Wanajamvi habarini za leo
Mimi tatizo langu nasumbuliwa sana na miguu chininya nyao wakati mwingine inawasha washa,nwakati mwingine inachoma choma na kunacwakati inawaka moto, usiku silali kabisa
nimeenda hospitali jimepewa dawa mbali mbali bila mafanikio, nimejaribu dawa za kimasai bado tatizo likompale pale, nimejaribu dawa za kisuni lakini wapi.
Ombi langu kwenu kwa yeyoyote anayejua tiba ya
ugonjwa huu anisaidie karibu mwezi wa pili sasa nateseka. Asanteni nawasilisha.
TATIZO LA MIGUU KUWAKA MOTO NA MIGUU KUFA GANZI
Katika mwili wa binadamu, kuna tatizo la kiafya ambalo huambatana na dalili za mtu kuhisi maumivu, kuhisi kuwaka moto na kufa ganzi kwa viungo vya pembezoni mwa mwili
yaani miguu na mikono. Tatizo hili kitaalamu hujulikana kwa jina la Peripheral Neuropathy.
Matatizo haya ya kiafya (miguu/mikono kuhisi ganzi, baridi au maumivu) husababishwa na kuumia au kudhoofika kwa neva za pembezoni mwa mwili (miguuni au mikononi) na
hivyo kupotea kwa uwezo wa kufanya kazi wa neva katika sehemu husika, miguuni au mikononi.
Dalili zinazoambatana na ugonjwa huu ni hizi zifuatazo
1.Mtu kuhisi ganzi
2. kushindwa kushika au kunyanyua kitu, kuchoka kwa misuli na kadhalika.
3.maumivu au kuwaka moto maeneo ya miguuni/mikononi,
Miongoni mwa mambo ambayo hupelekea neva hizi za pembezoni kudhoofika na kushindwa kufanya kazi vizuri ni haya yafuatayo:
1.Kupungua kwa virutubisho mwilini,hasa mkusanyiko wa
vitamini B, (Vitamin B Complex).
2.Matumizi ya dawa, mfano dawa za kutibu kifua kikuu au za kupambana na virusi vya ukimwi
3.Uzito mkubwa wa mwili,
4.Ugonjwa wa kisukari,
(diabetic polyneuropathy).
5.Shinikizo la damu,
6. Maradhi ya Figo kutofanya kazi vizuri.
Nina kuuliza Swali je una uzito wa mwili kilo ngapi? Una miaka mingapi? umeowa au umeolewa?
Unao ugonjwa wa kisukari? unao ugonjwa wa Maradhi ya Presha? Kapime huenda una Ukosefu wa Kupungua kwa virutubisho Mwilini? Na ukapime Figo lako je linafanya kazi sawa? Ukifuata ushauri wa wenzangu ikiw abado hujapona unaweza kunitafuta mimi nipate kukutibia upate kupona.Ukihitaji matibabu toka kwangu