Tatizo la miguu kuwaka moto (neuropathy): Ushauri, Kinga na Tiba

Tatizo la miguu kuwaka moto (neuropathy): Ushauri, Kinga na Tiba

Body mass index yangu ni 36,Nahitaji kujua pia ni aina gani ya mazoezi nahitaji kufanya,Kwani physician wamenishauri nisianze mazoezi makali kwanza.Nimewaona wataalam mbali mbali na dawa nimetumia lakini nafuu haipo kabisa.
BMI Yako tu inaonesha uzito ulionao Ni mkubwa hauendani na urefu wako. Ntafte kwa message private nikuelekeze namna ya kupungua uzito kiafya.
 
Aisee kwenu wataalam wa afya nina tatizo la kufa ganzi vidole vya mikono mara nyingi asubuh nikitoka kuamka najikuta niko kwenye hali iyo nyakat zingine hata nikiwa ktk mazingira ya kawaida. Je hali iyo inasababishwa na nini? Na kama kuna suluhisho naomba tuambiane.
Mzunguko wa damu mwilini hauko sawa. Nitafute kwa message private nikuelekeze namna ya kutatua changamoto hii
 
NJIA TANO ZA ASILI ZA KUONDOKANA NA MIGUU KUWAKA MOTO
Huu ni ugonjwa unaowasumbua watu wengi sana na Mara nyingi humfamnya mtu mwenye tatizo hilo kushindwa kusinzia japo anahisi kusinzia.

MIGUU KUWAKA MOTO
ni ugonjwa unaotokea ambapo katika mwili wa binadamu kutakuwa na matatizo kama kudhoofika kwa neva za pembezoni mwa mwili yani za miguuni hivyo kupoteza uwezo wa utendaji kazi wa neva miguuni, sababu zingine ni kama kutokuwa na mzunguko mzuri wa damu, kuwa na sumu nyingi mwilini,kurithi au mwili kushindwa kufanya kazi zake vizuri.

DALILI ZA UGONJWA WA MIGUU KUWAKA MOTO
Ugonjwa huu unadalili nyingi zikiwemo;
- Kuhisi ganzi,
- kuhisi kuchomwa na kitu chenye ncha Kali miguuni,
- kuhisi miguu kuwa na majimaji kwa ndani,
- joto Kali miguuni,
- kuhisi kama unaungua miguuni,kushindwa kushika au kubeba vitu na maumivu makali.

VITU/ MAMBO YANAYOWEZA KUPELEKEA MTU MIGUU YAKE KUWAKA MOTO
Kuna mambo mengi sana yakiwemo;
~UZITO MKUBWA WA MWILI(hii husababisha uti wa Mgongo kukaa tofauti na unavyostahili hivyo baadhi ya neva kukandamizwa na uzito wa mwili au misuli hivyo kusababisha miguu kupata maumivu na kufa ganzi.
~Matumizi ya baadhi za dawa zenye kemikali kwa muda mrefu au mara kwa mara mfanoDawaTB,HIVn.k
~Upungufu wa virutubusho mwilini hasa mkusanyiko wa VITAMINI B
~Magonjwa ya sukari na Shinikizo la damu , magoti ,Mzio na fangasi
~Matatizo ya Moyo
~Matatizo katika mishipa ya damu
~Ulevi wa kupindukia kwa muda mrefu

JINSI YA KUEPUKA UGONJWA WA MIGUU KUWAKA MOTO
~Kuwa na uzito unaoenda na na kimoja chako
~Fanya mazoezi ya mwili
~Kula chakula kinachokupatia virutubisho mwili hasa VITAMINI B
~Usafi wa viatu, sox na miguu
~ Ondoa sumu au kemikali mara kwa mara mwilini

MATIBABU
~Kula vyakula vyenye mkusanyiko wa vitamini B za kutosha
~ Fanya mazoezi ya mwili kama kukimbia, Kutembea n.k pia kufanya massaging
~Punguza uzito uliopitiliza
~Tumbukiza miguu katika maji ya vuguvugu yenye chumvi
~Tibu maradhi ya sukari.
 
