Body mass index yangu ni 36,Nahitaji kujua pia ni aina gani ya mazoezi nahitaji kufanya,Kwani physician wamenishauri nisianze mazoezi makali kwanza.Nimewaona wataalam mbali mbali na dawa nimetumia lakini nafuu haipo kabisa.
BMI Yako tu inaonesha uzito ulionao Ni mkubwa hauendani na urefu wako. Ntafte kwa message private nikuelekeze namna ya kupungua uzito kiafya.
Mzunguko wa damu mwilini hauko sawa. Nitafute kwa message private nikuelekeze namna ya kutatua changamoto hiiAisee kwenu wataalam wa afya nina tatizo la kufa ganzi vidole vya mikono mara nyingi asubuh nikitoka kuamka najikuta niko kwenye hali iyo nyakat zingine hata nikiwa ktk mazingira ya kawaida. Je hali iyo inasababishwa na nini? Na kama kuna suluhisho naomba tuambiane.
Ni kweli mkuuMwenye nia ya kupona na hatapona, kwa kufata masharti.
Kwani tiba hii ni kama kumwambia mtu mvivu fanya kazi, huwa kunakua na kaugumu flani.
Mada hili inahusu matatizo ya Miguu kuwaka moto na namna ya kukabiliana nayo.
View attachment 367274
Maswali...
Nimekuwa na tatizo la miguu yote miwili kuwaka moto sana, hata kutembea nashindwa kukanyaga chini vizuri.
Nina umri wa miaka 38 na uzito wa 98Kg.Sijaugua ugonjwa mwingine zaidi ya malaria ya kawaida kwa mwaka mara mbili au moja.
Kwa ufupi sina mazoezi yoyote ya viungo nifanyayo.Sasa natembelea fimbo kama mlemavu.
WanaJF, Niangalizieni hili na kama kuna mtaalamu wa viungo humu basi anipe ushauri ni mazoezi gani nifanye kupunguza uzito.
Ushauri, Kinga na Tiba...
Mrejesho/Ushuhuda
Umefanikiwa mdau? Tujuzane nami ninachangamoto hiyo.Ulifanyaje mkuu,tuelekeze
Habari wakuu,
Mimi pia nasumbuliwa na maumivu ya mgongo katikati, kwenye maungio ya mabega na KUELEKEA shingoni Hadi kichwani.
Muda mwingine yakizidi kichwa huuma pia Sana na nasikia kikigonga Sana kisogoni na shingo yote. Hii hupelelea mwili kuwa dhaifu, kukosa nguvu na kutamani nipate usingizi.
Naomba msaada kwa wataalam wanaojua hasa Hili Ni tatizo gani. Nipishapiga x-ray ya lumber dokta akasema pako vizuri.
Mwingine alinipima damu akasema Ina bakteria wa ulcer, nikatumia sawa lakini sikuona tofauti.
Ndugu yangu nimetingwa sanaaaaTatizo hili nahisi linasababishwa na uzito, mkubwa bacteria na au fungus mwilini au miguuni.
Tufanye mazoez tena ya kukimbia, anza na zoez la viungo , kimbia kidogo kidogo, punguza Carbohydrates, kunywa maji mengi kila siku saa mbili asb, saa nne, saa saba na saa kumi mwisho. Kiu za usiku labda ikitokea. Pendelea tangawizi, vitunguu maji na swaumu, karafuu, usinywe chai ya majani ya chai... Tumia mbadala. Kula matunda mengi. Achana na nyama nyekundu. Ya ng'ombe hasahasa.
MIGUU KUWAKA MOTOMada hili inahusu matatizo ya Miguu kuwaka moto na namna ya kukabiliana nayo.
Maswali...
Nimekuwa na tatizo la miguu yote miwili kuwaka moto sana, hata kutembea nashindwa kukanyaga chini vizuri.
Nina umri wa miaka 38 na uzito wa 98Kg.Sijaugua ugonjwa mwingine zaidi ya malaria ya kawaida kwa mwaka mara mbili au moja.
Kwa ufupi sina mazoezi yoyote ya viungo nifanyayo.Sasa natembelea fimbo kama mlemavu.
WanaJF, Niangalizieni hili na kama kuna mtaalamu wa viungo humu basi anipe ushauri ni mazoezi gani nifanye kupunguza uzito.
MIGUU KUWAKA MOTO
Hisia za kuwaka moto kwa miguu yako zinaweza kusababishwa na uharibifu wa mishipa ya fahamu ya kwenye miguu, jina la kitaalamu tunaita Neuropatahy.
Ingawa matatizo mengi ya kiafya yanaweza kusababisha miguu kuwaka moto, ugonjwa wa kisukari unashikilia usukani.
Sababu nyingine ni unywaji wa pombe kupita kiasi.
Na sababu nyingine nyingi ni hizi zifuatazo;
-magonjwa sugu ya figo
-upungufu wa vitamini B12, folate, na vitamin B6
-kiasi kidogo cha homoni ya tezi dundumio/tezi shingo(thyroid hormone)
-Virusi vya UKIMWI na UKIMWI
-ugonjwa wa lyme
-ugonjwa amyloid polyneuropathy
-maudhi madogo madogo ya dawa au kwa jina la kitaalam tunaita drug side effects ambapo ni pamoja na dwa za magonjwa ya kansa, kuzidisha dozi ya vitamin B6 au dawa za virusi vya UKIMWI
-ugonjwa wa erythromelgia
-sumu za metali nzito kama mekyuri, na arsenic
-majeraha kwenye mishipa ya damu
-ugonjwa wa sarcoidosis
-ugonjwa wa guillain-barre syndrome(GBS)
Matibabu mengi ya tatizo hili yanalenga kuzuia uharibifu zaidi wa mishipa ya fahamu na kupunguza maumivu.
Hospital zipi brother zenye vipimo hivyo?VIPIMO KWA MTU MWENYE TATIZO LA MIGUU KUWAKA MOTO NI HIVI:
1. Electromyography(EMG)- hiki ni kipimo kinachochunguza utendaji kazi wa misuli.
2. Nerve Conduction Test- kipimo hiki kinachunguza utendaji kazi wa mishapa ya fahamu ya kwenye miguu...
Brother Nina shida hii sana, vpimo hivi vinapatikana hospital gani?
nenda kwenye hospital za rufaa kama kcmc,muhimbili, bugandoBrother Nina shida hii sana, vpimo hivi vinapatikana hospital gani?
Sent using Jamii Forums mobile app
Brother ahsante.Hivi bongo mbona kila mtu daktari, aisee nendeni medical school mkaone maisha kule Msiwe rahisi kutoa maelezo ya kitabu, "wakati wewe sio taaluma yako",ndugu yangu nenda hospitali utapata ushauri na tiba.