Tatizo la miguu kuwaka moto (neuropathy): Ushauri, Kinga na Tiba

Ndugu wana jukwaa. Nasumbuliwa na tatizo la miguu kukosa nguvu pindi nikitembea.

Ninapoanza kutembea nakuwa kama nimeshatembea kilometa 10. Ilianza kwa kutembea mwendo mrefu kdg ndio nachoka ila kwa sasa hata mita mia siwezi kutembea bila kupumzika.

Nimeshafanya vipimo vya organs zote zipo safi. Kwa kifupi nimepita hospital zote bila mafanikio. Naomba msaada kwa anaejua solution ya tatizo hili. Ni zaidi ya mwaka na nusu tangu tatizo hili lianze.
 
Pole Mkuu, Je wewe ni me au ke?, je uzito ni kiasi gani na urefu pia ni kiasi gani?, katika masaa 24 ni mkao gani unatumia zaidi kati ya kukaa na kusimama?.

Pole Mkuu, Je wewe ni me au ke?, je uzito ni kiasi gani na urefu pia ni kiasi gani?, katika masaa 24 ni mkao gani unatumia zaidi kati ya kukaa na kusimama?.

mimi me nina kg 75 sijawahi kupima urefu ila nipo kwenye kundi la warefu sio mfupi. Nilikuwa nafanya kazi ya ualimu so nilikuwa nakaa na kusimama. Kwa sasa muda mwingi nalala siwezi fanya chochote.
 
Mkuu kama umefanya hospital chek ups na bado hujaona ufumbuzi ni bora kuchungulia makanisani kwa maombezi maana sometimes kuna vitu majibu yake hayapatikani mahospitalini......hasa masuala ya miguu kuwaka moto, miguu kufa ganzi na haya ya miguu kukosa nguvu bila sababu........
 
hilo tatizo lako ni dogo nenda mtafute mch yeyote akuombee kwa jina la YESU utapona kabisa ndugu na kuhakikishia barikiwa
 
mimi me nina kg 75 sijawahi kupima urefu ila nipo kwenye kundi la warefu sio mfupi. Nilikuwa nafanya kazi ya ualimu so nilikuwa nakaa na kusimama. Kwa sasa muda mwingi nalala siwezi fanya chochote.

Mkuu Una umli gani labda kabla sijaanza kukushauli?
 
Ni lazimaunipeurefu wako,tofauti na hapo sijuwi namna ya kukusaidia.

mimi me nina kg 75 sijawahi kupima urefu ila nipo kwenye kundi la warefu sio mfupi. Nilikuwa nafanya kazi ya ualimu so nilikuwa nakaa na kusimama. Kwa sasa muda mwingi nalala siwezi fanya chochote.
 
tatizo ni je umeenda hospital kama hujaenda ebu Pima sukari, pressure na kafanye chest xray waangalie ukubwa wa moyo make nadhan unapata heart failure.

Lakini pia uzito wako ni mkubwa kulinganisha na urefu. Punguza uzito kidogo walau 65.

But cha kuzingatia pima routine presure na sukari na kafanye chest xray.
Vp upo mkoa gani may be naweza kukuona
 
Mkuu nipo Tanga. Nimeshafanya vipimo vyote unavyosema. Sina sukari na moyo upo safi. Nilionana na doctor bingwa wa moyo nikafanya ECG, Xray na vipimo vingine. Ushauri walionipa ni kufanya mazoezi. Naendelea na mazoezi lakini bado hali. Sio nzuri.
 
ok safi fanya mazoezi. Na punguza sana kula vyakula vya wanga sana wali, ugali, chips .
Punguza sukari kwa kiwango cha juu
acha soda za kila wakati
 
Asante sana Mzizi mkavu nimepata kitu kwa ajili ya nyayo kuwaka moto.God bless
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…