Mwenye nia ya kupona na hatapona, kwa kufata masharti.

Kwani tiba hii ni kama kumwambia mtu mvivu fanya kazi, huwa kunakua na kaugumu fulani.
 
Ulifanyaje mkuu,tuelekeze
Mada hili inahusu matatizo ya Miguu kuwaka moto na namna ya kukabiliana nayo.

View attachment 367274

Maswali...
Nimekuwa na tatizo la miguu yote miwili kuwaka moto sana, hata kutembea nashindwa kukanyaga chini vizuri.

Nina umri wa miaka 38 na uzito wa 98Kg.Sijaugua ugonjwa mwingine zaidi ya malaria ya kawaida kwa mwaka mara mbili au moja.

Kwa ufupi sina mazoezi yoyote ya viungo nifanyayo.Sasa natembelea fimbo kama mlemavu.

WanaJF, Niangalizieni hili na kama kuna mtaalamu wa viungo humu basi anipe ushauri ni mazoezi gani nifanye kupunguza uzito.

Ushauri, Kinga na Tiba...

Mrejesho/Ushuhuda

Rudi hospital kwa dokta wako kamueleze tena atakubadilishia dawa. Kuna matatizo huwezi kupona kwa siku 5 au 10. Ni long term inahitaj uchunguzi wa kina na mfululizo wa dawa. Rudi hospital.
Habari wakuu,

Mimi pia nasumbuliwa na maumivu ya mgongo katikati, kwenye maungio ya mabega na KUELEKEA shingoni Hadi kichwani.
Muda mwingine yakizidi kichwa huuma pia Sana na nasikia kikigonga Sana kisogoni na shingo yote. Hii hupelelea mwili kuwa dhaifu, kukosa nguvu na kutamani nipate usingizi.

Naomba msaada kwa wataalam wanaojua hasa Hili Ni tatizo gani. Nipishapiga x-ray ya lumber dokta akasema pako vizuri.
Mwingine alinipima damu akasema Ina bakteria wa ulcer, nikatumia sawa lakini sikuona tofauti.
 
Tatizo hili nahisi linasababishwa na uzito, mkubwa bacteria na au fungus mwilini au miguuni.

Tufanye mazoez tena ya kukimbia, anza na zoez la viungo , kimbia kidogo kidogo, punguza Carbohydrates, kunywa maji mengi kila siku saa mbili asb, saa nne, saa saba na saa kumi mwisho.

Kiu za usiku labda ikitokea. Pendelea tangawizi, vitunguu maji na swaumu, karafuu, usinywe chai ya majani ya chai.

Tumia mbadala. Kula matunda mengi. Achana na nyama nyekundu. Ya ng'ombe hasahasa.
 
Tatizo hili nahisi linasababishwa na uzito, mkubwa bacteria na au fungus mwilini au miguuni.

Tufanye mazoez tena ya kukimbia, anza na zoez la viungo , kimbia kidogo kidogo, punguza Carbohydrates, kunywa maji mengi kila siku saa mbili asb, saa nne, saa saba na saa kumi mwisho. Kiu za usiku labda ikitokea. Pendelea tangawizi, vitunguu maji na swaumu, karafuu, usinywe chai ya majani ya chai... Tumia mbadala. Kula matunda mengi. Achana na nyama nyekundu. Ya ng'ombe hasahasa.
Ndugu yangu nimetingwa sanaaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mada hili inahusu matatizo ya Miguu kuwaka moto na namna ya kukabiliana nayo.

burning-feet.png

Maswali...
Nimekuwa na tatizo la miguu yote miwili kuwaka moto sana, hata kutembea nashindwa kukanyaga chini vizuri.

Nina umri wa miaka 38 na uzito wa 98Kg.Sijaugua ugonjwa mwingine zaidi ya malaria ya kawaida kwa mwaka mara mbili au moja.

