Mada hili inahusu matatizo ya Miguu kuwaka moto na namna ya kukabiliana nayo.
Maswali...
Nimekuwa na tatizo la miguu yote miwili kuwaka moto sana, hata kutembea nashindwa kukanyaga chini vizuri.
Nina umri wa miaka 38 na uzito wa 98Kg.Sijaugua ugonjwa mwingine zaidi ya malaria ya kawaida kwa mwaka mara mbili au moja.
Kwa ufupi sina mazoezi yoyote ya viungo nifanyayo.Sasa natembelea fimbo kama mlemavu.
WanaJF, Niangalizieni hili na kama kuna mtaalamu wa viungo humu basi anipe ushauri ni mazoezi gani nifanye kupunguza uzito.
MIGUU KUWAKA MOTO
Hisia za kuwaka moto kwa miguu yako zinaweza kusababishwa na
uharibifu wa mishipa ya fahamu ya kwenye miguu, jina la kitaalamu tunaita
Neuropatahy.
Ingawa matatizo mengi ya kiafya yanaweza kusababisha
miguu kuwaka moto, ugonjwa wa
kisukari unashikilia usukani.
Sababu nyingine ni unywaji wa pombe kupita kiasi.
Na sababu nyingine nyingi ni hizi zifuatazo;
-magonjwa sugu ya figo
-upungufu wa vitamini B12, folate, na vitamin B6
-kiasi kidogo cha homoni ya tezi dundumio/tezi shingo(thyroid hormone)
-Virusi vya UKIMWI na UKIMWI
-ugonjwa wa lyme
-ugonjwa amyloid polyneuropathy
-maudhi madogo madogo ya dawa au kwa jina la kitaalam tunaita drug side effects ambapo ni pamoja na dwa za magonjwa ya kansa, kuzidisha dozi ya vitamin B6 au dawa za virusi vya UKIMWI
-ugonjwa wa erythromelgia
-sumu za metali nzito kama mekyuri, na arsenic
-majeraha kwenye mishipa ya damu
-ugonjwa wa sarcoidosis
-ugonjwa wa guillain-barre syndrome(GBS)
Matibabu mengi ya tatizo hili yanalenga kuzuia uharibifu zaidi wa mishipa ya fahamu na kupunguza maumivu.