sijui tatizo nini, naombeni msaada tafadhali
Hudhuria kanisa la kilokole...
tatizo lako litakwisha..ovaaa
 
Habarini.
mshana jr na MziziMkavu na wataalamu wengine humu ndani naombeni msaada.
Miguu yangu inanisumbua sana, inakuwa kama inaganzi wakati mwingine kama inawaka moto nikienda hospitalini napimwa naambiwa naumwa U.T.I natumia dawa lakini bado.
Sijui tatizo nini, naombeni msaada tafadhali

mshana jr MziziMkavu mnaitwa huku kuna watu wanahitaji msada wazee
Tumia tiba hii ya kitunguu saumu na ndimu loweka miguu kwenye beseni la maji vuguvugu yenye mchanganyiko wa kitunguu saumu kilichopondwa na ndimu iliyokamuliwa
 
Wanaojua tupen elim maana ndugu yangu nae anasumbuliwa, akilala akiamuka miguu inauma sana,
 
Back
Top Bottom