Kwa ufupi sina mazoezi yoyote ya viungo nifanyayo.Sasa natembelea fimbo kama mlemavu.

WanaJF, Niangalizieni hili na kama kuna mtaalamu wa viungo humu basi anipe ushauri ni mazoezi gani nifanye kupunguza uzito.
MIGUU KUWAKA MOTO

Hisia za kuwaka moto kwa miguu yako zinaweza kusababishwa na uharibifu wa mishipa ya fahamu ya kwenye miguu, jina la kitaalamu tunaita Neuropatahy.
Ingawa matatizo mengi ya kiafya yanaweza kusababisha miguu kuwaka moto, ugonjwa wa kisukari unashikilia usukani.
Sababu nyingine ni unywaji wa pombe kupita kiasi.
Na sababu nyingine nyingi ni hizi zifuatazo;
-magonjwa sugu ya figo
-upungufu wa vitamini B12, folate, na vitamin B6
-kiasi kidogo cha homoni ya tezi dundumio/tezi shingo(thyroid hormone)
-Virusi vya UKIMWI na UKIMWI
-ugonjwa wa lyme
-ugonjwa amyloid polyneuropathy
-maudhi madogo madogo ya dawa au kwa jina la kitaalam tunaita drug side effects ambapo ni pamoja na dwa za magonjwa ya kansa, kuzidisha dozi ya vitamin B6 au dawa za virusi vya UKIMWI
-ugonjwa wa erythromelgia
-sumu za metali nzito kama mekyuri, na arsenic
-majeraha kwenye mishipa ya damu
-ugonjwa wa sarcoidosis
-ugonjwa wa guillain-barre syndrome(GBS)

Matibabu mengi ya tatizo hili yanalenga kuzuia uharibifu zaidi wa mishipa ya fahamu na kupunguza maumivu.
 
Kipimo gani inaweza kua msaada kutambua shida ipi inaleta shida?

VIPIMO KWA MTU MWENYE TATIZO LA MIGUU KUWAKA MOTO NI HIVI:

1. Electromyography(EMG)- hiki ni kipimo kinachochunguza utendaji kazi wa misuli.

2. Nerve Conduction Test- kipimo hiki kinachunguza utendaji kazi wa mishapa ya fahamu ya kwenye miguu.

Pia kuna VIPIMO VYA MAABARA ambavyo vyenyewe gharama zake sio kubwa ukilinganisha na hivyo vya hapo juu.
Vipimo hivyo ni pamoja na vipimo vya damu, mkojo, pamoja kipimo cha kuchunguza kimiminika cha uti wa mgongo..

Ni vyema mgonjwa akafika hospitali na kuzungumza na daktari kwa urefu zaidi juu ya tatizo lake na Daktari atachangua ni aina gani ya vipimo itafaa kwa mgonjwa kutokana na historia ya ugonjwa wake.

Na baada ya majibu ya vipimo kutoka ndipo daktari atachagua ni aina gani ya matibabu mgonjwa anastahiki kupata.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
VIPIMO KWA MTU MWENYE TATIZO LA MIGUU KUWAKA MOTO NI HIVI:

1. Electromyography(EMG)- hiki ni kipimo kinachochunguza utendaji kazi wa misuli.

2. Nerve Conduction Test- kipimo hiki kinachunguza utendaji kazi wa mishapa ya fahamu ya kwenye miguu...
Hospital zipi brother zenye vipimo hivyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuleni vitamins jamani maana most of us we don’t get enough vitamins through food ,tunatakiwa tu add supplements ,hiyo Dalili ya low vitamins b kwa uelewe wangu ,vizuri kama umepata Tiba
 
Hivi bongo mbona kila mtu daktari, aisee nendeni medical school mkaone maisha kule Msiwe rahisi kutoa maelezo ya kitabu, "wakati wewe sio taaluma yako",ndugu yangu nenda hospitali utapata ushauri na tiba.
 
Back
Top Bottom